Hapana,
Lakini hata ambavyo havipo navyo huwezi kuthibitisha.
Sasa unajuaje kwamba usichoweza kuthibitisha hiki huwezi kuthibutisha lakini kipo na kile huwezi kuthibitisha lakini hakipo?
Kuna kitu ambacho kinatokea nafsi mwangu kinachohusiana na kuamini Mungu. Hivyo nawe ukitaka uthibitusho ni kuamini naamni Mungu atajidhirisha kwako pia Kama ambavyo amewahi kujidhihirisha kwa waumini wenzako wengi.
Nashukuru kwamba umekubali kwamba uwezo wangu wa kuthibitisha au kutothibitisha hauwezi kuondoa uwepo wa kitu au kufanya kiwepo kitu kisichokuwepo.
Nimekueleza wazi kwamba Mungu hujidhirisha kwangu Mara nyingi katika nyendo za maisha yangu lakini pia kupitia maandiko ya Biblia nimepata kufahamu kuwa yeye ndiye muumba wa ulimwengu na vyote viluvyomo.
Na uthibitisho zaidi ni pale ambapo maandiko ndani ya biblia yamezungumzia kuhusu mwanzo wa ulimwengu na nyakati na vyote vilivyomo ulimwenguni ikiwa ni pamoja na dunia na vilivyomo.
Lakini Sayansi imethibitisha ukweli kwamba ukimwengu Una Mwanzo na Wakati pia Una Mwanzo.
Hivyo kwangu sayansi imetujuza kitu ambacho waamini Mungu tulikuwa tumejuzwa na Mungu mwenyewe.
Wakati sayansi bado inahangaika kujua chanzo cha uhai na haijui kabisi nini maana na madhumuni ya maisha/uhai lakini Mungu amekwisha toa majibu ya maswali hayo.
Sasa ni zamu yako uniambie ni kwa vipi kushindwa kwangu kukuthibitishia kuwepo kwa Mungu na kukiri kwako ya kwamba sina uwezo wa kuthibitisha chochote kumekufanya wewe uhitimishe kuwa hicho nilichoshindwa kuthibitisha hakipo !
Mimi siwezi kuhangaika kabisa na ambavyo havipo na sijajua kwa yakini Kama akili yangu itaanzia wapi kuhangaika na visivyokuwepo. Sipati mantiki ya namna MTU anavyoweza au asivyyoweza kuthibitisha acha kuhangaika na kisichokuwepo ! Labda Kama yeye maamuzi yake hayana mwongozo wa kanuni za hekima na maamuiz yake ni matokeo ya vinasaba kusakata rhumba mwili mwake...