Kwanini watumishi wengi wa Serikali wana hali duni kiuchumi?

Kwanini watumishi wengi wa Serikali wana hali duni kiuchumi?

Ile rate walitupa mkuu na hata sasa nazani wanapewa taasisi nyingi chini ya maliasili na utalii rafiki zangu wanasema wanalipwa hio 150k na kwa marafiki zamgu wa ruwasa pia wanalipwa 130k na tumeajiriwa nao hata miaka mitatu bado.
Yaani daraja lenu utapata 120 au 130 ndizo rates mpya hizo. Kisheria zimeshaanza kutumika tangu July mwaka huu.
 
Hizo ndo point na ile mentally kwamba mwisho wa mwezi si ntapata tu ...kuna watu Wana safari daily ila pesa haikai wao ni hanasa tu .

Nimeenda kijijini Kuna ticha yuko early 30's ana nyumba na pikipiki nje kwake ana kiduka cha kusogezee siku ana mke ni WA kawaida hanaga skendo na anapendwa ..

Uncle wangu ni mwalimu wa msingi hapo mtwara mjini ana nyumba mbili hata miaka 50 bado hajafika ,na anapokaaa kachimba kisima anauza maji maana huko alipo ni town ila maji ya shida Tena sio mbali ni mjini hapo hapo kwa bajaji kutoka mkanared(chipuputa) au town kabisa mpaka hapo ni jero tu.
Mkanaredi 😁😁😁
Mkuu, nimekupata
 
Akichukua mkopo makato ni miezi 60(miaka 5) atanunua kiwanja nakujenga ukuta Hadi sehemu Fulani Deni likiisha anakopa Tena amalizie palipobakia wakati huo ada inazingua balaa watoto ,bado hajatapeliwa na mumewe au mkewe ni SHIDA
Nyiieee, tabu juu ya tabu
Acheni tu
Ila Sasa nafasi za ajira zikitoka zinavyogombaniwa Utafikiri Kuna cha maana, ngoja upate Sasa ndio utajua
 
Dah! Nimecheka nilipokumbuka karatasi zinavyotumika kufutia ubao (sasa utaiba makaratasi ya jalalani?), Na vipindi vya chaki ukivyoiba ukienda darasani utamuuzia nani?
Tamisemi ni Shida blaza
On top of that, kuna songombingo za madiwani na wakurugenzi
 
Wengi ni kwa sababu za kujitakia maana wanachoamini ni kwamba ukishaajiriwa serikalini ndo mwisho..hawana uthubutu kutafuta green pastures sehemu nyingine tofauti na sisi wa private sector anytime unaweza hamia kwenye green pastures. Ntakupa mfano mmoja kuna ndugu yangu mmoja yupo serikalini nilimpa connection moja ya kuingia kwenye mradi mmoja unafadhiliwa na USAID ulikua mradi wa miaka mitano na mzuri sana,akachomoa kabisa eti hawezi toka serikalini. Basi akampa mwenzake connection mwenzake akajilipua. Hivi ninavyokwambia huyo jamaa yake yuko mbali mno na anasema hata angefanya kazi milele serikalini asingefikia mafanikio aloyapata sasa. Mradi uliisha akaingia kwenye mradi mwingine nao mtamu sana. Yule bro wangu anajuta vibaya sana hadi wife wake anamsemaga ila ndo too late kaishia kuwa na carina wakati mwenzie anapush Volkswagen Tiguan ya 2015 na kabla ya hapo alishakua na harrier new model, kajenga zake goba kapangisha ye anapiga zake kazi mkoa na hata ndege alikua hajawahi kupanda ila saizi hadi kachoka na mindege.

images (5).jpeg
 
Kwa mfano mimi binafsi bado mwajiriwa mpya per diem yangu bado 80k tuombe mpya ya mama irudi ya 150k...sasa imagine niko field ya siku 14...
Mahitaji yangu
Lodge 20000 kwa siku
Chakula na maji 15000 kwa siku
Ukaombwa home uchangie rambirambi lets say 50000
Hapo bado una familia nyumbani umeiachaje..bando,

Haya kama ndo mlevi ukienda tu bar ukisema unywe bia zako tano ukalale mara kaja mlevi mwenzako ili kumfurahisha ushamnunulia bia tatu yaani vijana changamoto nyingi bado hujaopoa demu...ebu nambie home unarudi na nini katika hio million maana ume save sana labda laki mbili...ukirudi home ma bill yanakusubiri...kumbuka mshahara ulishaukopeaga hivyo kama laki saba unakatwa hata laki nne kila mwezi...yaani ni maisha ya kipumbavu kbs
Leo hujanywa Henken naona unaakili Safi kabisa ,,,utumishi wa umma unamuumiza Sana mwenye salary ndogo hebu fikiria nasomesha wanangu na huu mfumuko wa bei ya home kutumia 10k Ni kuimiza familia ....hapo wazazi lazima kila mwezi uwabackup ........familia mzima na ukoo pia eti inanitazama msomi Mimi.....Ni upumbavu tu...
 
