Kwanini watumishi wengi wa Serikali wana hali duni kiuchumi?

Mr IQ

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
1,024
Reaction score
1,377
Habari za kazi wanajamvi,

Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa, na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi? Na nini kifanyike kutatua swala hilii?

Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
 
Solution ni moja tu.
Serikali izuie benki za kibiashara na taasisi za kifedha kukopesha watumishi badala yake huo mzigo wa kuwakopesha watumishi ubaki mikononi mwa serikali. Mikopo isiwe na riba maana tunakopeshwa MISHAHARA yetu ambayo ni haki zetu
Wazo zuri ivii kwani riba ndio chanzo cha kuwa na halingumu ya maisha??
 
Kabisa watumishi wa chini wana hari mbaya mimi nafikir walio juu namaanisha mabosi wana mishahara mikubwa kulinganisha na watumishi wa chini ivyo ata wakikopeswa benki uyu wa chini anabakiwa na kidogo sana kulinganisha na mabosi wa juu mtazamo wangu mdogo ndio upo ivyo.
 
Solution ni moja tu.

Serikali izuie benki za kibiashara na taasisi za kifedha kukopesha watumishi badala yake huo mzigo wa kuwakopesha watumishi ubaki mikononi mwa serikali. Mikopo isiwe na riba maana tunakopeshwa MISHAHARA yetu ambayo ni haki zetu
Serikali yenyewe inakopa kwa riba toka kwa mabepari wewe mfanyakazi wa serikali unataka ukope bila riba serious?

Mikopo isiyo na riba ipo Mombasa tu na Uarabuni.
 
Serikali yenyewe duni unataka wafanyakazi wake wasiwe duni? Hadi pale tutapokua na uchumi imara ndio wafanyakazi watapata ahueni kwanza nje ya mshahara kila mtumishi ana haki ya pesa ya usafiri, pesa ya makazi, pesa ya muda wa ziada kazini, pesa ya kuitwa kazini kwa dharula, pesa ya mawasiliano, lakini zote hizo wanapata wachache walimu, manesi, polisi, maafisa kilimo sidhani kama wanapata hizo
 
Kuna taasisi mpaka walinzi tuna posho ya usafiri, chakula na overtime.

Msikubali kuajiriwa na kila taasisi maadamu tu unataka check number.

Mimi nimejaribu kuwasemea waajiriwa tu wa Tanzania ambao wanakufa wakiwa na miaka 30 na kuzikwa wakiwa na miaka 60 , yaani watumishi wana mizigo ya madeni na ndio maana wengi huishia kua wezi tu wa mali ya umma
 
Habari za kazi wanajamvi...
Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa... na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi..?? Na nini kifanyike kutatua swala hilii??
Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Samahani, naomba kufahamu status yako, plus hali ya kimaisha!
Nijuavyo, watumishi wa Serikali hawafiki 1M! Tz tuko 60M+, hali ya watanzania kwa ujumla ikoje tafadhali?
 
Habari za kazi wanajamvi...
Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa... na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi..?? Na nini kifanyike kutatua swala hilii??
Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Akili zao zimelala
 
Angalia mabango ya wafanyakazi wa Tanzania siku ya mei mosi wengi hulia na maslahi duni
IMG_0933.jpg

IMG_0932.jpg

Hapo ndugu zetu walimu ndio hua wanalia hadi wanazimia
 
Habari za kazi wanajamvi...
Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa... na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi..?? Na nini kifanyike kutatua swala hilii??
Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Toka lini mwajiri akakulipa kiasi kikubwa cha pesa

1. Mwajiri anakulipa fedha ya kufanya uweze kula.

2. Uweze kununua nguo nadhifu ili uwavutie wengine kuajiriwa.

3. Uweze kupata matibabu ya kawaida

4. Uweze kujenga kibanda sio nyumba ya maana ili uweze kuishi humo na kufuga mabata, kulima mchicha.

5. Utapata mikopo yenye riba kubwa ili uwe mtumwa wa kudumu.

6. Ukionekana una mishe binafsi za kukuingizia kipato au kumiliki mali kama magari nyumba nzuri wanakuundia zengwe ili waweze kuharibia ramani zako.
Kwa ujumla kuajiriwa ni utumwa flani unafichwa na mshahara mdogo.
Kuajiriwa ni kimbilio la waoga wa maisha
 
Habari za kazi wanajamvi...
Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa... na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi..?? Na nini kifanyike kutatua swala hilii??
Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Kuna mzee mmoja niliwahi kutana naye 2009 wakati nilipoenda kupiga kimeo cha computer maintenance
kwenye wizara yao wakati tumekaa baada ya kazi kwisha katika kupiga stori akaniambia unajua kwanini sisi wafanya kazi wa serikali hatuna maisha ? nikamwambia sijui.. akaniambia.. Ni kwasababu tukiwa humu ofisini tunakuwa kama wafu vile akili zinakuwa zimepofushwa, akili ya kuzalisha katika ziada nje ya ofisi inatoweka katika kipindi chote cha utumishi wako, pili hii michezo ya kuiba iba hela za selikali unafanya watumishi wengi kuishi kwenye laana sana si kwa mtumishi anayeiba hizo hela tu mpaka familia yake, tatu ukiwa ofisi za serikali ukaanza kuishi maisha ya anasa, kushiriki vitendo vya ushirikina utaishi maisha ya kimaskini au utakufa kwa ajali au ugonjwa wenye uchungu sana hata kama ulikuwa na cheo cha juu..
 
Solution ni moja tu.
Serikali izuie benki za kibiashara na taasisi za kifedha kukopesha watumishi badala yake huo mzigo wa kuwakopesha watumishi ubaki mikononi mwa serikali. Mikopo isiwe na riba maana tunakopeshwa MISHAHARA yetu ambayo ni haki zetu
Kwaiyo wakikopeshwa na Serikali, Serikali haita wakata kila mwezi kulipia mikopo yao?
 
Back
Top Bottom