Naam, hawa viumbe acha tu, Waliosema ishini nao kwa akili hawakukurupuka, haikumaanisha kuwa hawana akili bali upeo wao ni mkubwa sana na usipokuwaa na akili za kudeal nao, rafiki yangu umeisha.
Sasa basi Mwanamke akikuletea zawadi wewe Mwanaume iwe ya sikukuu au yoyote ile, iwe fedha au zawadi maarufu kwao ya soksi na vest au boksa kama atajiongeza sana basi jua, gharama ya kununua vitu hivyo atairudisha kwake na faida juu.
Jua siku za hapo karibu au kama hana aibu siku hiyo hiyo aliyokupa zawadi atatengeneza tukio la kukuomba pesa kubwa zaidi ya gharama zake alizotumia kukununulia zawadi, kama katumia 20000 anaweza kuomba Elfu, 30, 40 au 50 kabisa na wewe kwa sababu ya furaha ya zawadi ukampa usijue kakuuzia zawadi kwa gharama mara 2 au 3 ya gharama aliyonunulia.
Wanawake ni wajanja sana, wanajua kucheza na ufahamu wa wanaume waweze kula fedha zao.