Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikikukataza kitu usifanye nikakupa tahadhari kitakacho kutokea ukapuuzia basi lazima kitatokea.
Wapo ndugu, rafiki na vijana wa wangu wa kazi wameshuhudia hilo.
Wengine nikisema kitu wanaogopa wananisihi nisiseme hivyo.
Sasa kama nakiona na najua madhara yake naachaje kukupa tahadhari?
Nikiota ndoto flani lazima nisikie habari ya msiba wa mtu ninaye mfahamu. Nikiota tu nawahi kuomba usiku huo huo isitokee kwa ndugu au rafiki wa karibu.
Bibi yangu alikuwa na uwezo wa kutafsiri(kuagua) ndoto. Nadhani nimerithi karama hizo toka kwake.
Ivi vitu ulivyovitaja vipo kiroho sana, wenzetu waislamu wanajuaSitumii chochote ila nikimwambia mtu au kumuwazia baya basi anza kuhesabu masaa ,siku,mwezi,mwaka mda wowote
Ivi vitu ulivyovitaja vipo kiroho sana, wenzetu waislamu wanajuaSitumii chochote ila nikimwambia mtu au kumuwazia baya basi anza kuhesabu masaa ,siku,mwezi,mwaka mda wowote
Hatari kweli.Duh! Hatari
Narudia tena, amebakishwa kuja kutoa shuhuda, regardlwss awike kama jogoo au mteteaHapa ndio huwa mnaonekana kituko. Makonda mwenyewe ndo kwanzaa anawika kuliko lissu
Ushuhuda mwema kabisa ,kula5!Kuna wakati, nikiwa kijana kabisa, nikiwa nimetoka kumaliza masomo ya chuo kikuu, na ikumbukwe kabla ya kumaliza chuo nikiwa nimetoka likizo, nilisurika kwenye ajali mbaya kabisa ya basi lililogongana na lorry na kisha kushika moto, na watu wengi kupoteza maisha. Baada ya kumaliza masomo, nilipata kazi, nikaenda fieldwork vijijini ndani kabisa huko Dodoma nikiwa na gari na hema.
Nilikosa nyumba ya kupanga na hapakuwa hata na guest house. Nikaupata mti mmoja, mbuyu mkubwa sana wenye kivuli kikubwa, na chini hakuna nyasi kabisa, nikaweka hema langu chini ya huo mti. Kama ilivyo kawaida yangu, kila siku kabla ya kulala, nilipiga magoti kumshukuru Mungu na kuomba mwongozo wake. Niliishi bila kuona kitu chochote kisicho cha kawaida.
Siku moja, mtu mmoja akaja akiniomba nimsaidie kwa sababu mke wake amerogwa, alisema mengi. Kwa kweli nilichukia, kwa nini afikirie kuwa mimi naweza kumsaidia kwenye mambo ya kurogwa, nami sijawahi kujishirikisha katika ushirikina katika maisha yangu yote? Nilipomkatalia, aliendela kunibembeleza. Alipoona nimechukia na nazidi kumwuliza kwa nini anafikiria mimi naweza kumsaidia kwenye ushirikina?
Akasema kuwa pale kwenye mbuyu mkubwa nilipoweka hema, wachawi wote wa kanda ile ndipo huwa wanakutanikia, lakini tangu nimeweka hema langu, hakuna anayeweza hata kusogea. Akadai kuwa kuna mchawi kiongozi wa eneo hilo, yeye alilazimisha kusogelea lakini nilimpiga na kitu cha ajabu, na tangu siku hiyo ni mgonjwa, hajaweza hata kuamka kitandani. Akasema kuwa hapo kijijini pao, kwenye vilabu vyao vya pombe, hiyo imekuwa habari kubwa inayozungumzwa, na watu wamekuwa wakisema kuwa mwamba huyo wa uchawi amekutana na kiboko yake, wakimaanisha ni mimi!
Nilipuuza na kuona hiyo habari nzima ni ujinga, upuuzi na uwongo mkubwa.
Ilikuwa ni kawaida yangu, nikitoka kwenye shughuli zangu, mara nyingi kwenda kanisani, nakutana na paroko kwa mazungumzo ya kawaida, maana ndiyo kampani ambayo niliweza kuendana nayo. Safari hii nilipoenda, nikamweleza juu ya habari hiyo niliyoambiwa, nikimsisitizia kuwa fikra za kishirikina zimeifanya ile jamii ya pale kuwa wajinga. Paroko alinishangaza aliposema kuwa eti hicho wanachoongea huenda ni kweli. Nikamkatalia kuwa ni uwongo kwa sababu mimi sina kabisa hizo nguvu za giza. Lakini Paroko akaniambia, siyo wewe bali kuna watu Mungu huwalinda, nguvu za giza haziwezi kuwasogelea. Nikasema kuwa kama ni kwa mantiki hiyo, siwezi kukataa.