Kabisa watumishi wa chini wana hari mbaya mimi nafikir walio juu namaanisha mabosi wana mishahara mikubwa kulinganisha na watumishi wa chini ivyo ata wakikopeswa benki uyu wa chini anabakiwa na kidogo sana kulinganisha na mabosi wa juu mtazamo wangu mdogo ndio upo ivyo.
Msingi mkubwa wa kuajiriwa iwe serikalini au private sector, ni kukulipa ujira na some few benefits (bima ya afya, salary advances/loans etc) ili uweze kujikimu kimaisha wakati ukitumishwa na kamwe siyo kukufanya uwe tajiri. Katika kila watumishi 10 very few (labda 3 or less) ndiyo utakuta wanausogelea utajiri/hali nzuri sana kimaisha. Sababu kubwa ni kutumia fursa vema kufanya uwekezaji au kupiga dili/ufisadi. Kumbuka wako wengi pia ambao hupiga Madili lakini huishia kwenye matanuzi tuu. So msingi mkubwa wa kuajiriwa ni wewe kufanya kazi kwa mwajiri wako mpaka ustaafu halafu waajiri wengine.
 
Leo hujanywa Henken naona unaakili Safi kabisa ,,,utumishi wa umma unamuumiza Sana mwenye salary ndogo hebu fikiria nasomesha wanangu na huu mfumuko wa bei ya home kutumia 10k Ni kuimiza familia ....hapo wazazi lazima kila mwezi uwabackup ........familia mzima na ukoo pia eti inanitazama msomi Mimi.....Ni upumbavu tu...
Kwanza nina siku tatu sijanywa naona niachane nazo kabisa inshallah mwenyeziMungu anifanyie wepesi niupakane na pombe maana appetite ilikata karibia mwezi baada ya kufululiza safari...


Back to topic vp tutajikwamua me naona ni kupitia biashara ya duka la rejareja kwani nimewahi kuifanya ni biashara nzuri ambayo inakutunzia mtaji wako..


Me nilifunguliwa duka na mama la mtaji wa million tatu baada ya kumaliza chuo kwa kweli hata kama nilikuwa mtumiaji wa pombe ila hela yake ilidumu sana kwa zaidi ya mwaka yaani mpaka napata kazi naondoka dukani nimeliacha labda na mtaji wa million na nusu...sio haba ikizingatiwa kuna madeni niliyaacha zaidi ya laki nne pia lilitusaidia mambo ya mboga home...so nikaja kugundua kumbe ningepata mtu muaminifu wa kuuza lets say mke wangu ikawa kila ninapopata pesa kutoka kwenye madokezo yao za safari basi chap naenda maduka ya jumla najaza bidhaa zile ambazo zinakaa muda mrefu...unaondoka kwenda site huna hela mke anakuwa anakutumia ndogondogo lets say 30000 kwa siku hapo lazima ujibane ulale lodge ya 15k na ule 10k...ukirudi home unakuta duka lina bidhaa hivyohivyo ukifanya huo mchezo utajikuta mna mtaji wa million kumi dukani hapo nyie ni maboss wa kitaa..
 
Serikali yenyewe duni unataka wafanyakazi wake wasiwe duni? Hadi pale tutapokua na uchumi imara ndio wafanyakazi watapata ahueni kwanza nje ya mshahara kila mtumishi ana haki ya pesa ya usafiri, pesa ya makazi, pesa ya muda wa ziada kazini, pesa ya kuitwa kazini kwa dharula, pesa ya mawasiliano, lakini zote hizo wanapata wachache walimu, manesi, polisi, maafisa kilimo sidhani kama wanapata hizo
Mkuu tuchukulie mfano wafanyakazi wa Elon Musk aliyonunua Twitter je ni matajiri? Ukweli ni kwamba hapana ila wanalipwa vizuri kuweza kumudu maisha yao ya kila siku.
 
