HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Nadhani tumekariri; tumemebeshwa taratibu za nchi za Kimagharibi, ambao hutoza kwa mwaka au nusu mwaka.
 
Nadhani tumekariri; tumemebeshwa taratibu za nchi za Kimagharibi, ambao hutoza kwa mwaka au nusu mwaka.
Nchi za kimagharibi hazifanyi huu ujinga, hata nchi karibia zote zilizotuzunguka hazina huu utaratibu.
Huu ni utaratibu wa Kiswahili tu.
 
Mkuu, unazungumza kana kwamba mpangaji hawezi kukosa hela ya kodi endapo atalipa kodi kila mwezi.

Kuna wenye nyumba ambao huweka masharti kwa wapangaji wapya kulipa kodi ya miezi mitatu au sita mapema, kisha baada ya hapo wanaanza kulipa kila mwezi. Lakini pamoja na utaratibu huo, bado wapo wanaokutana na changamoto na kusumbuana na wapangaji wao. Nimeshuhudia hali kama hizi.

Kama lengo la kuweka masharti hayo ni kupunguza usumbufu wa kufuatilia kodi, ni muhimu pia kuangalia sababu nyingine zinazosababisha migogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji, kwa sababu malipo ya awali pekee hayawezi kuwa suluhisho kamili.
 
Watu wanaosumbuana kulipa bills ya maji ya mwezi isiyozidi 30k unataka wakulipe kila mwezi Kodi ya chumba/nyumba?
Usumbufu wa kulipa Bills za maji ni kwa sababu watu wana changia, hata umeme ilikuwa hivyo enzi watu wana changia mita. Siku hizi kila mtu ana luku yake watu wanalipia na hakuna mpangaji analala giza.
 
Usumbufu wa kulipa Bills za maji ni kwa sababu watu wana changia, hata umeme ilikuwa hivyo enzi watu wana changia mita. Siku hizi kila mtu ana luku yake watu wanalipia na hakuna mpangaji analala giza.

Unahoja lakini hoja yako Haifai katika mazingira yetu.
Watu wakiweza kuthamini mali za wengine, kutunza ahadi hoja yako itakuwa na nguvu
 
Unahoja lakini hoja yako Haifai katika mazingira yetu.
Watu wakiweza kuthamini mali za wengine, kutunza ahadi hoja yako itakuwa na nguvu
Sioni namna gani kumlipisha mpangaji kodi ya miezi sita kunamfanya athamini nyumba, pia sioni namna gani akilipa kodi ya mwezi mmoja na mmoja wa tahadhari(deposit) kutamfanya asithamini nyumba aliyopangishiwa.
 
Hakuna mtu msumbufu kama mtu mweusi kwenye maswala ya fedha mtazungushana hadi umkatie Tamaa
Hujawah pangisha sio? Hebu jaribu halafu waambie walipe kila mwezi halafu uje utupe mrejesho
Watu weusi wengi wanatumia utaratibu huu, kuna mtu mweusi kutoka nchi ya jirani namsaidia kutafuta nyumba ya kupanga anashangaa sana huu utaratibu wetu, kwao ni mwezi mmoja mmoja au miwili tu wa pili ukiwa ni kama pesa ya tahadhari ambayo itarudishwa yote au kiasi wakati wa kuhama kama mpangaji hajafanya uharibifu mkubwa .
 
Naunga mkono hoja, Haingii akilini kabisa Shirika la Nyumba(NHC) lenyewe kodi unalipia kila mwezi husika iweje watu binafsi wadai miezi sita: kwa kuongezea hilo DALALI kuchukua kodi ya mwezi mmoja yaani kama kodi ni 300K, unamlipa mwenye nyumba 300x6 + 300K ya dalali, ni mambo ya kufanyia kazi haya.
 
Sisemi mpangaji hawezi kukosa pesa ya kulipa ikiwa ni kwa mwezi mmoja mmoja, ninachosema ni kwamba usumbufu ni mkubwa zaidi kadri miezi ya kulipa inavyokuwa mingi kwa sababu wengi wanaopangisha huwa hawana hiyo pesa nyingi kwa mkopo ila ikiwa ni kwa mwezi wengi wanaweza kulipia kwa wakati, huu ni uzoefu na common sense tu.
 
Hela ya broker ni makubaliano tu kati ya mteja na dalali, sehemu nyingi wala watu hawampi dalali kodi ya mwezi, mimi huwa nawapa ya nusu mwezi tu.
Upo sahii kwa muktadha huo.

Mimi nmeongelea kwa baadhi ya nchi ambapo wamerasmisha sekta hiyo na dalali analipa mpaka kodi serikalini...

Sio hawa wetu.
 
Nature ya wapangaji pia ni changamoto....mtu kila mwisho wa mwezi anaomba kwamba kuna ishu anaisikilizia....so sometimes ni rahisi kwa mwenye nyumba ili kuepuka usumbufu pia ... angalau unachukua kodi ya miezi mitatu na kuendelea...ili kila mtu apambane na mechi zake
 
Hebu jaribu uone atakavorundika madeni Kodi ya mwez huu Italipwa mwez ujao
 
Wabongo wengi hawana culture ya kulipa madeni bila ugomvi, na kisheria namna ya kuwabana wakulipe ni kama haipo, dawa ni hiyo miezi sita, kama una nyumba jaribu then baada ya miezi 3 tuletee mrejesho 😁
 
Ili ujenge yakoo

Shtuka amkaaa
 
Mpwaa unaoongelea wana nyumba za kupangisha kama zotee sahau huruma si sioo malezziii m nalipa miezi 3 toka nasoma wewe uko.kazini lipanaa tu hamna jinsi

Ila ilinsaidia kununua kiwanja na kujenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…