Pia nilipokuwa huko usukumani vijijini nikitimiza wajibu wangu, niliposhinda mgogoro uliokuwepo, wakatamka hadharani kuwa wameshindwa kwenye sheria lakini hawawezi kushindwa katika nguvu zao za kishirikina, nikawaambia waniroge hata muda huo huo, na hakukuwahi kutokea chochote.
Nilipokuwa Sekondari, kuna mganga wa kienyeji alipanda juu ya boneti ya gari ya rafiki yangu, nikamshusha kwa nguvu kwa kumvuta. Akaanza kupiga kelele kuwa, umenivuta mimi, tutaona, nisilaumiwe. Sikujali. Baadhi ya watu waliokuwepo pale, watu wazima wakaja kunisihi, nikamwombe msamaha yule mzee maana ni mchawi sana, mimi nikawaambia kuwa kama ni kufa kwaajili ya haki yangu, basi wacha nife. Hakuna chochote kilichotokea.
Kuna wakati tukiwa porini tunafanya kazi maeneo ya Ngula, mkoani Geita, tukafika kijiji fulani, na vijana walikuwa na mizigo iliyowaelemea, nikawaambia tuombe tuhifadhi kwenye nyumba iliyokuwa ikionekana maeneo ya karibu. Wale wafanyakazi waligoma kabisa wakisema kuwa hiyo nyumba ni kwa mganga wa kienyeji. Nikawaambia sisi tunaweka tu mizigo, uganga ni wa kwake. Wakanifuata kwa nyumva, kwa woga. Ilikuwa majira ya saa 4 asubuhi. Kufika pale nikawakuta watu wengi wametengeneza duara kama la nusu kipenyo cha meta 10. Mipaka ya lile duara ni unga/majivu. Na hakuna aliyeugusa ule unga/majivu. Watu wote waliolizunguka duara wameshika mioto inawaka. Katikati ya duara alikuwa huyo mganga, amevaa mashang na nguo nyeusi ya kujifunga. Mbele yake kulikuwa na mkuki ambao nchi yake ipo juu, na mpini haujashindiliwa kwenye ardhi, na juu ya ncha ya mkuki kulikuwa na chungu kikubwa, lakini hakianguki.
Mimi nilikatiza lile duara, nikaenda nikamsalimia kwa kisukuma yule mganga mkononi, na kumtania kuwa bamwona yupo kwenye maabara yake, akacheka sana. Nikamwomva kuweka mizigo yetu, akaturuhusu. Baada ya pale habari zikaenea hapo kijijini kuwa eti sisi ni wachawi kumzidi hata huyo mganga. Na sababu ya kusema hivyo, eti ule unga wa kutengeneza duara hakuna mtu anaruhusiwa kuuruka isipokuwa mganga pekee yake. Ukiuruka tu, unaanguka na kufa pale pale. Na kwa vile mimi niliuvuka bila ya kuanguka, basi mimi namzidi hata yule mganga. Lakini hilo mimi naamini huenda ni vitisho tu vya hao waganga il wawadanganye vizuri. Ila kile kitendo cha mtungi mkubwa kukaa juu ya ncha ya mkuki, ni ngumu kuielezea.
Lakini kwangu mimi mpaka leo, sijawahi kuuogopa ushirikina hata kwa kiasi kidogo kabisa. Na ninaamini ushirikina hauwezi kuishinda nguvu ya Mungu.
Tusiamini mtu ambaye hawezi kudhulumiwa, basi ana nguvu za giza. Mtegemee Mungu katika utatu wake mtakatifu, kamwe nguvu za giza hazitakukushinda.
Huyo nae kiboko,kukopa akope,mrejesho wafe wengine!Kuna jamaa mmoja marehemu sasa,alikopa pesa bank na hakuwahi kufanya marejesho ila kila meneja aliyekomaa ana inshu ya kupiga mnada nyumba alikufa zaidi ya mameneja watatu walikata moto.
Hadi ile nyumba wakaiogopa,hadi leo ile nyumba ipo,bina damu wana mambo.
Mtu pekee dunia hii ambaye huwezi kumloga na utakufa ukiendelea kujifanya ngangari ni Mkristo wa Kweli kabisa, nasema sio kila Mkristo, bali ni Wakristo wachache kabisa pengine 1 kati ya 10,000. Nafikiri ndio hao jamaa alikutana nao akakiona cha moto.Ana kinga ya kufa mtu au mizimu yake inamlinda. Ukitupa bomu linarudi kwako mara mbili. Ndio maana nakazia kuwa achana na hizi dini za kigeni, zingatia jadi yako.