Mimi nimejaribu kuwasemea waajiriwa tu wa Tanzania ambao wanakufa wakiwa na miaka 30 na kuzikwa wakiwa na miaka 60 , yaani watumishi wana mizigo ya madeni na ndio maana wengi huishia kua wezi tu wa mali ya umma
Ulaya hakuna mfanyakazi ambaye hana madeni. Wenzetu kule kila kitu wananunua kwa mkopo (mortgage) kuanzia nyumba, gari, furnitures mpaka hata simu kama Samsung na iPhone... Hivyo hukatwa kwenye mishahara yao mpaka wanapostaafu. Kuna binadamu yangu yuko huko majuu huwa anashangaa sana kuona huku nyumbani tunajenga nyumba au kununua gari bila kukopa.
 
Samahani, naomba kufahamu status yako, plus hali ya kimaisha!
Nijuavyo, watumishi wa Serikali hawafiki 1M! Tz tuko 60M+, hali ya watanzania kwa ujumla ikoje tafadhali?
Tumeshushwa kutoka uchumi wa kati kwenda wa chini (Namnukuu Prof Muhongo bungeni majuzi) kwa sababu kipato chetu kwa mwaka kwa walio wengi by end of the year itakuwa below dola 1000.
 
Jibu ni jepesi tu, Wao ni Watumishi wa Serikali na sio Watendaji wa Serikali.
Siku zote ukishaitwa Mtumishi maana yake unatakiwa kutumikia watu fulani kwa ujira mdogo, Ila ukishakuwa Mtendaji wa Serikali basi ujue mema yote yanaazia kwako katika kundi ulilopo.
Mwisho kabisa, ukiona Mtumishi tajiri ujue ni mwizi.
 
Habari za kazi wanajamvi,

Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa, na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi? Na nini kifanyike kutatua swala hilii?

Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Well Said mjumbe hali sio kbisa sema ndio hivo kila mtu lake rohoni
 
Mkuu tuchukulie mfano wafanyakazi wa Elon Musk aliyonunua Twitter je ni matajiri? Ukweli ni kwamba hapana ila wanalipwa vizuri kuweza kumudu maisha yao ya kila siku.
Utajiri sio rahisi kiivyo kma unavyosikia ,nakueleza na ishu ya kuajiriwa lazima iendelee ...siwezi kukificha wanaoangukia pua mpaka kuchanganyikiwa kweny biashara ni mwengi ...katika muundo wa biashara haswa nchi za kiafrica ambazo ngumu watu kuexport kupata fedha za kigeni ni ngumu mno hata asilimia 30% ya wafanyabiashara wote wawe na mfanikio makubwa zaidi wachache wale mafia ndo wanakaa kweny soko na kupiga faida Kuna michezo kibao unafanyika ,majungu ,chuki yaani balaa.

Nina experience na kuishi na watu ambao nafanya kazi nao kazi sehemu tofauti walishaangukia pua kweny business mpaka wamekuja kurecover ni mda mrefu... Biashara sio rahisi na sio kwa kila mtu tambua iyo haswa kama startup hata hao matajiri wengi haswa wa Asia ni watu wanarithishana kibongo ngumu sana yaani una bet kabisa ..

Huyo tajiri lazima awe na wafanyakazi katika shughuli zake lazima Maisha yaende ivyo.
 
Ila tusisahau kuna mapepo na uchawi katika familia kuna wabaya wanaroga, wanachukua nyota za watu, wanawatesa, nyie mnaona mwana anazingua pombe, mademu, usharo, pesa haikai kumbe kawekwa chuma ulete nafsi yake.

Mshukuru sanq mola wako kama una hali nzuri ya maisha.

Wengine aina ya wake zao sio, waume sio mambo ni mengi sana.

Tujipambanie sana kilq wakati fanyq check up ili mradi hurogi mtu wala huna husda pambana sana haya maisha ni battle kubwa sana.
 
Serikali yenyewe duni unataka wafanyakazi wake wasiwe duni? Hadi pale tutapokua na uchumi imara ndio wafanyakazi watapata ahueni kwanza nje ya mshahara kila mtumishi ana haki ya pesa ya usafiri, pesa ya makazi, pesa ya muda wa ziada kazini, pesa ya kuitwa kazini kwa dharula, pesa ya mawasiliano, lakini zote hizo wanapata wachache walimu, manesi, polisi, maafisa kilimo sidhani kama wanapata hizo
Nikweli mshahara wa mtumishi unatimika kwenye mambo ya utumishi yaani unanufaisha serikali sio yeye mtumishi
 
Back
Top Bottom