Kwenu wanaume wema: Bado mpo na Mungu, awape maisha marefu sana sana!!

Kwenu wanaume wema: Bado mpo na Mungu, awape maisha marefu sana sana!!

Nimesoma kidogo sijaona ulipoomba afu 15 ya kusukia. Itakua ndio sababu umeipata ndoa.

Pia wakati mwingine jitahidi hata kaparagraph kamoja kupongeza Serikali ya Mama.
hey, napenda kua natural, halafu nina asili flani ya nywele bila hizo za kuunga zinaenda poa sana yan za mkono tu haizid hata elf tano na nilikua nasuka kwa hela zanguniliwah kuomba nauli tulishakua deep and madly in love sio kuwa sikua nashindwa kuomba hela lakini mtu ndio anajikusanya hata maisha yake hayakua vizur lakini nilipenda spirit yake ya kutafuta nikasema sasa hata nikimuomba hela s namuongezea majukum
 
Story yako mwanzon inafana Na yangu...tulikutana kanisan Ibada ilivoisha kwenye kusalimiana....the way alivokua ananiangalia while tunaongea made me fall in love with him hata siku alivokuja kunifungukia sikupoteza muda Kesho yake nilimpa jibu la yes
Ndo huyo ambaye amekuacha juzi hapa 🤔
 
Naona kuna mtiririko wa mada nyingi za kukataa ndoa, kwanza niseme mimi nimeolewa na mume ambaye sijutii, hakika sijutii kabisa kuolewa naye tulianzaje bas kisa hiki nina imani kitakua na namna flan ya kufundisha hata kutia moyo wale ambao mioyo ilishakufa zamani kuhusiana na ndoa au mahusiano thabiti

Fast forward hiki kisa kinanihusu mm japo kuna vitu sitaexpose sana na 95% kinanihusu mwenyewe.

Ilitokea siku moja nimekwenda mkoa fulani kwa ajili ya likizo, ni mwishoni mwa mwaka 2009, sjui nisemeje lakini sehemu niliokwenda nikakutana na huyu mwanaume ile kumuona tu kwa mara ya kwanza kuna kitu nikahisi hakiko sawa kwenye nafsi yangu na mwili wangu, nilikua natamani kumuona yan nimuone apite tu roho yangu iridhike, niko radhi khjitumisha dukan bila sababu ya msingi ili mradi tu nimuone na ilikua tukionana tu lazima atabasam bas mm mwenzie nakua hoi sijiwez.

Nikajikaza mtoto wakike nisonekane dhaifu tenambele ya stranger,lakini tukionana lazima tupeane eye contact halafu aniachie zawadi ya tabasam lake, bas nahisi hata yeye alikua amenielewa na hapo mwenyewe sio kua nilikua virgin siku mingi ilishakwenda hivi,nilishajua mapenzi n nn yanaumaje japo sio kiviiile lakini hizo exprience tayar nilishakua nazo so hakikua kitu geni then boom moyo unamuangukia mtu hata sjawah kujua ningekuja kukutana naye,bas mimi hapo kumbuka niko likizo ugenini,

Mungu sio athumani akanipa sound unaitwa nani nikamjibu, mimi sitaki kujua yeye anaitwa nani anafanya nn anaishi wapi eneo hilo mana tunaonana tu nyumba yetu ilikua barabarani so watu wengi hupita na movements n nyingi na maduka mengi hupatikana eneo hilo karibu na kwetu, hii siku sitaisahau mimi sina subiri nikufikirie sijui kuchelewesha wakat mtu ninayemwelewa ninaye mbele ya macho yangu.

Nikatabasamu akamwaga vyombo mimi nimetokea kukupenda sana nimeona leo nikuambie tu kilichopo moyoni, mimi meno yote niliyobarikiwa nje nikamkubalia nikaondokanzangu kurud nyumbani, sasa baada ya kurud nyumban ndio akili inarudi mahali pake nikaanza kujiuliza hivi mm n mzima au kitu gani, huyu mtu nimemkubali bila hata kumpa muda wa kumjua kama kaniona mgeni mtaani anitumie tu anibwage?

