Kweli nawaambia, ili nchi hii iendelee inahitaji Rais Shupavu, Smart, Mwenye Uchungu na Nchi na Mapenzi kwa watu wake

Wawekezaji wanawekeza sehemu ambayo kuna demokrasia. Ndo Mana wakati wa dictator jpm wawekezaji walikuwa wanakimbia kwa speed ya 5G aliposhtuka akaanza kuwabembeleza akina rostam but too late
China wana demokrasia ipi?UAE wana demokrasia ipi?maana huko kute wawekezaji wamejaaa tele mpaka wanamwagika...
Heb acheni kukariri ujinga..
democracy has never been one of the factor for investment.. investor anaangalia faida, akiacha kupata faida aliokua anaitegemea anaondoka na si vinginevyo.
 
Mifumo huundwa na wananchi, hivyo wananchi imara vivyo hivyo mifumo.
Tatizo kubwa ni raia kufikiria kuwa kuna watu wa kuwajengea nchi yao.
Kodi zinakusanywa kwa ajili ya nini ?? Mavieite ?!!
 
Duh !!
 
.
Ili afilika iendelee, yafuatayo ni lazima yafanyike.

1.
Ipitishwe sheria ya kunyongwa hadi kufa kwa yeyote atakaye husika na ufisadi, wizi na ubadhirifu wa mali za umma. Wakinyongwa kikamilifu watu wawili watatu, nchi inanyooka. Hii italeta hofu kwa wahusika wasione kodi zetu ni shamba la bibi. Rejea China, hii imewasaidia sana.

2.
Mishahara na marupurupu ya viongozi wa serikali ipunguzwe kwa mgawanyo wa 10. Mfano mbunge analipwa 12M, alipwe 1.2M. Hii itafanya wapiga dili wasigombee nafasi za uongozi kwani hakuna tena maslahi. Watakaogombea nafasi hizo ni wale wenye nia ya dhati ya kuwa viongozi. Mfano halisi mshahara wa raisi wa china ni kama 4.5M kwa mwezi lakini nchi za afilika, maraisi wanalipwa............Lakini unaweza kuniuliza mishahara midogo si itasababisha wakwibe zaidi? Rejea point namba moja.

3.
Kuwe dira/sera ya taifa ambayo haitegemei raisi gani yuko madarakani. Ili mtu, kampuni, taasisi au taifa lisonge mbele, lazima liwe na dira, mwelekeo. Huwezi kufika kama hujui unaenda wapi. Ni ajabu sanaa afilika haina dira! Huyu ubinafsishaji, anayemfuatia kilimo kwanza, yule viwanda na biashara, anayekuja utalii etc etc. Ni kama genge la vichaa ambao hawajui wanafanya nn. Mfano mdogo, ni miaka 60 tangu tupate uhuru lakini hatuna maji ya uhakika wala umeme wa uhakika! Kama tangu tupate huru, nchi ingekuwa na malengo hata ya miaka 10 kumaliza tatizo 1 kati ya haya, leo yangekuwa historia.
 
Mimi naungana nawe katika haya uliyoandika hapa, hasa namba moja na tatu. Namba mbili inahitaji kufanyiwa marekebisho kidogo tu.
Isiwe ni kutafuta ufukara kuingia kwenye siasa, lakini ninakubaliana nawe kwenye hoja ya msingi kwamba siasa kisiwe kichaka cha wahujumu na utapeli wa nchi.
Siasa iwe ni kuvutia watu wenye uwezo na wanaojitoa kulitumikia taifa kwa dhati, huku taifa nalo likitambua kazi yao nzuri wanayofanya.
 
100% correct
 
100% correct
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…