Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

"Habari yako? umeshindaje? za mihangaiko? wanao hawajambo? vipi huko kwenu umewaachaje? unaelekea wapi? vipi huko mjini hawajambo? Naona unazidi kupendeza tu,Sisi tupo bhana,maisha magumu tu"
Salam kama hii ikutane na mtu wa Dar, jamani watu wa Dar wanajua kuongea haraka..hujajibu yeye keshaongea, kashauliza mara mia kidogo....mimi huwa nasikiliza akimaliza ndio najibu.
 
Sasa ukija kwetu maeneo ya unyakyusani mtu mmoja mnasalimiana nusu saa, akija mwingine hivyo hivyo..ukienda kusalimia siku ya kwanza umefika inakuwa maalumu kusalimiana alafu mengine yanafuata.
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kishamba sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract halafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
Sijaona Tatizo la kusalimiwa kama ni shida...

Ungesema mtu kujenga mazoea ya lazima hapo NDIO shida....

Salamu sioni kama ni shida mkuu...
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kishamba sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract halafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
Ungeliingia jeshi hata kwa mujibu wa sheria (short term), usingeongea haya kwa sababu salamu ni lazima na siyo ombi wala hiyari.

Usiposalimia ni kosa na ukisalimiwa usiitikie ni kosa pia na makosa hayo yanakutia jela na kutumikia adhabu ya kifungo.

Katika mazingira ya vijijini salamu hubeba thamani ya bima au akiba ya benki, kwa sababu baadaye salamu zako hizo kwa watu hukulipa.

Mgeni anayesalimia watu huwekwa kwenye kundi la watu wenye heshima, upendo na wenye nidhamu.

Mgeni anayewapita kimya kimya watu huonekana jeuri, mbinafsi na mjivuni.

Nimesema salamu ni kama Bima ama akiba ya amana nimemaanisha kuwa, unapopata tatizo lililo juu ya uwezo wako wa kifedha maeneo hayo, jamii itakulipa kwa msaada watakaoutoa kwako kwa upendo na unyenyekevu tena bure.

Sasa wewe endelea na hizo tabia zako mbofu mbofu za kuwapita watu kimya kimya kama chizi, utakuja kuona matokeo yake yalivyo hasi, hadi utakuja kujidharau mwenyewe na kujiona kuwa kumbe wewe si chochote si lolote mbele ya hao wapori pori kama unavyowaita wewe!

Salamu ni ishara kuonesha dhamira ya ushirikiano, ni nidhamu na ni heshima unayoonesha kwa mtu pia.

Ogopa sana jamii kukuchukulia tofauti.
 
Bushi kawaida hata aliyekuzidi anaweza kukuamkia.
Mjibu Mimi mtu wa mikausho mikali sana .
Nashanga sana hapa mjini unakuta mtu mzima ananiamkia shikamoo huwa siwaelewi kabisa .
 
Kwani mzungu ndio Nani sasa Sasa Hadi awe Kama special case?kwanza ushawahi ona huyo mzungu anasalimia kila mtu,anasalimia mtu mwenye kazi nae.
Nimetaja wazungu kwa sababu huo utamaduni wa kutosakimiana ndio wakwao.
Wazungu ndio wenye mila ya kutosalimiana wakiwa huko uzunguni.
Ila wauzungu hao wakija kwetu hizo mila zao ambazo wewe unawaiga ilihali ukiwa kwenu huko namanyere huwa wanaziacha.

Tumeshuhudia viongozi wakuu wa nchi wakienda ziara mikoani wanasimamisha magari ili kusalimiana na wnavijiji halafu we masikini kapuku usiye na kitu unavimbisha matako hutaki kusalimia wanao kusalimia.
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kishamba sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract halafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
Simu za mvua vip inanyesha hukooo
 
Umenikumbusha mbali sana.

Kuna kipindi nilienda likizo Mwanza, nikakuta kuna vitoto fulani barabarani nikavipita tu. Vitoto vidogo tu, hata siku vi register.

Basi wee, vile vitoto vilimind vibaya sana. Vikawa vinasema Kisukuma kwamba huyu mbona kapita tu kama hajatuona.

Nilishangaa sana, nikaja kugundua siko Dar. Halafu nilishanmgaa kwa sababu nilitegemea wao kwa sababu ni wadogo, kama wana mind kusalimiana sana wangeanza kunisalimia wao.

Nilikuja kugundua kuwa kum recognize mtu pale ni kitu cha muhimu sana.

Ila, unaweza kuvipita vitoto hivi, halafu ukakutana navyo ukaambiwa ni vitoto vya shangazi yako fulani, vinakujua ila wewe huvijui.

Sasa hapo muhimu kusalimiana tu.

Tatizo bora salamu zingekuwa fupi zile kama za Kiswahili "Za saa hizi?" unajibiwa "Salama" unapita.

Msukuma salamu anakusimamisha, ukimaliza kumtajia ukoo wako, anakuuliza na mkeo hajambo, na watoto? Na hapo hapo anaunga stories, kama una haraka unachelewa.
Aisee kabisa Yani na hawana salamu fup na kilamtu asalimiwe pekeyake ukikuta wapo wengi uanze kuwasalimia mmoja mmoja
 
Aisee kabisa Yani na hawana salamu fup na kilamtu asalimiwe pekeyake ukikuta wapo wengi uanze kuwasalimia mmoja mmoja
Hahaa,

Wakihamia mijini wataacha tu.

Kuna Uncle mmoja alikuwa hivyo hivyo, ti na yeye baada ya kukaa mjini sana akawa analalamika watu wanaosalimia sana.

Unajua kuna spidi fulani ya maisha ikiongezeka mambo kama hayo yanaondoka yenyewe.
 
Kabisa ila inabidi kama hujazoea ujizoeshe mfano tumezoea kusalimia za sahiz then unaamkia ukimwambia mtu mzima za sahiz hakuelew anataka shikamoo 😀 alafu wana Ile mnapiga story wee anakaribia kuondoka ndo anasalimia 😂😂😂
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kishamba sana,
umesema upo shamba, bado unalalamikia code za kishamba.. ulitaka code zipi wakati upo shamba??? next time uje na watu wako wa mjini uwamwage huko halafu waambie wasikusalimie, simple.
 
Back
Top Bottom