Kwanini watu wanaiponda sana wilaya ya Rombo kwa ulevi lakini bado kuna maendeleo?

Kwanini watu wanaiponda sana wilaya ya Rombo kwa ulevi lakini bado kuna maendeleo?

Unajua Hii wilaya kwanza kijiografia ipo mwinuko kati ya mita 1300 hadi 2200. Kuna hali nzuri sana ya hewa hilo halina ubishi.

Watu wanaposikia hii wilaya kitu cha kwanza wanajua watu wa huko ni walevi choka mbaya kiasi kwamba hakuna maendeleo yeyote. Ila laiti wangejua Hii wilaya kila mtumishi wa umma aliyeajiriwa iwe kwenye shule, benki au polisi hawatamani kuhama wasingeibeza.

Ni kweli pombe inanyweka tena sana kuanzia pande za kikelelwa mpaka mamsera mashati, usseri ndani ndani pombe inanyweka ila watu wanapadis ohooo Rombo hakuna maendeleo kisa ulevi.

Na huku kunywa pombe kunachangiwa na upatikanaji rahisi wa malighafi ya kutengeneza pombe ya mbege ambazo ni ndizi pamoja na hali ya hewa (baridi) ila maendeleo yapo na watu wapo wanakimbizana kuitafuta shekeli kwa udi na uvumba. Iwe ni kwenye biashara kilimo n.k mfano Kilimo cha viazi Rongai, mahindi japo sio sana n.k.

Viwanda vya mbao vipo kuanzia kikelelwa tarakea hapo kwa maulid peleka hadi Mashima usseri n.k. kwa takwimu za haraka haraka za pale ofisi ya Rongai kuna karibia viwanda 200 ambavyo vipo registered katika kuchakata mbao.

Kama msitu upo Norh Kilimanjaro forest plantation wenye almost hectare 8000 na point.
Utalii wa mlima Kilimanjaro n.k.

Kwa vile tupo mpakani hapa siku za weekend wakenya wanakuja ku spend na familia zao kupata kitimoto ,bia au ugali samaki snow cape AU resort inn. Kwa kifupi wakenya kutoka kwenye miji ya kimana, oloitoktok, illasit n.k

Sehemu yao ya kujivinjari ni tarakea, Mashima au mashati huko....maana huku bia ni rahisi sana ukilinganisha na kwao. Kwa kifupi kiuchumi wilaya ya Rombo inajiweza. Msipadis sana kama hamjawahi fika naomba mfike.

Haters karibuni kwa mapovu
Picha yako wewe tuone ulivyolewa na picha ya mji wenu.
 
Mtoa mada amesema kweli kabisa, kwa ujumla rombo na maeneo mengine ya Moshi ni mazuri mnooo, yani migombani huko unakuta mijumba ya maana.
Ad magorofa yamo ya kutosha..hakuna uhaba wa madarasa na vitendea Kazi vyake..pia imeunganishwa kwa lami kuanzia Moshi mjin ad tarakea. Hata barabaran za mtaaan zinapitika.. kipindi Cha mvua ndo utakuta barabara chache zenye utelezi tu
 
Back
Top Bottom