HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
ngoja waje utasikia
Huyu jamaa roho ya kichawi katoa wapi hahahaaaahahaha ๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜‚ m nikopale naangalia ....

Mbayimbayii
 
Wala hatulazimishi. Huu ni utaratibu tu tuliojiwekea. Kama hutaki jenga nyumba yako, au jenga nyumba zako halafu pangisha kwa kodi ya mwezi mmoja mmoja.

Miezi 3 yenyewe ni usumbufu! Hiyo ya kila mwezi si ndiyo itakuwa usumbufu mara dufu! Unampigia mpangaji hapokei simu! Akipokea anakupanga atatoa ndani ya siku 2 zijazo! Na zikifika hizo siku 2, hatoi! Usumbufu tu
Wapo wanaolipa kwa mwezi lakini wasumbufu kweli,mtu amepigana amejenga,amekukodisha,unajistiri hapo kwa mvua na jua,unajipumzisha baada ya kutoka kazini unapaki na gari lako salama bado unamsumbua hakika ni jambo baya sana,ni bora hizo hela sometimes uziweke UTT-AMIS.
 
Kodi ya luku ya jengo analipa mpangaji, nyie wenye nyumba mnatakiwa mlipe kodi ya mapato kutoka kwenye kipato cha wapangaji wenu.
Hakika mwenye nyumba alistahili kurudisha 18,000/-kwa mpangaji..
 
Mimi nafurahi kuwa na mwenyenyumba ambaye huniazima fedha basi mimi humpatia haraka sana,huwa zinakuja kupunguza amount ya malipo...
 
Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.

Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.

Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
Jenga ya kwako
 
Acha unalaya na pombe ujenge yako kama ni rahisi.
 
Kuna sehemu niliwahi kwenda kuuliza Frem zilikuwa mpya nikichokutana nacho yule mwenye fremu kwa mwezi kodi ni laki na nusu lakini alichokifanya dalali kalipia yeye kodi ya miezi 6 halafu anaipangisha tena ila sasa kajiwekea kodi yake yaani yake kwa mwezi laki tano.

Niliduwaa kiufupi.
Aisee
 
Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.

Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.

Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
hili jambo si ni limekaaa kimakubaliono zaidi?!
 
Ningepata wapangaji wanaojitambua kama wa nchi wanazolipa kodi kwa mwezi, ningechukua kodi kwa mwezi maanake idadi ya units nilizonazo hata nikichujua kwa mwezi inatosha.
Lakini, kwa wabongo hawa kuchukua kodi kwa mwezi maana yake utasumbuana na mtu kila mwezi. Wacha tufanye kwa miezi sita at least.
Halafu ni vigumu sana kumtoa asiyelipa kwa wakati kwa sheria zetu.
 
Wamiliki wa nyumba wafanya vema kudai kodi miezi mitatu au sita ili wapangaji wapate akili ya kujenga zao.Zamani watu walikuwa waminifu walilipa kodi mwisho wa kila mwezi bila shuruti lakini sio miaka hii ambapo hutoroka bila kulipa na kumwacha mwenye nyumba akisaga meno.kama hamtaki jengeรฑi zenu
 
Kuna sehemu niliwahi kwenda kuuliza Frem zilikuwa mpya nikichokutana nacho yule mwenye fremu kwa mwezi kodi ni laki na nusu lakini alichokifanya dalali kalipia yeye kodi ya miezi 6 halafu anaipangisha tena ila sasa kajiwekea kodi yake yaani yake kwa mwezi laki tano.

Niliduwaa kiufupi.
Nchi hii sio mbaya, watu wake do wabaya. Nchi hii inaharibiwa vikajanja wa DAR kila kitu utapeli utapeli na uswahili mwingi.

Mfano mzuri, kule usukumani tunatumia gharama kubwa sana kulima mahindi, kipindi cha mavuno wanakuja makajanja wenye vitumbo vyao wanapima 600 kwa kilo.

Viongozi wetu wameendelea kuruhusu huu uhuni ni hudhuni kwa kweli.
 
Nadhani tumekariri; tumemebeshwa taratibu za nchi za Kimagharibi, ambao hutoza kwa mwaka au nusu mwaka.
Hakuna cha nchi ya magharibi ,huu ni upumbavu unaoexist Tanzania tu , nenda marekani ,Europe nk ,hamna rent ya miezi sita au mwaka .Rent inalipwa on monthly basis
 
Nchi za kimagharibi hazifanyi huu ujinga, hata nchi karibia zote zilizotuzunguka hazina huu utaratibu.
Huu ni utaratibu wa Kiswahili tu.
Na ndicho chanzo cha umasikini kwenye kaya nyingi , pesa ambayo ilitakiwa kuwa Kama mtaji kwenye biashara na uwekezaji inatumika kumlipa mwenye nyumba mwaka mzima au miezi sita ,poverty mindset
 
Mjinga mwenyewe ,jenga yako ufanye hivyo. Suala la nyumba za kupangisha ni kama shule tu. Shule zingine unalipa ada mara moja kwa mwaka, nyingine unaambiwa mara 2, nyingine mara 4. Hivyo unapeleka mtoto kwenye shule unayoimudu. Ni hivyo hivyo kwenye nyumba wengine wanachukua miez 2, wengine 3, wengine 6.

Serikali haiwezi kujiangaisha na mawazo yako ya kijinga sababu sio lazima kukaa nyumba za kupanga, unaweza kuishi lodge ukawa unalipa kila siku.
Bahati nzuri hizo nyumba mtakufa na kuziacha!

Utamuachia mke wako atakuwa ananipangisha Kwa mwezi huku nikimxhomeka Mashine.
 
Back
Top Bottom