Sijui anaishi wapi sjui chochote kumhusu nimeanza lini kua mwehu wa kuhangaika na mapenzi? nimesahau kilichotokea nyuma? mimi ni mtu hua napenda kusema na nafsi yangu unaweza sema niko kimya kumbe nina kikao kizito cha kunihusu, bas najiuliza hayo huku majibu hutoka papo kwa papo, mpe muda utamjua, huwez jua watu hawafanani, lakini unakiri moyoni mwako unampenda s unajiona unavyobehave juu yake, kubali unampenda, mengine utayajua taratibuu!!


itaendelea.
Seen.
 
nikaanza kuvuta picha jinsi tulivyokutana had tulipofikia nilijikuta nalia sana, nililia halaf leo ananipigia anasema et kirahisi tu mume ni mm mumeo nikasema huyu sio mzima ana wazimu unamsumbua, sjui nilala saa ngapi kuja kushtuka kunekucha nikawasha sim nikaichaji nikahisi ile ilikuandoto tu nikapotezea mchana sasa naona msg inaingia umeshindaje nina uhakika uko sehem flan nineingia asbh naomba tuonane nikajisemea kumbe haikua ndoto ni kweli tukakutana sehem ambayo alinitongoza na kunimwagia nondo kwa mara ya kwanza jaman nililia kama nimefiwa na mzazi, nililia kusema siwez machozi yananitoka alikuja na washkaj zake na mdogo wake wakiume hata siwanon namuona yeye tu mm nalia ananibembeleza ananikumbatia amebadilika akaniambia tusogee pembeni akauliza unaendeleaje? nikamjibu namuangalia simmalizi namuuliza leo hii kwa nn ukanifanyia vile unajua nimepitia nn mm? unajua mambo yanayoendelea? ananikumbatia yan nikiwa naonhea nakabwa na hasira machozi kusema siwez ananikumbatia napata amana natulia mwisho akasema kesho tukutane sehem ni beach tupate lunch tutaongea nimerudi na nimerudi rasmi kwa ajili yako narudi kwetu nawaza kikuche tuongee sjamalizana naye, usiku wa deni haukawii kukakucha tukakutana kuanzia saa saba had saa kumi ni kula kuongea ananambia umenenepa sana lakini hapo tulizika rasmi tofuauti zetu tulifungua tena ukurasa mpya wa mapenzi akanielezea anasema wewe unajua ungeweza kunipotezea mm nilikua huwez kufanya hivo na nilikua nahngaika pamoja kwamba hatukua na mawasiliano mazuri lakini sikuacha kukutafuta had kwa watu wako wa karibu ndugu zako,naomba sana Mungu nikukute hujaolewa tu, hapo nikamwambia sasa ungefanya nn kama ungenikuta nimeolewa, akasema ningekutorosha, tukacheka,najua upo upo usijali nimerudi na wakat huu siondoki tena nataka nikuoe sasa ukirudi nyumbani ongea na mama yako mgusie utanijibu niko serious, nawaza mambo mengi sasa huyu mbona anapeleka mambo mbiombio hapo ni 2018 kwwnye oktoba hivi mimi najikaza hasa namwita mama namwambia nimepata mchumba anataka kunioa ameniambia nikuambie ajue hatua anazotakiwa kupita anioe, mama yangu alikua amelala kwenye sofa aliamka akakaa vizur habari imuingie, nikashusha pumzi nikamweleza tena akasema ngoja nitamwambia kwanza baba yako ni nani anaishi wapi ni kabila gani, sjui nilipata wapi ujasiri nikamjibu haijalishi kuhusu kabila wala yeye ni mtu wa wapi mama hayo hayana maana mimi huyu ndio chaguo langu, mama yangu akaniangalia hakujibu kitu na kitu kingine mm na