Kwenu Wanaume, Mwanamke akikuletea Zawadi jua ni mtego, atachukua kwako mara 2 yake

Uliyoongea yote 'mswano', lakini umesahau lile la muhimu kuliko yote, lile la kuboost upendo.

Unapopewa zawadi na mwanamke, lazima ujikute unahamasika na kujiona unapendwa.

Hata ile nje ya mapenzi, zawadi huwa ni deni la fadhila, ni lazima tu ulilipe.
 
Kwa utafiti wangu mdogo:

Wanaume wenzangu tukae na watoto wetu wa kiume na usimuachie mwanamke suala la malezi hasa mtoto wa kiume peke yake.

Mtoto anajifunza kwa kuona zaidi, akiona baba yake jinsi anavyopambana kwenye himaya yake na kutafuta suluhisho kwenye matatizo mbaimbali humjenga mpaka ukubwani.

Mwanamke ana sehemu ndogo sana kwenye malezi hasa ya mtoto wa kiume na sehemu yenyewe ni huruma! Huruma siyo malezi!

Dunia haina huruma kwa mtoto wa kiume! Mtoto wa kiume akilelewa kiume na baba yake hawezi kulalamika hata siku moja kwenye jambo lolote hata liwe gumu vipi!

Wanawake wameachiwa mzigo wa kuwalea watoto wa kiume, matokeo yake mtoto wa kiume lakini anakuwa na sifa za kike!

Mwanamke anaongozwa na hisia zaidi , hivyo hata malezi atayapeleka kihisia zaidi!

Huruma,kulalamika,kususa,kubembelezwa,kupendwa,kudekezwa n.k ni sifa za kike zaidi.Mtoto wa kiume akipata malezi kwa mama yake kwa muda mrefu bila baba kuingilia kati, huambukizwa hizi tabia!

Wanaume wengi kupenda kulalamika ni matokeo ya hayo malezi!

Wewe mwanaume uliyetelekeza mtoto wako hasa wa kiume ujue unaandaa mwanaume mwenye sifa za kike!

Na inawezekana wewe pia ukawa za la hilo coz mwanaume kamili hakimbii majukumu na halalamiki bali hutafuta suluhisho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…