Kwanini wazazi wa siku hizi wako 'obsessed' sana na ufaulu wa Division One kwa watoto wao?

Baada ya miaka sita hao hao wazazi watakuwa wanalia kuhusu hao hao watoto waliopata division 1 kukosa Ajira
 



Wewe ni bure kabisa -- kwa hiyo mtoto kushindwa pi ndiyo kawa kichwa maji!??? Basi na wewe nitajie tarakimu ya 2021 ya π na mwanasayansi aliyeikokotoa!???
 
A
Kwa hiyo madaktari wetu na mainjinia wa Tanesco na Madereva wa mabasi na marubani wetu wamekariri masomo? Hawajui practicals? Mafundi ujenzi je? Wamekariri masomo?


Hana lake huyo, amekariri tu msamiati ^kukariri^
 
Unaposema maisha mazuri unamaanisha nini? Mwenzio anazungumzia uwezo wa mtoto kupambanua mambo,kuhoji,nk. Jibu kitaalam usijibu km ligi mkuu
Mtoto mwenye uwezo wa kuhoji ni yule aliyefaulu mana anaelewa..
Huwezi niambia mtu na division 4 ama F ya hesabu alete mezani discussion yoyote ya maana ya kuhoji vitu alivyofeli!!..

Elimu inasaidia sana kuja kupambanua vitu badae maishani hasa ukiingia sekta za 'problem solving' za maisha ya kila siku..km one ya form 4 ilikushinda uta'analyze vipi issue kubwa watu waende mbele?

Tusibeze elimu na juhudi za watu jmn
Japo nakubali watoto wajengewe uwezo zaidi kujieleza na ku'analyze mambo bt msiseme hamna impact.,

uambiwe Surgeon wako alipata F ya Biology utafanyiwa operation?.!!
 
Wewe ni bure kabisa -- kwa hiyo mtoto kushindwa pi ndiyo kawa kichwa maji!??? Basi na wewe nitajie tarakimu ya 2021 ya π na mwanasayansi aliyeikokotoa!???
Hehe amenikumbusha mambo ya derive Pi..akijibu nitag😅
 
Baada ya miaka sita hao hao wazazi watakuwa wanalia kuhusu hao hao watoto waliopata division 1 kukosa Ajira
Heri kujitahidi kumpa mtoto yote
Akifaulu inaongeza confidence tu anaweza kuja kujiajiri

ukifeli hio ajira yenyewe sahau
Na ukijiajiri unajihami kisa matokeo hayakua mazuri

sawa maisha ni bidii ila confidence zinginw tusiwanyime watoto
 
Mtu anaweza kushindwa geometry akapata F kwa kuhoji kwa nini mstari mnyoofu una nyuzi 180 na si 181 wala 179?

Watu wakamdharau bila kumjibu.

Ukiwauliza kwa nini, wanakupa jibu la kukariri kanuni za Euclid. Kanuni ambazo haziwezi kuwa proved.

Zimesemwa tu by fiat.

Kumbe wanachodharau ni somo kubwa zaidi la Riemannian Geometry.
 
Kama ana hoja kweli aende mbele kama kina Mpemba akachallenge huko mbele zaidi ndo ntaamini kweli ana hoja ya kuboresha!na we ana akili kweli sio mtu unakuja na F afu huna maelezo yoyote (which is the case for most people)

its 180 with reasons,..unakuja na 179 basing on what?.kama anabisha aje na thesis zake na yeye..atuaminishe dunia nzima...how many people can actually do that?.

sio mtu hata getting proper marks saivi ni issue how can you challenge while you dont even understand existing facts properly?!
Comprehend kilichopo then challenge!
 
Na kiukweli hawajui div.1 hazisaidii chochote ktk mishe za kimaisha zaidi ya kujiona kichwa afu hukazi kwenye mishe.
Naigawa hii div.1 yangu mimi
Hata hizo PhD sioni zimesaidia nini kwenye Nchi hii. Kuna shida katika Elimu yetu, au nasema uongo ndugu zangu?
 
Riemannian geometry ina mistari minyoofu wenye nyuzi 179 na 181.

Kuna watu wengine wanafeli kwa sababu hawaoni vizuri na vijijini hawana access na miwani tu.
 
Riemannian geometry ina mistari minyoofu wenye nyuzi 179 na 181.

Kuna watu wengine wanafeli kwa sababu hawaoni vizuri na vijijini hawana access na miwani tu.
Sasa nini kilisababisha adoption ya common geometry ya 180 degrees na sio 179/181?
Mi sijui....

ila tunaweza kubaliana kuwa common cases kibongo bongo sio watu ku'question logic ya 'content' ya elimu wanayopata bali kutozingatia masomo ama kukosa huduma nzuri za elimu kutokana na umaskini...wa

ss mtu ndo anakutana na geometry for the first time anaanzaje kusema about Riemannian?..
 
Kwani Riemann alianzaje kuuliza mpaka akagundua Riemannian geometry ikaitwa jina lake?

Kama ni mtu wa kuhoji utahoji tu.

Tunaambiwa mstari mnyoofu una nyuzi 180.

Kwa nini tunasema nyuzi 180, na si nyuzi 1, wala 2 wala 179? Wala si nyuzi 1000?

Ni sheria ya kujitungia watu tu.

Na hata ukiikubali, kwa maana lazima jamii iwe na makubaliano kuhusu conventions fulani kuepuka chaos, unakuta kwamba kumbe kuna geometries nyingine tofauti na hizi za Euclid, ambazo pembetatu ina nyuzi zaidi au pungufu ya 180.

Udadisi tu.

Sasa kibongo ukiwa na maswali sana kama haya, unaonekana "Wewe Kiranga sana".

Kumbe maswali haya yanaweza kuibua ugunduzi mzuri sana.

Riemann alivyoanza geometries zake za mstari wenye nyuzi zaidi ya 180 au pungufu alionekana kama chizi.

Baadaye Einstein alivyokuja kugundua Relativity na kuona jinsi spacetime inavyopinda, kwenye gravity kubwa kama pembeni ya black holes na karibu ya jua, akajikuta hesabu anazotumia ni za geomerty ya Riemann ile ya mstari ulionyooka ambao una nyuzi zaidi au pungufu ya 180 (kwa sababu upo katika spacetime iliyopinda).
 
Mpk leo 2021 bado unaandika utumbo tu .
Dah...
Mama kiranga kapata hasara kubwa sana.
 
Wewe ni bure kabisa.

Kufaulu hakuhusiani kabisa na kua na akili ya kohoji.

Hua unaangalia hata bunge letu kweli? Mle kuna maprofesa na watu wa darasa la nne, kuna kitu unajifunza kule?
 
Mitihani ya miaka hii mwanao hasipopata Division one Basi Kuna shida mahali maana Necta walishamtoa kipa golini.
 
Wewe baki hivyo hivyo na fikra za kibolizozo wenzako wanapiga one wanakwenda University wakirudi wanaendesha makampuni na mwanao anarudi kuwa Mlinzi wa geti siku zinasonga.
 
Wewe ni bure kabisa -- kwa hiyo mtoto kushindwa pi ndiyo kawa kichwa maji!??? Basi na wewe nitajie tarakimu ya 2021 ya π na mwanasayansi aliyeikokotoa!???

Kiranga ni mjuaji wa hovyo kabisa, unamhoji 'mtoto' kuhusu pi kitu ambacho hata yeye "kama kaijua" ni juzi tu hapa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…