mama yangu hatuivi sana muda mwingi kila mtu na mambo yake saa zingine anaweza mkaamka mtu kakununia bas kipindi niko na huyo shemeji yenu alikua ananipa sana amani ananituliza na natulia, nikaona huyu mama anataka kunipeperushia njiwa niliyemfuga mwenyewe kwa muda mrefu ,skupata jibu direct lakini nikamwambia nineshamwambia mama kasema ataongea na baba, siku zinakatika sijibiwi baba kasema nn mimi tena nishamsevu mchumba jina jipya akipiga niko huru kabisa kuongea sijifichi tena, sasa baba yangu alikua anaumwa na nakumbuka sikujua kama ni serious sana alikwenda kupata matibabu zaidi, kumbe hizo habar hata mama sjui kama alisema au la lakini mzee wangu akafariki, tukazka na ikatokea kama coincidence baba yangu mkwe n baba yangu wana unasaba so alikuja kuzikwa ilibidi mzee aletwe alipotaka kumalizia uzee wake tukazika, maish sasa yakabadilika tuna mama tena hana bazi tunamtegemea yeye kwa kils kitu sasa kaz at least nna mtu ambaye ananisupport ilibidi tu wazee wake waje wapose tukafuata taratibu bi mkubwa akaniozesha hiyo ilikua dec 2018 had leo tupo pamoja tumevuka vingi nimefupisha story mana visa n vingi hapo katikati, lakini iko hivi mwanaume anakwambia mimi ndio najua kwa nn nakuoa na kwa nn nimekubali kuanzisha familia n ww kaa tulee watoto tuzikane maisha ndio haya haya, nilijiambia pia huyu ndio mtu abaye nilitaman aje awe mwanaume wa maisha yangu, hakuna kigeni nisichokijua chini ya jua hili,natakiwa kutuliza akili namjua ananijua tunafahamiana vya kutosha so dec 2018ndio tulipoana had leo hii tuna watoto wawili sjawahi kumhesabia makosa, ni mwepes wa kusamehe i dont care anaishije nje ya ndoa yetu ninachoangalia he respects me, anajus kutimiza wajibu wake kama baba kama mume, kuna muda tukikaa hivi tunakumbushana story za nyuma tunacheeeka ndio tunakumbuka daah kumbe tumekata miaka sio haba tuna watoto wawili wakike wote tumewapata baada ya kuoana alijua kunimezesha ptwo yan huyu ubavu wangu haukunywewa supu kabisa ni sahihi Mungu amenipa yule niliyemtaka niliyemataman enz hizo nilikua najiambiaga nipate mume ambaye tutaendana so jaman watu wema wapo, sisemi ndoa yangu ndio ndoa bora kuwah kutokea tunahitiliafiana lakini ni mara chache na zenye kuhesabika tunachojali ni amani furaha siwi kikwazo cha kumkosesha furaha na sipendi akose raha Mungu anitunzie huyu mume wangu, aamin




mwisho.
Seen
 
Hapo Kwenye kununa wanaume Tunateseka Unakuta Mtu Ananuna tuu Na Kazi Hupewi Daah Basi Inabidi Ubembeleze Sanaa Ndio Mambo yanakaa Sawa Na Kazi Unapewa Ila Kweli Bible Haisemi Uongo Kwamba ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI HAPO NI KWELI
Mwee mnawadekeza wake zenu....yaani jitu nalilisha nalivalisha lininunie,, alooh. Atanunaa mpaka kufa kwake.
 
Mwee mnawadekeza wake zenu....yaani jitu nalilisha nalivalisha lininunie,, alooh. Atanunaa mpaka kufa kwake.
mkioana sio kua kuishi kwa mahaba ndio basi tena, kuna mahaba na mawaa upo baba weee huwezi achia wenzio,
 
Back
Top Bottom