Kwenye maisha usiruhusu kila mtu akuzoee ni KOSA kubwa mno pia weka muda maalum wa watu kukupigia simu

Kiujumla jamii ni Muunganiko na muingiliano wa watu mbali mbali wenye hulka, wajihi, mitizamo , utashi na maoni tofauti tofauti.........

Kwenye kila jamii Kuna makundi mbali ya wanajamii na kila kundi lina faida na hasara zake na Wewe katiba ya muongozo wa maisha yako..............

Kuishi na kubakia salama kwenye jamii zetu hizi zinazotuzunguka ni unatakiwa tu ubakie nafahamu zako katika kukuongoza kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.......

Huwezi kuwaamulia watu mitazamo yao juu yako lakini wewe unaweza ukaamua mitazamo yako juu yako.........

Maamuzi au maoni yako yanaweza yasiwafurahishe watu wote lakini hakikisha hayakuathiri wewe kwanza kabla ya kuyatoa........

Maisha ni watu na watu wenyewe ni mimi na wewe na wengine wanaotuzunguka.......tujitahidi kuishi na watu vyema na kunufaika kupitia kwao lakini usitoke nje ya taratibu na miongozo yako ili kuwafurahisha watu........

Hakuna mtu asiye na faida isipokuwa kuna watu faida zao ni ndogo sana.............


DUNIA MSONGAMANO.....
 
Maishani usipojua kuchagua yupi wa kwenda naye, hawo hawo unaojirundikia kuna siku watakutumbukiza shimonni.

Hasa watu wa karibu ndio hatari.
 
Huu uzi nafkiri kwa sisi wasukuma haituhusu maana sisi tuna salimiana kutwa mara 3 ....... yani nikae siku nzima bila kumpigia maduhu ..... hiiiii in JPM voice
 
Nakubali mazoea hupunguza heshima,,, Na mara nyingi mtu akiwa hakufahamu vizuri basi huwa na level fulani ya heshima.... kukuzoea sana inaweza punguza au kuongeza heshima...

Kingine Kijana jifunze kujali muda,,Yajue ya kuzingatia,,,na hayo mengine yote yatakaa mahala pake kwa sababu tayari unajua thamani ya Muda wako...

Kiujumla tunaita Growth.... but Ndege wafananao huruka pamoja...
 
Kweli kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watajifanya wana kujua sana kumbe sio kweli. Safi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikosa password kwenye maisha we ni fala tu.
 
Hilo nalo NENO!
 
Mimi napokea simu muda wowote na sizimi simu labda itokee nipo safarini lakini sio eti ntasumbuliwa sasa mimi ndio natakiwa nifungue njia harafu naleta vipengele ili iweje maisha yenyewe ndio haya haya...
 
Yaani huyu aana kadigrii kamoja ama tuwili nadhani,Ana kanyumba ka vyumba vinne ama vitatu na kabebi woka Fulani ivi,anakula kasarali Fulani Kama 1.5M+ teki homu na halafu benki anayo chini ya 50M. Na hajazaliwa maisha Bora nadhani Kama hajatokea bush Kama mie sijui. Saivi anajiona Kama yeye amekuwa Bora kuliko wengine anawaona Kama nzi kwake. Hajui hata anayekupigia simu usiku anajua mipaka iliyopo baina yenu.
Yaani bana hawezi ongea hivi Kama anachoma mahindi road. Sema siku akiwa Hana tuivyo tuvitu atajirudi hapa kuandika Uzi kuwa bi hambo endi lafu within pipo ,dhei keni helpi you ati enye taimu jamani
 
Kuna jamaa alikuwa hivyohivyo,sitaki mazoea sitaki mazoea.Saivi anasalimia Kilamtu nakila mtu ni msaada kwake..
Alipata ajali na gari yake tumiguu Hana anatembelea matako.Watu ni watu tu.
Hujaielewa mada. Soma upya usituharibie uzi.
 
Sijaona sababu kubwa ya kuweka limitations dhidi ya watu, kama mtu anakudharau ni tabia yake tu na atakuheshimu muda ukifika.

Binafsi mtu akinidharau nachukulia poa tu maana binadamu tunapita. Sisi sote tupo kwa muda maalam ukipita ndio basi.
 
Sijaona sababu kubwa ya kuweka limitations dhidi ya watu, kama mtu anakudharau ni tabia yake tu na atakuheshimu muda ukifika.

Binafsi mtu akinidharau nachukulia poa tu maana binadamu tunapita. Sisi sote tupo kwa muda maalam ukipita ndio basi.
Muumba wa mbingu na nchi kuna watu wanamdharau sembuse mimi kiumbe chake!!!
 
Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…