Rivers walikalili kuwa Yanga ndio ile ile walioipiga nje ndani msimu uliopita, wakawachukulia poa. Sasa wameona wana mlima mrefu sana wanatafuta namna ya kupata sababu ili wapate ushindi wa mezani au tu kuich
afua Yanga. Kabla ya Yanga kucheza na Rivers, ilishacheza mechi na timu nyingi tena zingine ni ngumu zaidi ya hao Rivers na zingine zilishatangulia kumfunga wakiwa kwao lakini timu zote zilizocheza na Yanga hakuna hata timu moja iliyowahi kuripoti kuhujumiwa na Yanga kwa sumu.
Leo hii timu iliyofungwa goli mbili wakiwa kwao ndio eti waje wahujumiwe na Yanga kwa kipi zaidi wakati timu ipo mbele kwa goli mbili? Mambo mengine yanachekesha sana