Kwa hiyo madaktari wetu na mainjinia wa Tanesco na Madereva wa mabasi na marubani wetu wamekariri masomo? Hawajui practicals? Mafundi ujenzi je? Wamekariri masomo?
Wengi sio tu wamekariri, bali mfumo wetu hauwaruhusu kuja na kitu kipya au kuhoji.
Angalia historia ya mtu anaitwa Erasto Mpemba, aligundua - alitukumbusha- kitu kinaitwa Mpemba-Aristotle effect. Aristotle alikiandika hiki kitu miaka kama 2500 iliyopita, kikaja kusahaulika na ulimwengu wa sayansi.
Kitu chenyewe ni kwamba, katika mazingira fulani ya kugandisha maji, maji ya moto yanaganda kwa haraka zaidi ya maji baridi, kitu ambacho kinaonekana kuwa counter-intuitive, kwa sababu maji ya baridi yapo karibu zaidi kufikia temperature ya kuganda kuliko maji moto.
Erasto Mpemba aligundua hilo, kwa sababu alikuwa anafanya kazi ya kugandisha barafu na kuuza, tulikuwa tunaita asikirimu.
Shuleni walipewa jaribio linalofanana na hilo, mwalimu akategemea majibu kama ya kitabuni, Mpemba akamuonesha practically kwamba majibu yanayotegemewa kitabuni si halisi. Mwalimu alim dismiss Erasto Mpemba kwa miaka kadhaa, mpaka akaja mzungu kwenye program moja. Erasto Mpemba wakati huo mtoto tu, bado alikuwa na hamu ya kuchunguza zaidi, akaona Watanzania hawamuelewi, akamfuata huyo mzungu. Akamuelezea alivyofanya experiment na matokeo yake yalivyokuwa tofauti na kitabu. Mzungu akamsikiliza, wakafanaya majaribio, wakaona kweli Mpemba yuko right. Papers zikawa published. Hiki kitu kiliwazingua wansayansi kuanzia miaka hiyo ya sitini mpaka wamepata jibu hivi karibuni
(PhysOrg.com) -- Scientists have known for generations that hot water can sometimes freeze faster than cold, an effect known as the Mpemba effect, but until now have not understood why. Several theories have been proposed, but one scientist believes he has the answer.
phys.org
Kwa nini walimu wa Erasto Mpemba hawakumsikiliza na kufuatilia experiment yake kwa umakini? Kwa nini ilibidi Erasto Mpemba amfuate mzungu ili asikilizwe? Kuna kina Erasto Mpemba wangapi huko vijijini ambao wamezimwa ideas zao kwa sababu hawajapata mzungu?
Unapozima ideas za vijana wadogo mashuleni, wakikua wakubwa watapata wapi nguvu za kuondokana na dunia ya kukariri na kuanza kuhoji mambo?
Unaweza kunisoma kirahisi kwamba nasema watu wetu hawana akili ya kuhoji. La hasha, sina maana ya kusema hivyo.Tuna watu wenye akili sana.
Kuna mtu aliuliza, wako wapi kina Newton na Einstein wa Africa? Ina maana watu wote wa Africa hakuna wenye akili kama hizo?
La hasha, wapo wengi tu.Wameminywa na utamaduni. Utamaduni wa mambo kufanywa kwa "amri kutoka juu". Utamaduni wa "mkubwa hakosei".Utamaduni wa "funga kombe mwanaharamu apite".
By the time mtu anafika kuwa Engineer na Doctor huko, anakuwa kashafundishwa self censorship.Anafanya kazi ndani ya office politics, kwa kukariri.Akianza kuhoji na kuleta innovation tu anapigwa daflao.
Zaidi ya watu, tuna tatizo la mfumo na utamaduni.
Ndiyo maana ukitafuta vitu vipya tunavyogundua, ni vichache na katika hivyo vichache, vyenye impact kwenye kutatua matatizo katika maisha ya kila siku ni vichache zaidi.