Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Dah sisi kwenye tunafundishwa kua tupende kusalimiana sanaa ata kma umepita na kupituka ukirudi msalimie muislamu mwenzako tena

Dah we hujui kua Salamu huleta upendo na faraja baina ya watu
Dunia imeharibika watu wengine nuksi ukiwasalimia unapata mikosi tu
 
Habari wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract alafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
Mikoani bado wana elements za kibinadamu na uungwana .
Huku mjini tumeshakengeuka , ndugu qkija kukusalimia unaona kaja kudoea na kuivurugia bajeti .
The only time born town ana value salamu na uwepo wa ndugu ni pale anapopata matatizo.
 
Umeona ehe, kuna kitu hakipo sawa kwenye undeshaji wa maisha yetu, wakati ni fedha
Imagine mtu humjui,upo zako na mawazo yako kibao kichwani unasikia "habari yako?Aghhhrrrrrr🤯🤯🥵🥵..Kweli huwa naboreka, jamani salamu ziwepo palipo na tija nakuumga mkono kabisa wazo lako
 
Imagine mtu humjui,upo zako na mawazo yako kibao kichwani unasikia "habari yako?Aghhhrrrrrr🤯🤯🥵🥵..Kweli huwa naboreka, jamani salamu ziwepo palipo na tija nakuumga mkono kabisa wazo lako
Alafu ukute ata hajasafisha kinywa, gundu juu ya gundu
 
Ukiwa na umri wa Bi. Mkubwa wako utaelewa akifanyacho.
Mjini Salamu inaweza Isiwe na maana Sana Kutokana na wingi wa Watu lakini Kijijini salamu ni muhimu Mno
Nasalimia,lakini siwezi salimia kila mtu!eti naambiwa nitakosa watu wakunizika Sasa hizo shida zangu kweli?hakuna maiti uliyomkosa mzikaji
 
Nasalimia,lakini siwezi salimia kila mtu!eti naambiwa nitakosa watu wakunizika Sasa hizo shida zangu kweli?hakuna maiti uliyomkosa mzikaji

Shida haipo Kwa maiti, shida Ipo Kwa wenye maiti kama Mumeo, watoto, nduguzo.
Alafu bahati Mbaya hatujui ni wapi Mauti itatupata, huo ndio mtihani.

Ukifika mazingira ya kusalimia Watu salimia Watu hata kama ni wote, hautopungukiwa na kitu.
Ukifika mjini mazingira ya kila MTU na time yake fanya vivyohivyo.

Siku hizi kuzika ni gharama Sana sio kama zamani
 
Kwetu salamu ni kukumbatiana na kupiga magoti sasa kama una haraka zako utakoma. Nyinyi watu wa dar muna matatizo hamsalimiagi ishiiiiiy!
Imagine una hug watu wasiosafisha vinywa, hawaogi na hawapaki deodorant
 
Tumesema tusalimiane Kama Kuna haja ya kufanya hivyo!hayo Tena ya kuvumiliana Hapana kwa kweli😁

😀😀😀
Utakwama, Ila fanya utakavyo,

Mimi mwenyewe sipendi masuala ya kusalimiana salimiana Ila nasalimia kulingana na mazingira.
Kutokupenda Jambo Fulani haikufanyi usilifanye Kwa ajili ya wengine, huo unaitwa ubinafsi.
 
Jifunze kuzowea tu Mkuu.

Sasa ukienda kule kwetu Pwani ndo utachukia zaidi kwani kule hatuna kawaida ya kupitana popote pale we kila unayemuona hata kama humfahamu basi salamu ni kawaida si njiani wala kwenye usafiri wa Umma.

Yaani usiposalimia mtu anakushangaa.
 
Back
Top Bottom