Mfano gani huo sasa mkuu, salamu ina shida gani? sisi huku vijijini tunaishi kama ndugu na wote tunafahamiana. Lazima tujuliane hali, hata kama napita nje ya nyumba ya mtu nitamuita nimsalimie. Tukiona mgeni ni kama tumemuona ndugu yetu, na ukiwa na shobo wanakushangaa sana. Huwa tunapokea wageni toka mikoa mingine na kupitia salamu wanakuwa sehemu yetu. Hata hao volunteer toka nje wakija, wanajiblend kirahisi kupitia salamu. Wewe wala hutokaa huko sana, salimia watu, then utarudi ulikotoka. Huwezi lazimisha mabadiliko kwa namna hiyo.