Kwenu wanawake: Hakika, hakuna mstari wowote katika Biblia unaomwadhibu wanaume mwenye wake wengi

Wanaume tumeumbwa na matamanio makubwa sana hilo liko wazi ila sio kwamba tunashindwa kujizuia.

Acheni uzinzi mbona kuwa na mwanamke mmoja uliempenda ni bora pia ina faida nyingi kuliko kuchomeka chomeka.
Pia utaheshimika zaidi na jamii
Haya matamanio tuliyopewa ni kipimo cha uvumilivu wakiume kuweza kutulia kwa mkeo.
(Usiache hisia zikuendeshe maana siku zote utaishia kufeli "Farid Kubanda")

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleeza vema sana mkuu.
 
Umeelewa swali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sitaki kwenda huko unapotaka,we umesema uzito hauonekani kwa macho hivyo maana yake kuna kuona tofauti na kutumia macho na ndiyo maana nikasema mie sijakusudia kuona kwa kutumia macho na nikafafanua nilichokusudia.
UHURU JR nimekuelewa vizuri ila kukujibu swali lako litadiverge lengo la mada...jus be patient tutafika huko.
 
Maandiko yana tafsiri nyingi, kama haikuandikwa kwa uwazi kama ilivyo kwa mwanamke basi isichukuliwe moja kwa moja kuwa hakuna mahali mwanaume anabanwa

sent from my Tecno W3
 
Na hilo aliloliongelea paulo ni rai yake si sheria.

kama umesoma vizur
Mkuu ni mpagani? Kusoma biblia haitoshi, sharti utafakari neno la Mungu Mchana na Usiku; Kwa watu wanomjua Mungu katika biblia hakuna kitu kama Rai yake kama ambavyo umesema. As long as imetolewa na mtumish wa Mungu Paulo au uamini au Usiamini ila sio Rai yake tu, ni kitu ambacho binafsi naweza sema kimetoka kwa Mungu mwenyewe, ila paulo akakisema.
Na simply Mungu ametupa sisi nafasi ya Kuchagua So ukitaka kuona hilo kama ni Rai ya Paul ni swa pia, ila ukitaka kuona kama ni Maelekezo kutoka kwa Mungu ni sawa pia.
 
Biblia Takatifu haijawahi kumruhusu Mwanamke kumuacha Mumewe kwakuwa tu Amezini ila Mungu ndiye atakayemwadhibu Mwanaume huyo.


Kama unapinga hili...LETE MISTARI YA BIBLIA.

Wanaoelewa vifungu vya biblia tayari wameshakuwekea.
Mungu si mjinga aruhusu Mke anung'unike moyoni kisa tu biblia inasema hawezi akamuacha mume ambae amezini nje ya ndoa. Mnatake advantage ya unyonge wa mwanamke ili tu kujustify tamaa zenu za mwili. Huyu Mungu ninayemwamini mimi sidhani kama ni katili kiasi hicho. Ingekuwa hivyo basi asingetuumba tuwe na wivu au hisia.
Mke avumilie uzinzi wa mume lakini yeye akishikwa na matamanio kwa mwanaume mwingine akatoka nje basi linakuwa kosa na anaadhibiwa kikatili.
Ni Mungu yupi huyo mnayemzungumzi??
Kama siku ya mwisho Mungu ataniadhibu kwa kutoshika mistari ya biblia na iwe hivyo. Lakini kwa sasa nitasimamia msimamo wangu kuwa. Ndoa ya kikristu ni mke mmoja na mume mmoja tu, amri ya uzinzi inawahusu wote wawili kwa uzito ule ule.
Ukichepuka acha kuhalalisha upuuzi wako.
 
Ninavyo jua

Kutokana na asili ya uumbaji ambao tumejikuta tu tumeumbwa hivyo,

Mwanamume ndiye anayemwoa mwanamke.
Mwanamme anaweza kuoa wanawake zaidi ya mmoja.

Hivyo mamlaka ya kutaliki anayo mwanamume kwani ndiye aliyeoa.

Sababu za kutaliki anazo mwanamme kwani ndiye aliyeoa.

Hapa mwanaume ni mtendaji (subject) na mwanamke ni mtendewa (object)

Mwanamke hana mamlaka wala sababu za kutaliki, (kutoa talaka)

Akiona ndoa imemshinda anamwomba mumewe ampe talaka.

Mme akikataa kutoa talaka, mke anaenda kuziomba mamlaka kama za dini mf. (kanisa mchungaji) au
Selikari (mahakama hakimu)
Ili zimshawishi au kumlazimisha mumewe atoe talaka.

Vitabu kalibu vyote vya dini vinampa mwanaume mamlaka na sababu za kuoa na kutaliki.

Hii inatokana na ukweli kuwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi, anajitambulisha kama Mwanaume.
Hivyo amemrithisha binadamu mwanamume nguvu ya kuitawala dunia pamoja na kumtawala Mwanamke.

Nawasilisha
 
WE BANA WEE
ZINI KIVYAKO NA SIE TUZINI KIVYETU!
mambo ya kujadili uzinifu na biblia msitufanye tushindwe kwenda kanisani!
 
TALAKA NI NINI?
AHAHHAHAHHAHA NANI ANASUBIRI TALAKA SIKU HIZI?
WE BAKI NA MAMLAKA yako
 
Hizi zote ulizoandika tunaziita Mboyoyo....!

Naam... kwasababu ni mtazamo wako.

Mimi sijahitaji Mboyoyo...nimehitaji Mistari ya Biblia inayomuamuru Mwanamke kumuacha Mume wake kwa ajili ya uzinzi.
 
WAPI ULIAMBIWA MUNGU ANA JINSIA!?
yani mnajiaminishaga vitu vya kiwehuuuu!
ETI MUNGU ANAJITAMBULISHA KAMA MWANAUME!
 
Ni kweli kabisa.
 
Hizi zote ulizoandika tunaziita Mboyoyo....!

Naam... kwasababu ni mtazamo wako.

Mimi sijahitaji Mboyoyo...nimehitaji Mistari ya Biblia inayomuamuru Mwanamke kumuacha Mume wake kwa ajili ya uzinzi.
Jukwaa la dini wanaweza wakakusaidia
 
WE BANA WEE
ZINI KIVYAKO NA SIE TUZINI KIVYETU!
mambo ya kujadili uzinifu na biblia msitufanye tushindwe kwenda kanisani!
Nani amekuagiza au amekuzuia kuzini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…