Kwanini Watu wenye sifa nzuri kama uzuri na uhandsome au utajiri husemwa kwa mabaya? Je, ni wivu kwa waliokosa sifa hizo?

Aaiiii hata wewe MNEK?? Kwanza badili hiyo avatar inanitisha mie 😂😂
 
Hawa wapuuzi huwq wana pretend wanakuchukia but ukiwakazia vizuri utawaona walivyo dhaifu, huanza kufanya kila unachofanya ni viumbe dhaifu sana kisaikolojia.
 
Huko uzunguni kwenyewe waswahili washafika siku hizi... Nilishangaa sana kukuta vijiwe vya bodaboda Masaki, Mbezi, Upanga na Mikocheni.... Mama ntilie nao bila haya wamejazana huko, sasa sijui ni kutafuta sifa anafanyia biashara Masaki, Mikocheni na Upanga au ni kweli kuna walaji mabarabarani na wapanda bodaboda huko... Mungu na wao wenyewe ndo wanajua.

Na hao ndo huleta uswahili uzunguni hao... Nafkiri hili nalo litizamwe.
 
Sijui kwa hao wengine ila ukiona mwanamme unaanza kujiita handsome boy(wewe ndo unajiita sio waanawake wanakuita) mara nyingi unakuwa hatua moja kabla ya kuanza kuliwa jicho. Wengi wanaojiita mahandsome ukiwauliza demu wako yuko wapi huwa hawana majibu ya kuridhisha.

Cc. Ni yule yule super handsoome
 
Hapa tunazungumzia wale natural handsome kwa kuzaliwa na sio kujiita.

Yaani umefika tu Duniani unakuta uko hivyo na hujajichagua.

Sasa wenye sura ngumu kama wewe huwa kufidia mapungufu yenu huanza kuchafua wenzao kama unavyofanya hapa.

Mleta mada hakukosea ni jambo linalotokea kweli.
 

Kikawaida hakunaga Handsome anayejiita Handsome.
Ila kuna wale ambao hushindwa kutofautisha utanashati na ûhandsome.
Wale wanaume ambao wengi wao sio Handsome semà hujipodoa na kujivika kisha hujiita Handsome na kutenda mambo kama wanawake. Wengi wao ninaowajua ambao baadhi yao ni maarufu kwenye media hasa wasanii hawapo kwenye nafasi hiyo.

Ni kama wanawake. Wapo wanaojiremba na kujiona wazuri wakati kiasili wao sio wazuri.
Wanashindwa kutofaurisha urembo na uzuri
 
Wivu tu ni kawaida ya binaadamu hawapendi kuona vitu vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…