Kivipi imebadilika kuwa dunia haihitaji rubani aliyefaulu mitihani? Dunia haihitaji daktari aliyefaulu mitihani? Haihitaji wakili aliyefaulu mitihani? Haihitaji mhasibu au mchumi aliyefaulu mitihani?Acha aminisha ndoto za zamani dunia imebadirika saivi
Umepigilia msumari penyewe. Tanzania tumeingia kwenye mfumo mbaya sana na kuja kutoka hapo ni kazi na itahitaji nguvu kubwa na akili. Hili ni tatizo na kinachofanyika sasa hivi shuleni ni wanafunzi kukaririshwa ili washinde mitihani. Mambo ya kuelewa wanachofundishwa yamewekwa pembeni. Sasa hivi kila shule inahijitahidi kutumia ''mbinu mbadala'' ili ifaulishe na kusifiwa. Na wanafunzi nao wanajitahidi kutumia ''mbinu mbadala'' ili wafaulu. Matokeo yake ni kuwa tutakuwa na ''wataalam'' wasio na utaalam wowote na watanzania kushindani kwenye soko la ajiri itakuwa ngumu sana. Kinachotakiwa sasa hivi ni kufumua mfumo wote wa elimu na kutahini ili turudi kwenye mwelekeo mzuri. Mitihani ya mwisho inatakiwa iwe sehemu ndogo ya kutahini wanafunzi.Sio kilaza ana division one point saba, kwa mawazo na akili kama zako sio kilaza kabisa, ni genious kabisa na hakuna mtu kwenye ukoo wenu amewahi kupata hiyo ufaulu lakini kwetu sisi wenye akili kubwa huyu mtoto sio genious.
Kwani wewe ulikua unahoji nini mkuu?Kivipi imebadilika kuwa dunia haihitaji rubani aliyefaulu mitihani? Dunia haihitaji daktari aliyefaulu mitihani? Haihitaji wakili aliyefaulu mitihani? Haihitaji mhasibu au mchumi aliyefaulu mitihani?
kwa hiyo wewe mkuu unaka kutwambia kwamba mtu aliyepata division one o level na advance hana maarifa? mpaka uanze kumfanyia usaili. Labda ungezungumzia wafanyiwe usaili wenye degree. Lakini sio hizo level mbili. nadhani umesoma olevel na advance na unazijua vizuri.Nilikwenda kusoma nchi fulani hivi. Nilishangaa sana kuona kuwa wanafunzi kupata first class kwenye shahada ya kwanza ni kawaida tu. Na actually inategemewa.
Mimi naona ishu siyo kupata division one au first class. Ishu ni kama hizo division one na first class kweli zinaendana na maarifa yanayohitajika. Na hili ni suala linalogusa mfumo mzima wa elimu. Kwa hiyo hoja yako haijakaa sawa. Hoja yako ilipaswa kuegemea kwenye kusaili kama hizo divisheni wani zinaendana na maarifa yanayohitajika kwa wanaozipata.
Ndiyo. Wazazi wanataka watoto wao wafaulu vizuri kwa sababu hakuna mzazi anayemtakia mabaya mtoto wake. Na ufaulu mzuri bado ndiyo kigezo kikuu cha watoto kuendelea na masomo ya juu. Bado tunahitaji madaktari. Wahandisi. Walimu. Wafamasia. Wanasheria...na yote haya yanahitaji watoto waliofaulu vyema. Kama hutaki ufaulu wa mitihani utumike kama kigezo kikuu basi pendekeza kigezo kingine mbadala.
Na unaposema hao divisheni one wamefanya nini la maana, unamaanisha nini? Katika mazingira haya ya kwetu, we ulitaka wafanye nini ndiyo uwaone kuwa wamefanya la maana? Ukienda hospitalini ukafanyiwa upasuaji na daktari aliyepata divisheni one hiyo haitoshi? Ukipita kwenye daraja au kuishi katika jengo lililojengwa na huyo mwenye divisheni one haitoshi?
Ili kutenda haki, huu unapaswa kuwa mjadala mpana unaohusu mfumo mzima wa elimu na siyo hawa wanaopata divisheni one ambao nao ni kama "wahanga" tu wa mfumo wenyewe.
Wengi sio tu wamekariri, bali mfumo wetu hauwaruhusu kuja na kitu kipya au kuhoji.Kwa hiyo madaktari wetu na mainjinia wa Tanesco na Madereva wa mabasi na marubani wetu wamekariri masomo? Hawajui practicals? Mafundi ujenzi je? Wamekariri masomo?
