Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Ndio maana nikamwambia huyo no limbukeni na hajatembea. Binafsi nilikuwa sisalimii watu lakini baada ya kukaa na wapoli Poli nimejifunza kusalimia watu.

Kuna siku tulienda na jamaa yangu sehemu wakati wa kurudi tukapotea Giza likaingia alafu Piki Piki ikaisha mafuta. Ikabidi tutembee kufika sehemu tukasikia mbwa wanabweka ikabidi twende kwa kufuata sauti za mbwa maana giza lilikuwa tororo kufika kwenye mji jamaa akatumulika na tochi, sikumfahamu huyo jamaa Lakini yeye alikuwa ananifahamu;
Ilibidi nimuulize mbona ananifahamu alafu simfahamu. Akanikumbusha Kwa kuniuliza wewe si ndio ulipoteza ufungu wa gari nyeupe nikamwambia ndio Mimi; jamaa akatuuliza mnashida gani tukamweleza akachukua mafuta akatupa tukapewa na maziwa tukanywa.
Wakati tunaondoka akasema nimekupa mafuta kwa sababu hujisikii, unasalimia watu na lift unatoa. Akatuelekeza njia tukasepa

Imagine kama ningekuwa kama mleta mada siku hiyo ingekuwa je?
 
Wewe mwenyewe umeanza kwa kutusalimia "habari wana jf"... Utatupotezea muda wetu kukujibu na pia haitasaidia.πŸ˜€
Nb: Salaam ndio mwanzo wa kujuana
 
You are so bitter
Huli ukashiba au?
 
Kwa jibu hili ulikuwa na maada Gani sasa kupost thread ya namna hii, si ungebaki na Imani yako tu kama ulilijua Hilo. Umeleta mada ukitegemea attention na support lakini imekuwa vice versa umekutanishwa na vikombe
Umebaki kupaniki tu
Mkuu, umeuliza swali la muhimu sana. Ukileta uzi humu JF, ina maana unahitaji mjadala na kupata mtazamo na uzoefu wa members wengine. Lengo ni kujifunza na kuwekana sawa. Sasa mleta mada anataka kutudictate badala ya kuacha mjadala uende vyema
 
Wewe mwenyewe umeanza kwa kutusalimia "habari wana jf"... Utatupotezea muda wetu kukujibu na pia haitasaidia.πŸ˜€
Nb: Salaam ni ndio mwanzo wa kujuana
Hakuna hoja kwenye Uzi wake Bali ni majigambo tu na kujiona yeye ndio kontawa ulimwengu huu. Kaanza na salamu ya nini hapa wakati anaikemea? Au anatujua sisi hadi atusalimu??
 
Mtuache,usitake tuige tabia zenu huko,kila kukicha kila mtu yuko mbio,barabarani utadhani anafukuzwa,huo muda wa kusalimia atautoa wapi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…