Kwanini watumishi wengi wa Serikali wana hali duni kiuchumi?

Kwanini watumishi wengi wa Serikali wana hali duni kiuchumi?

Solution ni moja tu.

Serikali izuie benki za kibiashara na taasisi za kifedha kukopesha watumishi badala yake huo mzigo wa kuwakopesha watumishi ubaki mikononi mwa serikali.

Mikopo isiwe na riba maana tunakopeshwa MISHAHARA yetu ambayo ni haki zetu
Isipokuwa wa tiara ei.
 
Toka lini mwajiri akakulipa kiasi kikubwa cha pesa

1. Mwajiri anakulipa fedha ya kufanya uweze kula.

2. Uweze kununua nguo nadhifu ili uwavutie wengine kuajiriwa.

3. Uweze kupata matibabu ya kawaida

4. Uweze kujenga kibanda sio nyumba ya maana ili uweze kuishi humo na kufuga mabata, kulima mchicha.

5. Utapata mikopo yenye riba kubwa ili uwe mtumwa wa kudumu.

6. Ukionekana una mishe binafsi za kukuingizia kipato au kumiliki mali kama magari nyumba nzuri wanakuundia zengwe ili waweze kuharibia ramani zako.
Kwa ujumla kuajiriwa ni utumwa flani unafichwa na mshahara mdogo.
Kuajiriwa ni kimbilio la waoga wa maisha
1-4 ndio maisha ya standard mzee.hata uwe na nyumba kubwa kama uwanja wa taifa huwez kuilalia yote.portion yako ni 5×6 au 6×6 tena ubavun mwa chumba wala hata chumba hukimaliz.nunua kilo za muchele manyama masosej ila ukila sana sahan moja yan mambio yote ila maisha ndio mzu guko huo
 
Serikali yenyewe duni unataka wafanyakazi wake wasiwe duni? Hadi pale tutapokua na uchumi imara ndio wafanyakazi watapata ahueni kwanza nje ya mshahara kila mtumishi ana haki ya pesa ya usafiri, pesa ya makazi, pesa ya muda wa ziada kazini, pesa ya kuitwa kazini kwa dharula, pesa ya mawasiliano, lakini zote hizo wanapata wachache walimu, manesi, polisi, maafisa kilimo sidhani kama wanapata hizo
Siku za nyuma huko mambo yalikuwa mazuri lakini wahusika walikuwa na nyumba ndogo mpaka vikkandikwa vitabu vya penzi kitovu cha uzembe
 
Habari za kazi wanajamvi,

Kiuhalisia swala la watumishi kuwa na madeni kila kona ni jambo la kawaida sanaaa, na hili linanipa maswali mengi sana bila majibu kwasababu watumishi wa vyeo vya juu na kwa uchache wanahali nzuri ya kiuchumi ila wengi hawana haki nzuri Tatizo liko wapi? Na nini kifanyike kutatua swala hilii?

Nakaribisha mawazo yako ili wote tujifunze ili iwe msaada kwa watumishi wa serikali na wasio watumishi wa serikali.
Jamii inaamini waajiriwa wanapesa na wako stable kuliko mtu anayefanya harakati zake .. hii imepelekea kuwa na dependence level kubwa na wao hawawezi kulikataa hili ukizingatia maisha waliyopitia huko nyuma kusomeshwa kwa michango nk...hivyo wanalazimika ku-pay back .



Kingine wanaingia kwenye mikopo na kuanzisha busness mpya ambazo hawana uzoefu nazo.
 
Wengi ni kwa sababu za kujitakia maana wanachoamini ni kwamba ukishaajiriwa serikalini ndo mwisho..hawana uthubutu kutafuta green pastures sehemu nyingine tofauti na sisi wa private sector anytime unaweza hamia kwenye green pastures. Ntakupa mfano mmoja kuna ndugu yangu mmoja yupo serikalini nilimpa connection moja ya kuingia kwenye mradi mmoja unafadhiliwa na USAID ulikua mradi wa miaka mitano na mzuri sana,akachomoa kabisa eti hawezi toka serikalini. Basi akampa mwenzake connection mwenzake akajilipua. Hivi ninavyokwambia huyo jamaa yake yuko mbali mno na anasema hata angefanya kazi milele serikalini asingefikia mafanikio aloyapata sasa. Mradi uliisha akaingia kwenye mradi mwingine nao mtamu sana. Yule bro wangu anajuta vibaya sana hadi wife wake anamsemaga ila ndo too late kaishia kuwa na carina wakati mwenzie anapush Volkswagen Tiguan ya 2015 na kabla ya hapo alishakua na harrier new model, kajenga zake goba kapangisha ye anapiga zake kazi mkoa na hata ndege alikua hajawahi kupanda ila saizi hadi kachoka na mindege.

View attachment 2420396
Next time nipe connection na mm mkuu nijilipue ntoke local gvnmt.
 
Serikali yenyewe duni unataka wafanyakazi wake wasiwe duni? Hadi pale tutapokua na uchumi imara ndio wafanyakazi watapata ahueni kwanza nje ya mshahara kila mtumishi ana haki ya pesa ya usafiri, pesa ya makazi, pesa ya muda wa ziada kazini, pesa ya kuitwa kazini kwa dharula, pesa ya mawasiliano, lakini zote hizo wanapata wachache walimu, manesi, polisi, maafisa kilimo sidhani kama wanapata hizo
Hii haki iko kisheria au n matamko tu na kama kunakifungua Cha sheria naomba hicho kifungu kinachotaja haki za mtumishi kama ulivyoziainisha ktk andiko lako tafadhari
 
Wazo zuri ivii kwani riba ndio chanzo cha kuwa na halingumu ya maisha??
Unakopa milioni 14 unarudisha milioni 27 hauoni huo mzigo, hata mikopo ya utumishi ikiletwa wanapeana wakubwa tu
 
Hawana akili na matumizi ya akili pia.
 
Unakopa milioni 14 unarudisha milioni 27 hauoni huo mzigo, hata mikopo ya utumishi ikiletwa wanapeana wakubwa tu
Yeah, hapo kwenye mikopo ya utumishi ile ya BOT wanajikopesha wao wenyewe umbwa wale
 
Kwa mtu ambaye hajawahi kuajiriwa na serikali hawezi kujua nini kipo ndani yake,mtoa mada nikukumbushe tu kuna watanzania wenzetu tena kundi kubwa sana wanaishi maisha magumu na ya kubahatisha halafu eti useme mfanyakazi wa serikali ana maisha magumu unajua unachekesha watu ukiachana na mishahara kuna taasisi zina ma allowance kibao mtu ukitoka tu ofisini kwenda kufanya kazi za nje analipwa pesa nzuri tu halafu uje ufananishe na masikini ambaye anajipa moyo kwa kusema one day yes wakati hana shughuli ya uhakika ya kumpa kipato tuwe serious jamani.
 
Back
Top Bottom