😂😂😂😂Imebidi nicheke.Mkuu nina uhakika hujafika chuo
Hujapata one
Advance hujafika
O level ulikunja sifuri nzuri
Unawaonea wivu madogo wanaopasua div one kwa sasa
Tulia dawa ikuingiee
Nani alikwambia usisome kenge weweee
Sikuwa na maana hiyo. Nilitumia kusaili kama ku- question ubora wa hizo divisheni one jambo ambalo linaturudisha kule kwenye mfumo mzima wa elimu. Nimesharekebisha. Ukisoma tena pengine utapata nilichokuwa najaribu kusema..kwa hiyo wewe mkuu unaka kutwambia kwamba mtu aliyepata division one o level na advance hana maarifa? mpaka uanze kumfanyia usaili. Labda ungezungumzia wafanyiwe usaili wenye degree. Lakini sio hizo level mbili. nadhani umesoma olevel na advance na unazijua vizuri.
Kuna watu tulikuwa nao huku, very bright fellows. Wakaamua kurudi nyumbani kujaribu kubadili mambo.Naam! Ndiyo maana akina Erasto Mpemba wengi wanajichokea na kuamua kwenda zao nje huko ambako wanaweza kufanya mambo yao kwa uhuru. Sijui ndiyo wanaita brain drain hiyo.
Kuna Mtanzania alikuwa software engineer kule Silicon Valley alifariki. Nilikwenda katika msiba ule. Aisee nilikutana na Watanzania vipanga hatari na wanaofanya mambo ya kueleweka katika nyanja zao. Nikawa najisemea tu watu kama hawa ukiwa na mfumo mzuri wa kuwawezesha ukawarudisha nyumbani na kuwapa uhuru, si wanaweza kuleta msukumo mpya na hata kubadilisha sura ya nchi? Lakini sisi kila kitu ni siasa. Kujibana mumo kwa mumo katika mawazo yale yale miaka nenda miaka rudi. Ukijaribu kuleta mchapuko wa mawazo unaonekana adui...
Mimi Auncle wangu ni computer engineer hajarudigi mpaka leo yupo Texas huko, na kampuni alizozifanyia kazi katika top leve ni zifuatazo, Philips, BP, Schlumburger (ambayo ndio yuko kwa sasa) ana hela chafu hana hata mpango wa kurudi kwenye ardhi yetu ya udogo mwekundu.Naam! Ndiyo maana akina Erasto Mpemba wengi wanajichokea na kuamua kwenda zao nje huko ambako wanaweza kufanya mambo yao kwa uhuru. Sijui ndiyo wanaita brain drain hiyo.
Kuna Mtanzania alikuwa software engineer kule Silicon Valley alifariki. Nilikwenda katika msiba ule. Aisee nilikutana na Watanzania vipanga hatari na wanaofanya mambo ya kueleweka katika nyanja zao. Nikawa najisemea tu watu kama hawa ukiwa na mfumo mzuri wa kuwawezesha ukawarudisha nyumbani na kuwapa uhuru, si wanaweza kuleta msukumo mpya na hata kubadilisha sura ya nchi? Lakini sisi kila kitu ni siasa. Kujibana mumo kwa mumo katika mawazo yale yale miaka nenda miaka rudi. Ukijaribu kuleta mchapuko wa mawazo unaonekana adui...
Ukienda U.S, CANADA lazima utoke. Waafrika tuna akili hata huu mfumo wetu wa elimu ni mzuri na unaendana na dunia inavyo kwenda changamoto kubwa ni mazingira yetu ya kujifunzia ni magumu. Hatuna vitendea kazi vya kujufunzia.Sikuwa na maana hiyo. Nilitumia kusaili kama ku- question ubora wa hizo divisheni one jambo ambalo linaturudisha kule kwenye mfumo mzima wa elimu. Nimesharekebisha. Ukisoma tena pengine utapata nilichokuwa najaribu kusema..
Ukifanya kazi top level IT Marekani, unaweza kurudi Tanzania ukakuta hakuna kazi ya kufanya ya kutumia ujuzi wako.Mimi Auncle wangu ni computer engineer hajarudigi mpaka leo yupo Texas huko, na kampuni alizozifanyia kazi katika top leve ni zifuatazo, Philips, BP, Schlumburger (ambayo ndio yuko kwa sasa) ana hela chafu hana hata mpango wa kurudi kwenye ardhi yetu ya udogo mwekundu.
Ni kweli mkuu,Ukifanya kazi top level IT Marekani, unaweza kurudi Tanzania ukakuta hakuna kazi ya kufanya ya kutumia ujuzi wako.
Tanzania bado hata hatujaweka legal framework ya kueleweka ya mambo ya IT .
