Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Kuna Miafrika mitaahira inafikri kuiga mila za Wazungu ndio maendeleo hayo! Utakuwa umelelewa kwenye li familia la hovyo hovyo, pengine la Singo mazafanta!
 
Fikiria upo katika mazingira ya ugenini,umepatwa ajali unataka kusema watu wakuache mpaka waje wanaokujua ? Acha maringo salimia watu
huko mikoani na vijijini watu wamekua wabaya zaidi, kama una experience ya kusafiri omba Mungu usipate tatizo.
 
Kuna Miafrika mitaahira inafikri kuiga mila za Wazungu ndio maendeleo hayo! Utakuwa umelelewa kwenye li familia la hovyo hovyo, pengine la Singo mazafanta!
Jibu hoja mkuu, ujinga unaondolewa na elimu, usione aibu kuwa mjinga, njoo utibiwe
 
Usiwe hivyo mkuu, jifunze kuishi kulingana na mazingira.itikia salamu hizo Wala usichoke ikiwezekana Anza wewe ukiwakuta.

Watu wako very hospitality, hukaribisha chochote bila kinyongo au kumjaribu mtu, hawana unafiki
Muache ajifanye anajua watamsusa mpaka atashangaa. Yaani huyu ni mshamba kweli kweli. Yaani hapo kajiona mjanjaa
 

Uzee ndio huo Mzee 😂😂😂

Wazee wenyewe haelewi imekuaje kuaje wamekuwa wazee kwani wanaona walizaliwa juzi tuu hapa. Yaani hawaelewi kabisa
 
Mkuu, muda ni fedha, uwezi tumia nusu ya siku yako kuulizana mambo ya kipuuzi, mtu anakuuliza haujambo wakati uko road, ungekua na shida si ungekua hospital au rumande. Tumia kichwa kufikiri siyo kusukia rasta madam
Kama muda ni hela na unautumia vizuri leo umefika kwenye hizo fedha
 
Kwa hivyo ukiwa shamba ukaona watu wanakunya vichakani na wewe ukanye vichakani, siyo kuwajengea vyoo? Is it? Hapo ndipo akili yako ilipofikia mwisho?
 
Umenikumbusha kabila la WANYIHA huko mbozi mkoa wa songwe. Yaani lazima mtu akusalimie salamu ndefu then akwambie pole na kazi, Sasa mimi hicho kipindi hata kazi sina, nabaki kushangaa tu ni kazi gani hii nayopewa nayo pole?? Au hawa watu wananipaga kazi za usiku bila kujua, Maana nao ni wataalam kwelikweli Hawa wanyiha
 
Kwa hivyo ukiwa shamba ukaona watu wanakunya vichakani na wewe ukanye vichakani, siyo kuwajengea vyoo? Is it? Hapo ndipo akili yako ilipofikia mwisho?
Mfano gani huo sasa mkuu, salamu ina shida gani? sisi huku vijijini tunaishi kama ndugu na wote tunafahamiana. Lazima tujuliane hali, hata kama napita nje ya nyumba ya mtu nitamuita nimsalimie. Tukiona mgeni ni kama tumemuona ndugu yetu, na ukiwa na shobo wanakushangaa sana. Huwa tunapokea wageni toka mikoa mingine na kupitia salamu wanakuwa sehemu yetu. Hata hao volunteer toka nje wakija, wanajiblend kirahisi kupitia salamu. Wewe wala hutokaa huko sana, salimia watu, then utarudi ulikotoka. Huwezi lazimisha mabadiliko kwa namna hiyo.
 
Nimecheka kwa nguvu sana, ni code za kipori pori sana
 
NAKAZIA
 
Mkuu, huwezi lazimisha mimi nitafakari au kuchakata vitu au mambo kwa namna yako, wewe amini unacho aminini na mimi naaamini ninacho amini
 
Hii sio sawa. Kijijini wanajua thamani ya Salam. Acha tuendelee na utamaduni wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…