HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Sawa sawa, unaeza kugombana na mpangaji Bure, miezi 6 imekaa vzr kwa wengi
 
Umewahi kumpangisha mpangaji kwa kodi ya mwezi akakusumbua kulipia?

Kwa nini usianze na wafanyakazi muandikishane bank standing order ili benki iwe inakata yenyewe na kukulipa direct kila mwezi?
 
nimecheka kama mazuri,, pole sana kwahiyo uliamua kuachana nayo au ulikodisha hivyo hivyo
 
Umewahi kumpangisha mpangaji kwa kodi ya mwezi akakusumbua kulipia?

Kwa nini usianze na wafanyakazi muandikishane bank standing order ili benki iwe inakata yenyewe na kukulipa direct kila mwezi?
Sijawahi. Nitajaribu nione. Deposit mwezi mmoja,kodi mwezi mmoja. Ila kwenye masuala ya hela wabongo ni wasumbufu.
 
Hii sekta ya real estate haija rasmishwa kila mtu anafanya kiholela na kufanya serikali kupoteza mapato makubwa sana.

Sekta imeshikiliwa na madalali ambao hawajasajiliwa so haina any regulation.

Nchi nyingine wanapangisha kwa mwezi ila kila jambo lina mambo yake. Unatakiwa kulipa gharama zifuatazo.

1. Hela ya broker - kodi mwezi mmoja.
2. Kodi ya mwezi mmoja
3. Caution fee (kodi ya mwezi mmoja) hii inarudishwa iwapo siku unahama nyumba itakua katika hali nzuri.

Kwa hiyo gharama huwa ni ule mwezi wa 1. Mingine unakua unalipa kodi kila mwezi. Na hulipi kwa mwenye nyumba unalipa kwa broker/dalali...
 
Madalali, mawinga siwapendi nikienda sokoni hqlafu winga anifate kuniuliza maswali ya bidhaa gani nataka huwa natamani kumtukana
 
Sote kama wapangaji,pia mimi ni mpangaji,je unapenda kulipa kodi mwezi mmoja,mitatu au sita?,binafsi bora nilipe miezi sita nitulize akili na kupata muda wa kufanya mambo mengine..
 
Sijawahi. Nitajaribu nione. Deposit mwezi mmoja,kodi mwezi mmoja. Ila kwenye masuala ya hela wabongo ni wasumbufu.
Usumbufu unaopatikana ni kwa sababu mpangaji anatakiwa kulipa miezi mitatu, minne au sita, kwa mwezi ni rahisi zaidi mtu kulipa. Mfanyakazi mwenye familia anayelipwa net milioni moja kwa mwezi ili aweze kulipa kodi ya miezi sita ya 1.2M lazima akope na hapo ndipo usumbufu wa malipo unapokuja, ila angeambiwa alipe laki mbili mbili kwa mwezi ni rahisi sana.
 
Mkuu wengine hela wanayo ila wasumbufu tu. Watu hawataki kodi ya mwezi usumbufu ndio sababu kuu.
 
Madalali, mawinga siwapendi nikienda sokoni hqlafu winga anifate kuniuliza maswali ya bidhaa gani nataka huwa natamani kumtukana
Aisee upo kama mimi na mwingine anakushika na kukushika. 😒.

Kwa Dsm hao mawinga kuna wale wa Karume , yaani unaweza kughairi kilichokupeleka mana ni wasumbufu hatari.

Wanasahau kabisa umetoka ulipotoka hadi unafika pale mwenyewe na kwa hali hiyo unajua ni wapi unakwenda.
 
Kulipa kodi ya miezi mitatu au sita kwa mkupuo ni mtihani kweli.
Siamini pia kama kuna mwenye nyumba atakataa endapo utampa plani yako!,kaa naye andikeni mkataba mpya,pia hakikisha tarehe 28 ya makubaliano haivuki,naona si jambo baya!..(kaa naye)
 
Bidhaa 5k utaambiwa 15k ili winga nae apewe.
Wengine wanakufata nyuma ukiingia dukani anajifanya mmekuja wote ili mwenye duka amkatie hela.
Mimi huwa namwambia mwenye duka huyu dalali sijaja nae.
 
Na Kuna wenye nyumba wengine ni wachawi hata huo mwezi mmoja unaotaka hutakaa ni bora kupambana uwe na kwako Cha mtu mavi.
 
Huu mtindo wa miezi mitatu/sita ni wa kishenzi sana, dawa yake ni kuja kuwapa mwezi mmoja moja baada ya miezi mitatu/sita kuisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…