Kwa sababu hakuna mifumo iliyo sophisticated hivyo, na hata ukitaka kuanzisha private practice hakuna uchumi wa kutosha.
Na hata ukisema utafute projects interesting za kuanzisha Tanzania, hata za non-profit tu kusaidia jamii, ambazo ukiwa makini huwezi kukosa, hiyo attitude ya serikali kuanzia kodi, rushwa, wizi, mpaka kukubali teknolojia mpya, kwa mtu aliyezoea kufanya kazi Marekani, itakufanya uchoke mwenyewe.
Mimi nilipeleka proposal serikalini tuachane na proprietary software, tutumie open source, tupunguze gharama za software license.
Project ilikuwa nzuri sana, ina breakdown nzuri sana. Wakubwa hawakuipenda. Kwa sababu inainekana wanapolipa software license ndiyo wanapata cha juu hapo hapo. Ukiwapa software za bure hawapati sehemu ya kula cha juu!
Huyo Uncle wako naweza kumuelewa vizuri sana, kwa sababu mimi mwenyewe nishafanya kazi kama hizo naongoza project kubwa dunia nzima. Najiuliza hivi hii kazi ningekuwa Tanzania ningeweza kufanya kweli?
Kule Arusha Kuna Vocational secondary school nafikiri hiyo Ni nzuri hasa ukizingatia kuwa Ni Private.Ukikutana na kila mzazi leo anataka shule inayofaulisha, wazazi wako busy kuulizia ufaulishaji wa shule.
Juzi matokeo yalitoka kila mzazi ama mlezi anakata kujua shule hiyo division one ngapi, sijui nini.
Swali langu, kwa nini wazazi ama walezi wameshikwa sana na ufaulu wa watoto, division one, two na vitu kama hivyo?
Hii obsession ya ufaulu inafanya hata shule ama waalimu watafte namna ya kuiba mtihani ili waonekane wanafaulisha.
Kinachonisikitisha, wao wanaopata division one mbona hatuoni mchango wao wowote wa maana kwenye maisha yetu ya kila siku?
Kila mwaka nchi hii tuna division one za 7 zaidi ya 500, division one za 3 zaidi ya 200, hizo division zina mchango gani kwenye jamii?
Watoto wanaopata division one hizo mbona ni weupe sana vichwani?
Mimi kama mlezi, natamani kuona watoto wakiwa na uwezo wa kuhoji (questioning mind) kufikiri (reasoning skills), kutafakari na kuchambua (analytical skills), vitu ambavyo ndio Dunia ya sasa inachokitaka na sio huu utaratibu wa kukaririsha watoto ili wapate division one ama two.
Mbaya zaidi sioni kama wazazi ama walezi mnaona kama huu mfumo ni mbovu, mfumo wa kuwakaririsha watoto, mfumo wa kuwafanya wasifikirie, wasihoji.
Kuna mtoto wa kaka yangu hapa ana division one ya point 7 lakini nachokiona kichwani mwake ni mweupe kabisa, hata baba yake anauliza huyu amepataje hii one ya 7.
Natafta hela mtoto wangu asome Cambridge ama IB schools.
Unaposema maisha mazuri unamaanisha nini? Mwenzio anazungumzia uwezo wa mtoto kupambanua mambo,kuhoji,nk. Jibu kitaalam usijibu km ligi mkuuWe ulitaka akipata hiyo one agundue Nini,umefatilia maisha yake baada ya kumaliza elimu ya chuo?? .Nina sample ya watu wengi waliopasua form 4 na form 6 na kwa sasa Maisha yao ni mazuri kitu ambacho ndio dream ya kila mzazi .kM unataka. Mwanao asome ili agundue kwenda kuishi Pluto sawa
Humu hatuongezi kitu kichwani,hatuchambui hoja,tunabishana tu,yaani tupo kishabiki tu.Kwenye ukoo wenu majiniazi mlipata ngapi?
Hii ni sawa tu na ile kusema wasomi hakuna kitu, ni afadhali sisi la saba B tumefanya blah blah.... tusiosoma tuna hela kuliko wasomi.
Wewe hukufaulu vizuri, ulikuwa average ila ukafikia kiwango chako hicho cha elimu... acha wivu kwa wenzio.
Suala la ufikiri halifundishwi tu, fundisha hao wanao kuanzia nyumbani.
Hao waliosoma Cambridge ni wote wanatoka super na 'kukufanyia' cha maana?
Hao wote uliowataja walipata dvn one kwani?Kwa hiyo madaktari wetu na mainjinia wa Tanesco na Madereva wa mabasi na marubani wetu wamekariri masomo? Hawajui practicals? Mafundi ujenzi je? Wamekariri masomo?