hizo pesa nje nje mbona mi sizioni? nipe connection basi mkuu,,Mjini pesa nje nje. Kuna jamaa namfahamu kajenga apartment block ina 8 apartments. Kila moja anapangisha 1m kwa mwezi. Kuna raia wa kigeni kachukua zote na yeye anazifanya Airbnb. Weka hela upate hela.
Mimi nataka kumlipa mwenye nyumba kodi kila mwezi, ninaweza kujisimamia mwenyewe na pesa zangu, sioni sababu ya kumpa mwenye nyumba mkopo usio na riba badala ya kuongeza mtaji wangu kufanyia biashara hizo pesa za miezi mitano ya ziada ninayompa.Sote kama wapangaji,pia mimi ni mpangaji,je unapenda kulipa kodi mwezi mmoja,mitatu au sita?,binafsi bora nilipe miezi sita nitulize akili na kupata muda wa kufanya mambo mengine..
Nyumba iko wapi MkuuHuyo nwambie aje kupanga kwangu, Kwa mwezi 250k ,anilipe kila mwezi ,
Maji na umeme atajitegemea
Daah! kiufupi wanakera sana.Bidhaa 5k utaambiwa 15k ili winga nae apewe.
Wengine wanakufata nyuma ukiingia dukani anajifanya mmekuja wote ili mwenye duka amkatie hela.
Mimi huwa namwambia mwenye duka huyu dalali sijaja nae.
Hela ya broker ni makubaliano tu kati ya mteja na dalali, sehemu nyingi wala watu hawampi dalali kodi ya mwezi, mimi huwa nawapa ya nusu mwezi tu.Hii sekta ya real estate haija rasmishwa kila mtu anafanya kiholela na kufanya serikali kupoteza mapato makubwa sana.
Sekta imeshikiliwa na madalali ambao hawajasajiliwa so haina any regulation.
Nchi nyingine wanapangisha kwa mwezi ila kila jambo lina mambo yake. Unatakiwa kulipa gharama zifuatazo.
1. Hela ya broker - kodi mwezi mmoja.
2. Kodi ya mwezi mmoja
3. Caution fee (kodi ya mwezi mmoja) hii inarudishwa iwapo siku unahama nyumba itakua katika hali nzuri.
Kwa hiyo gharama huwa ni ule mwezi wa 1. Mingine unakua unalipa kodi kila mwezi. Na hulipi kwa mwenye nyumba unalipa kwa broker/dalali...
Huku kwetu unaweza hata kulipia kwa mwezi hata kwa kudunduizaHata mikoani.
Wazo lako si baya sana,kaa nae in written,shida ni peaneni tarehe,na conditions,sioni baya!....Mimi nataka kumlipa mwenye nyumba kodi kila mwezi, ninaweza kujisimamia mwenyewe na pesa zangu, sioni sababu ya kumpa mwenye nyumba mkopo usio na riba badala ya kuongeza mtaji wangu kufanyia biashara hizo pesa za miezi mitano ya ziada ninayompa.
Wala hatulazimishi. Huu ni utaratibu tu tuliojiwekea. Kama hutaki jenga nyumba yako, au jenga nyumba zako halafu pangisha kwa kodi ya mwezi mmoja mmoja.Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.
Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.
Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
Wafanyabiashara wengi wa Kariakoo wameshakuwa na ule ujinga wa baadhi ya wenye nyumba ambao hawakupi nyumba bila kuja na dalali. Hapo hata ukimuambia mwenye duka hujaja na hao matapeli wanaoitwa winga bado tu atakupiga cha juu ampe huyo winga baadaye.Bidhaa 5k utaambiwa 15k ili winga nae apewe.
Wengine wanakufata nyuma ukiingia dukani anajifanya mmekuja wote ili mwenye duka amkatie hela.
Mimi huwa namwambia mwenye duka huyu dalali sijaja nae.
Mmejiewekea kwa makubaliano ya nani wakati hata kodi hamlipi serikalini wala risiti hamtoi??Wala hatulazimishi. Huu ni utaratibu tu tuliojiwekea. Kama hutaki jenga nyumba yako, au jenga nyumba zako halafu pangisha kwa kodi ya mwezi mmoja mmoja.
Wengine wanakwepa usumbufu.
Wabongo wengi kulipa kodi kwa wakati ni mtihani.
Sasa ukimruhusu alipe kila mwezi ni shida.
Huu uzi utawajua wenye nyumba na sisi wapangaji.Wala hatulazimishi. Huu ni utaratibu tu tuliojiwekea. Kama hutaki jenga nyumba yako, au jenga nyumba zako halafu pangisha kwa kodi ya mwezi mmoja mmoja.
Miezi 3 yenyewe ni usumbufu! Hiyo ya kila mwezi si ndiyo itakuwa usumbufu mara dufu! Unampigia mpangaji hapokei simu! Akipokea anakupanga atatoa ndani ya siku 2 zijazo! Na zikifika hizo siku 2, hatoi! Usumbufu tu
Mjomba kila mwezi kodi inakatwa kupitia LUKU. Halafu Mjomba nyumba inajengwa kwa fedha. Unategemea hizo fedha zinarudi kwa mkupuo, au ni baada ya miaka mingi kupita? Mnataka na risiti za nini tena?Mmejiewekea kwa makubaliano ya nani wakati hata kodi hamlipi serikalini wala risiti hamtoi??
Mjukuu wangu mimi mwenyewe hapa nilipo ninaishi nyumba ya kupanga. Hela yote ya mafao aliitafuna mke mdogo. Baada ya kugundua imeisha, alinikimbia. Nyumba imeishia kwenye renta.Huu uzi utawajua wenye nyumba na sisi wapangaji.
Shikamoo baba mwenye nyumba...!
Kodi ya luku ya jengo analipa mpangaji, nyie wenye nyumba mnatakiwa mlipe kodi ya mapato kutoka kwenye kipato cha wapangaji wenu.Mjomba kila mwezi kodi inakatwa kupitia LUKU. Halafu Mjomba nyumba inajengwa kwa fedha. Unategemea hizo fedha zinarudi kwa mkupuo, au ni baada ya miaka mingi kupita? Mnataka na risiti za nini tena?