Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Nilitaka kuanzisha uzi wa namna hii baada ya kwenda mkoa mmoja hivi. Yaani hata kama umeinama hujamuona mtu utashangaa mtu kasimama analalamika hujaitikia salamu yake na humjui hakujui very boring

Mwingine yupo mbali mita kadhaa nae analazimisha salamu kelele kama zote hata hamfahamiani
 
Nilitaka kuanzisha uzi wa namna hii baada ya kwenda mkoa mmoja hivi. Yaani hata kama umeinamna hujamuona mtu utashangaa mtu kasimama analalamika hujaitikia salamu yake na humjui hakujui very boring

Mwingine yupo mbali mita kadhaa nae analazimisha salamu kelele kama zote hata hamfahamiani
🤣🤣🤣🤣🤣Umenichekesha!
 
Aah mtongozo wapi ndio salamu zenyewe hizo zinazochosha ubongo.

Ukiwa na Mimi utaona kila kitu. Ni rahisi, hakuna kitu kitakuchosha.
Ni Raha tuu!

Mimi sipendi mazoea Zoea ya kijinga, Ila kumsalimia MTU iwe NI Kwa ishara, Au habari za Mchana, au jioni, hiyo kwangu sio tatizo,
Ni rahisi kunizoea Ila sio mazoea yaliyopitiliza.

Mazoea ya kujua mambo yangu, mahusiano yangu, nyumba yangu, Ndugu zangu, kimsingi ukishajiingiza kwenye umbeya kwangu lazima utanichukia na kuniona ninadharau,
Bahati nzuri nitakujibu palepale, majibu makavu
 
Utafanya jamii na wanaJF wanione nimeoa Mwanamke asiye na tabia njema, hivyo ni Bora ubakie palepale ili nieleze kuwa MKE wangu ni mgeni Kutoka Nchi za Ulaya Huko hajui Kiswahili vizuri, ndio maana anashindwa kusalimia, alafu utapewa nafasi ya kupunga angalau kamkono na kutabasamu tuu.
Hilo halitokushinda Darling 😊
Kha😂😂😂
 
Hupendi salamu, ila umeanza na "habari wana jf" hufikirii kama utatupotezea muda kukujibu!?
Hiyo ni opening statement, ata kwenye barua formal tunaanza na opening statement.
 
Unajua unaweza jiona una msimamo kumbe umejawa kiburi au ukajiona upo sahihi kumbe utoto na ushamba unakusumbua. Nasikitika unatuonyesha udhaifu wa wazazi wako hujui thamani ya salamu kwakua unahisi atakaekuzika ni yule ndugu yako tu unaemjua.

Watu kama nyie mnakuaga hamna mchango wowote kwenye familia alafu ndio wakwanza kukaza fuvu.
 
Huwa inakera sana mtu kushindwa kufuata mambo yake anasalimia salimia mara kuulizia ulizia hovyo. Mimi napenda ukimya na nafurahi mtu akiwa busy na mambo yake

Just itikia then chill. Plus si wote wanakereka labda ww.
 
Unajua unaweza jiona una msimamo kumbe umejawa kiburi au ukajiona upo sahihi kumbe utoto na ushamba unakusumbua. Nasikitika unatuonyesha udhaifu wa wazazi wako hujui thamani ya salamu kwakua unahisi atakaekuzika ni yule ndugu yako tu unaemjua.

Watu kama nyie mnakuaga hamna mchango wowote kwenye familia alafu ndio wakwanza kukaza fuvu.
Mkuu, muda ni fedha, uwezi tumia nusu ya siku yako kuulizana mambo ya kipuuzi, mtu anakuuliza haujambo wakati uko road, ungekua na shida si ungekua hospital au rumande. Tumia kichwa kufikiri siyo kusukia rasta madam
 
Jamaa ameanza kuzeeka sasa shikamoo nyingi zinamuuma. Uzee sio dhambi wewe

Kwa kweli uzee bhana!
Siku hizi nasalimia Shikamoo Uncle, mwanzoni nilihisi kama wanakosea Kwa bahati Mbaya, lakini kadiri siku zinavyoenda nimethibitisha nimekua Mzee SASA.

Haiwezekani niende sehemu nyingine nisiyojulikana alafu Watoto wa eneo hilo wanisalimia Uncle.
Hiyo ilikuwa taa nyekundu kuwa uzee hauko mbali
 
Jamii za vijijini zinaamini katika ujamaa , communalism. Kwahiyo ni kawaida sana hata kukukaribisha ule japo hawakujui. Wanaamini binadamu wote ni ndugu na ni kitu kimoja kama familia moja. Ila mijini Ubepari umetutawala. Kijijini ukienda Halafu Usimtembelee mtu anasikitika sana. Na unapoondoka wanapenda uage na watakupatia chochote kitu. Tofauti n mjini mtu asipokuja unafurahi na unaona angekupotezea muda tu.
 
Kwa kweli uzee bhana!
Siku hizi nasalimia Shikamoo Uncle, mwanzoni nilihisi kama wanakosea Kwa bahati Mbaya, lakini kadiri siku zinavyoenda nimethibitisha nimekua Mzee SASA.

Haiwezekani niende sehemu nyingine nisiyojulikana alafu Watoto wa eneo hilo wanisalimia Uncle.
Hiyo ilikuwa taa nyekundu kuwa uzee hauko mbali
Ni kama mimi tu, shikamoo zimekuwa nyingi mpaka kero. Naamkiwa mpaka na vijana wakubwa. Naamkiwa mpaka kwenye sms. Kwenye bus unaambiwa "mzee onyesha tiketi". Unajiuliza hii ni mzee ya kishkaji au ndio uzee tayari?!

Nilikuwa naboreka ila hakuna jinsi. Ila kwa vile sijafikisha 40 bado nakula kula ujana
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kishamba sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract alafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
Fikiria upo katika mazingira ya ugenini,umepatwa ajali unataka kusema watu wakuache mpaka waje wanaokujua ? Acha maringo salimia watu
 
Back
Top Bottom