Kwanini watumiaji wa simu za itel, Tecno na Infinix wanadharaulika sana Dar?

Mimi ni fundi simu upande wa hardware na ni mzoefu kwa miaka 10 na 90% ya simu ninazotengeza ni tecno, infinix na itel. ni kweli kila simu inaharibika na kila siku napokea simu zenye matatizo mengi na matatizo mengi ni yale tuliyo yazoea.
Lakini kuna mengine ni mapya kulingana na teknolojia inavyo kuwa.

Lakini kuna matatizo ambayo nimeyagundua kwenye hizo simu tatu kwa hii wiki nimepokea
Simu karibia 15 ambazo zimezima Peke yake na kwa maelezo ya wateja wanasema walikuwa wameziweka tu ndani.

Na kwa sababu mbali mbali Na mwisho wa siku wakakuta zimezima peke yake Na hizo simu mara nyingi huwa nikizipima na nakuta zina umeme mdogo ambao hauwezi kuwasha simu. hata ukibusti betri haziwaki kabisa hata ukiweka betri mpya zenye moto wa kutosha haziwaki na hata tukichomeka kwenye kwenye computer ili kuziflashi zinakuwa hazionekani kabisa. Na hivyo ndivyo zinakuwa imekufa moja kwa moja.

Lakini baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu nimegundua hizo simu nyingi zinazozima kwa namna hiyo ni zile simu zilizo Isha warranty na nimeyagundua hizo simu ni zile toka zimetengenezwa baada ya mwaka mmoja na ikikaa siku 30 ikiwa imezima chaji hiyo simu ujue itakufa moja kwa moja.

Na nimegundua hiyo inatoka na mikataba mibovu waliyo Ingia hayo makampuni yanayo wauzia software kwamba wao wanao wauzia software wanawapa security ya mwaka mmoja tu.

Kwahiyo ushauri wangu kwa watumiaji wa infinix tecno na itel usiiache simu yako iishe chaji kabisa na ikae siku 30 bila kuichaji.

Wakati tunaendelea kutafuta solution.
Huu ni uongo,
Jamaa umecopy hii kitu kwa uzio usio onekana
Acha copying and paste kwani ungedirect wadau kwenda kwenye uzi husika umpe credit jamaa ungepukiwa nini!??

Acha wizi dogo
 
Mimi ni fundi simu upande wa hardware na ni mzoefu kwa miaka 10 na 90% ya simu ninazotengeza ni tecno, infinix na itel. ni kweli kila simu inaharibika na kila siku napokea simu zenye matatizo mengi na matatizo mengi ni yale tuliyo yazoea.
Lakini kuna mengine ni mapya kulingana na teknolojia inavyo kuwa.

Lakini kuna matatizo ambayo nimeyagundua kwenye hizo simu tatu kwa hii wiki nimepokea
Simu karibia 15 ambazo zimezima Peke yake na kwa maelezo ya wateja wanasema walikuwa wameziweka tu ndani.

Na kwa sababu mbali mbali Na mwisho wa siku wakakuta zimezima peke yake Na hizo simu mara nyingi huwa nikizipima na nakuta zina umeme mdogo ambao hauwezi kuwasha simu. hata ukibusti betri haziwaki kabisa hata ukiweka betri mpya zenye moto wa kutosha haziwaki na hata tukichomeka kwenye kwenye computer ili kuziflashi zinakuwa hazionekani kabisa. Na hivyo ndivyo zinakuwa imekufa moja kwa moja.

Lakini baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu nimegundua hizo simu nyingi zinazozima kwa namna hiyo ni zile simu zilizo Isha warranty na nimeyagundua hizo simu ni zile toka zimetengenezwa baada ya mwaka mmoja na ikikaa siku 30 ikiwa imezima chaji hiyo simu ujue itakufa moja kwa moja.

Na nimegundua hiyo inatoka na mikataba mibovu waliyo Ingia hayo makampuni yanayo wauzia software kwamba wao wanao wauzia software wanawapa security ya mwaka mmoja tu.

Kwahiyo ushauri wangu kwa watumiaji wa infinix tecno na itel usiiache simu yako iishe chaji kabisa na ikae siku 30 bila kuichaji.

Wakati tunaendelea kutafuta solution.

Uko sawa mkuu, hata mimi nafanya hivyo kazi, yote uliyosema uko sahihi !
 
Ukweli utabaki pale pale
Africa ni jalala la mchina...
Ma-pikipiki
Ma-simu
Ma- nguo
Nk
Nakuongezea tu kitu kichwani mwako
Si kila kitu cha mchina ni cha ovyo. Mfano kwenye simu China ina simu za ovyo kama TECNO, Infinix, itel, Doogee na kadhalika ila pia ana simu kali zenye international standards kama Xiaomi, One plus, Asus, Oppo, Motorola, Meizu na Vivo.
 
Yaani haina ubora haina class yeyote bora Samsung , Iphone napenda sana ila mmh! Ngumu kuitumia isije ikajiloki mie natumia hizi simu za wahuni za bei yakawaida tu red mi basi
 
Back
Top Bottom