Kwenye haya Maisha kuna watu ni untouchable , hii nimejifunza kwa njia ngumu.

Duh! Hatari
 
Hii nimeiona hata kwa baba yangu, wengi wanaomzingua huwa wanafariki ghafla. Yeye mwenyewe haelewi inakuaje
 
Katika maisha ya binadamu tunapitia zama nyingi sana na kila zama ina kitabu chake. Tunajaribu kutafakari kama ipo siku ambapo mambo yote yatakuwa sawa? Zama hizi kuna mambo yapo vizuri sana lakini eneo la baadhi ya watu kuwa unteachable hili nalo ni Kero kubwa ingawa wadau hawaoni kwasababu madhara yake unaweza kuyaona endapo utavaa miwani ya kuona mbali.
Msingi wa yote haya inawezekana ni kukosekana kwa uwajibikaji mfano ulio wazi ni huduma za jamii zimezorota karibu kila Sector wahalifu hawashtakiki kwasababu wapo baadhi ya wasimamizi wa Sheria wamejipanga kubadili ukweli kuwa uongo. Wananchi hawajali kama vile nchi hii haiwahusu.Nini kifanyike? Utawala wa juu watafute mbinu ya kubaini wanaokwamisha juhudi kwa maksudi,Muhari iwe ni kosa la jinai ili kukabiliana na wizi wa kiufundi pamoja na ubadhilifu.Viongozi wasiofaa wanajulikana lazima nguvu itumike kuwaondoa na wasipewe fursa ya kugombea nafasi.Hakuna Chama kibaya bali watu wanaokizunguka Chama wanahujumu Chama kwa maslahi binafsi.
 
Situmii chochote ila nikimwambia mtu au kumuwazia baya basi anza kuhesabu masaa ,siku,mwezi,mwaka mda wowote
Ivi vitu ulivyovitaja vipo kiroho sana, wenzetu waislamu wanajua
Sekunde, Dakika, masaa, siku, wiki, miezi, miaka
Ivi vitu vipo kiroho
 
Situmii chochote ila nikimwambia mtu au kumuwazia baya basi anza kuhesabu masaa ,siku,mwezi,mwaka mda wowote
Ivi vitu ulivyovitaja vipo kiroho sana, wenzetu waislamu wanajua
Sekunde, Dakika, masaa, siku, wiki, miezi, miaka
Ivi vitu vipo kiroho
 
Duh! Hatari
Hatari kweli.
Nikiota vitu fulani sisemi naogopa itakuwa kweli.
Pia nawasihi watu Kuna vitu ukiota usiwaambie watu bali omba kwa imani yako visitokee kama Ni vitu vibaya.

Niliota kifo cha kiongozi mmoja wa nchi flani niliyekuwa namkubali Sana.
Jamaa alikufa kweli ndani ya miezi 5 hadi 8.
Katika ndoto kisichotimia ni machafuko na kuuwawa siyo kifo cha kawaida. Niliota atauwawa na kukatokea machafuko.

Nilikuja kumsimulia mtu mmoja tu baada ya kifo cha jamaa. Sikuwaambia watu baada ya kutimia ndoto wangeniona mwongo, mbona sikusema kabla?
 
Kuna jamaa mmoja marehemu sasa,alikopa pesa bank na hakuwahi kufanya marejesho ila kila meneja aliyekomaa ana inshu ya kupiga mnada nyumba alikufa zaidi ya mameneja watatu walikata moto.

Hadi ile nyumba wakaiogopa,hadi leo ile nyumba ipo,bina damu wana mambo.
 
walilishwa utotoni na wazazi wao, hakuna cha natural wala nini.

Ila ziko nguvu za asili kweli. mimi huwa nikiota tukio kubwa huwa lipo au linakuja au lilitokea.

Kuna wakati nikimwapiza mtu 75% litamkuta.

Lakini hilo wanalosema mtu akimtafuta anapoteana ni nguvu nzuri za giza ambazo mhusika ama alizitafuta au alipewa utotoni.
 
Ushuhuda mwema kabisa ,kula5!
 
Huyo nae kiboko,kukopa akope,mrejesho wafe wengine!
 
Basi utakuwa na pure heart, Ogopa sana innocent man unayemfanyia ubaya na asikuchukie wala kukukusudia lolote baya.
 
Ana kinga ya kufa mtu au mizimu yake inamlinda. Ukitupa bomu linarudi kwako mara mbili. Ndio maana nakazia kuwa achana na hizi dini za kigeni, zingatia jadi yako.
Mtu pekee dunia hii ambaye huwezi kumloga na utakufa ukiendelea kujifanya ngangari ni Mkristo wa Kweli kabisa, nasema sio kila Mkristo, bali ni Wakristo wachache kabisa pengine 1 kati ya 10,000. Nafikiri ndio hao jamaa alikutana nao akakiona cha moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…