Kuna mzee mmoja niliwahi kutana naye 2009 wakati nilipoenda kupiga kimeo cha computer maintenance
kwenye wizara yao wakati tumekaa baada ya kazi kwisha katika kupiga stori akaniambia unajua kwanini sisi wafanya kazi wa serikali hatuna maisha ? nikamwambia sijui.. akaniambia.. Ni kwasababu tukiwa humu ofisini tunakuwa kama wafu vile akili zinakuwa zimepofushwa, akili ya kuzalisha katika ziada nje ya ofisi inatoweka katika kipindi chote cha utumishi wako, pili hii michezo ya kuiba iba hela za selikali unafanya watumishi wengi kuishi kwenye laana sana si kwa mtumishi anayeiba hizo hela tu mpaka familia yake, tatu ukiwa ofisi za serikali ukaanza kuishi maisha ya anasa, kushiriki vitendo vya ushirikina utaishi maisha ya kimaskini au utakufa kwa ajali au ugonjwa wenye uchungu sana hata kama ulikuwa na cheo cha juu..