wazazi waliitilia mashaka hiyo kazi ndo maana na mimi nikaielezea hiyo kazi kwa namna yangu inawezekana wazazi wamekosea kuingilia uhuru wa mtoto wao kuchagua mpenzi anayemtaka.
Huyo mke huenda ndiye angeenda kututengenezea mume tycoon wa bodaboda kwa kumshauri vizuri mume wake jinsi ya kui modernize business, kuipatia technology ya app na tracke, online payment, na kumfanya mwanetu awe bonge la CEO wa bodaboda.
Ila ndiyo hivyo tena, imekuwa si riziki!
Unajua nini? Huwa nakaa naangalia Wamarekani wanatengeneza biashara kama Uber, halafu nikisoma historia zao, nagundua kwamba hawakuwa na chochote zaidi ya idea nzuri tu ya biashara, idea ambayo ukimpa Mtanzania wa kawaida kabla haijaletwa na watu wa nje, anaidharau, atasema "hii mbona biashara ya bodaboda". Kumbe mtu akijishusha akaisoma biashara hata ya bodaboda na kuleta solutions kuifanya iwe bora, anaweza kufanya biashara kubwa sana.
Lakini, sisi tumeishia kuona "hii biashara ya bidaboda".
Granted, naelewa kuna tabu za mitaji na kukubakika, but still, siku hizi ukiwa na idea nzuri unaweza kupata mitaji hata kutoka nje.
So, tusipende kudharau watu kwa sababu ni bodaboda tu.
Kuna mabinti hawaangalii mtu alipo, wanaangalia huyu ana uwezo wa kuwa wapi miaka 5, 10 na zaidi ijayo. Tunaweza kujenga future gani?