Makari hodari
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 3,339
- 6,666
Habari za leo wanajamvi!
Natumaini wote ni wazima wa afya na tunaendelea vyema kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa letu ingawa ni kwa kasi ya kobe lakini si haba, tukishirikiana na serikali yetu tukufu.
Kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni kama wewe/nyinyi ni wafuatiliaji/mfuatiliaji/wadadisi/mdadisi wa mambo Kumekuwa na wimbi au tabia ya watanzania wengi hususani vijana kuthubutu bila woga kujifanya na kutamka mbele ya umati kwamba yeye au fulani ni mwanajeshi au askari.
Wapo wanaofika mbali kufanyia watu ubabe au unyang'aji na huku wakitoa vitisho, dhihaka na kujinadi au kutafuta sifa kwamba yeye/wao ni mwanajeshi/wanajeshi au polisi. Bila hofu wala uoga mwingine anadiriki kusema au kutafuta sifa kwambe yeye ni member wa "TISS" (Mwanajeshi/afisa Usalama wa taifa) na anathubutu kuzisambaza taarifa zile bila woga dhidi ya fulani au yeye mwenyewe. Inamaana vitengo hivyo vimekuwa poapoa tu kiasi kwamba hata ule usiri haupo tena? Yaan TISS siku hizi anafahamika kizembe tu kama katibu kata wa kawaida au mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
Mnafkiri kwanini ongezeko la watu wajingawajinga wa namna hii linakuwa kwa kasi hapa nchini?!...Ni ukosefu wa ajira kiasi kwamba mtu/watu wanaona huko ni sehemu bora na salama zaidi. au kutafuta kuogopeka au ni kutest mitambo kama waswahili wasemavyo uone nini kitatokea? Au wao wenyewe TISS, na vyombo vingine vya usalama wanaachia hali hii iendelee na vitengo hivi nyeti viendelee kuonekana ni kitu cha kawaida au mihemko tu?
Sijui kama watu wa namna hii kama wanaitambua hatari yake pale ambapo wao wenyewe wakiamua kukuchukua/kuwachukua na kukuweka/kuwaweka chini ya ulinzi kwenye machimbo yao wanayoyajua wao wenyewe na serikali yao.
Tafadhali TISS ni vyema mkashughulika na hili rasmi ingawa mnashughulika na critical issues, this is terrible!
Nakupenda Tanzania! 🇹🇿❤💪🏾