Kwenye maisha usiruhusu kila mtu akuzoee ni KOSA kubwa mno pia weka muda maalum wa watu kukupigia simu

Kwenye maisha usiruhusu kila mtu akuzoee ni KOSA kubwa mno pia weka muda maalum wa watu kukupigia simu

Kiujumla jamii ni Muunganiko na muingiliano wa watu mbali mbali wenye hulka, wajihi, mitizamo , utashi na maoni tofauti tofauti.........

Kwenye kila jamii Kuna makundi mbali ya wanajamii na kila kundi lina faida na hasara zake na Wewe katiba ya muongozo wa maisha yako..............

Kuishi na kubakia salama kwenye jamii zetu hizi zinazotuzunguka ni unatakiwa tu ubakie nafahamu zako katika kukuongoza kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.......

Huwezi kuwaamulia watu mitazamo yao juu yako lakini wewe unaweza ukaamua mitazamo yako juu yako.........

Maamuzi au maoni yako yanaweza yasiwafurahishe watu wote lakini hakikisha hayakuathiri wewe kwanza kabla ya kuyatoa........

Maisha ni watu na watu wenyewe ni mimi na wewe na wengine wanaotuzunguka.......tujitahidi kuishi na watu vyema na kunufaika kupitia kwao lakini usitoke nje ya taratibu na miongozo yako ili kuwafurahisha watu........

Hakuna mtu asiye na faida isipokuwa kuna watu faida zao ni ndogo sana.............


DUNIA MSONGAMANO.....
 
Maishani usipojua kuchagua yupi wa kwenda naye, hawo hawo unaojirundikia kuna siku watakutumbukiza shimonni.

Hasa watu wa karibu ndio hatari.
 
Huu uzi nafkiri kwa sisi wasukuma haituhusu maana sisi tuna salimiana kutwa mara 3 ....... yani nikae siku nzima bila kumpigia maduhu ..... hiiiii in JPM voice
 
Nakubali mazoea hupunguza heshima,,, Na mara nyingi mtu akiwa hakufahamu vizuri basi huwa na level fulani ya heshima.... kukuzoea sana inaweza punguza au kuongeza heshima...

Kingine Kijana jifunze kujali muda,,Yajue ya kuzingatia,,,na hayo mengine yote yatakaa mahala pake kwa sababu tayari unajua thamani ya Muda wako...

Kiujumla tunaita Growth.... but Ndege wafananao huruka pamoja...
 
Ukiwa unaingilika ingilika kirahisi utajishushia heshima weka limits za watu kukuzoea. Wengine salamu tu inatosha wasikuzoee sana

Kawaida ya mbongo akikuzoea anakushusha thamani ndo maana hata wasanii somo lao kubwa kwenye kazi zao za sanaa ni kujiweka mbali na mazoea yani kutojichanganya changanya hovyo na watu.

Maana utasikia yule jamaa msanii atakuwa yule mbana deile tupo naye hapa tunapiga naye stori ni wa kawaida mno.

Kingine usipende kuchati chati ovyo kwenye groups mtu akiwa interested kuchati na wewe akufate inbox

Kingine weka muda wa watu kukupigia simu ukiona unapigiwa simu mpaka usiku wa manane hiyo ni dharau na wamekuchukulia cheap
Kweli kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soon watakuja humu kukutukana kuwa unajiona bora na kuwadharau wengine [emoji23], lkn huo ndio ukweli mchungu hata kama huna pesa usiruhusu unyanyasike na kuchukuliwa powa, kuna muda inabidi uwe na mipaka ili uheshimike, kamwe usiruhusu watu wakuzoee sana maana watakuharibia cv
Watajifanya wana kujua sana kumbe sio kweli. Safi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa unaingilika ingilika kirahisi utajishushia heshima weka limits za watu kukuzoea. Wengine salamu tu inatosha wasikuzoee sana

Kawaida ya mbongo akikuzoea anakushusha thamani ndo maana hata wasanii somo lao kubwa kwenye kazi zao za sanaa ni kujiweka mbali na mazoea yani kutojichanganya changanya hovyo na watu.

Maana utasikia yule jamaa msanii atakuwa yule mbana deile tupo naye hapa tunapiga naye stori ni wa kawaida mno.

Kingine usipende kuchati chati ovyo kwenye groups mtu akiwa interested kuchati na wewe akufate inbox

Kingine weka muda wa watu kukupigia simu ukiona unapigiwa simu mpaka usiku wa manane hiyo ni dharau na wamekuchukulia cheap
Hilo nalo NENO!
 
Absolutely true, we pokea simu muda wotewote mana uwezi kujua simu ipi ni ya dharura na simu ipi ni ya salamu! Na hakuna mtu anayekupigia usiku halafu akuambie namalizia dakika zangu huyo atakuwa amekuzoea sana! Binafsi nilishapokea simu usiku sana kumbe kuna mzazi yupo hatua za mwisho ilibidi kuwasha gari fasta. Dharura zipo jamani pokeani simu
Mimi napokea simu muda wowote na sizimi simu labda itokee nipo safarini lakini sio eti ntasumbuliwa sasa mimi ndio natakiwa nifungue njia harafu naleta vipengele ili iweje maisha yenyewe ndio haya haya...
 
Walikuwepo watu muhimu zaidi yako walitembea na magari yenye misafara yenye ulinzi mkali na juu helcopter lakin leo wamelala peke yao chato.

Kama unataka thamani Basi wathamini watu wengine usipo mthamini mtu usitegemee kuthaminiwa kwakua kila unacho fanya utalipwa mfano wake.
Siku utakayopata dharura usiku na ukampigia simu mtu ambae humpokeleagi ndo utajua thamani ya kuthamini
Yaani huyu aana kadigrii kamoja ama tuwili nadhani,Ana kanyumba ka vyumba vinne ama vitatu na kabebi woka Fulani ivi,anakula kasarali Fulani Kama 1.5M+ teki homu na halafu benki anayo chini ya 50M. Na hajazaliwa maisha Bora nadhani Kama hajatokea bush Kama mie sijui. Saivi anajiona Kama yeye amekuwa Bora kuliko wengine anawaona Kama nzi kwake. Hajui hata anayekupigia simu usiku anajua mipaka iliyopo baina yenu.
Yaani bana hawezi ongea hivi Kama anachoma mahindi road. Sema siku akiwa Hana tuivyo tuvitu atajirudi hapa kuandika Uzi kuwa bi hambo endi lafu within pipo ,dhei keni helpi you ati enye taimu jamani
 
Kuna jamaa alikuwa hivyohivyo,sitaki mazoea sitaki mazoea.Saivi anasalimia Kilamtu nakila mtu ni msaada kwake..
Alipata ajali na gari yake tumiguu Hana anatembelea matako.Watu ni watu tu.
Hujaielewa mada. Soma upya usituharibie uzi.
 
Sijaona sababu kubwa ya kuweka limitations dhidi ya watu, kama mtu anakudharau ni tabia yake tu na atakuheshimu muda ukifika.

Binafsi mtu akinidharau nachukulia poa tu maana binadamu tunapita. Sisi sote tupo kwa muda maalam ukipita ndio basi.
 
Sijaona sababu kubwa ya kuweka limitations dhidi ya watu, kama mtu anakudharau ni tabia yake tu na atakuheshimu muda ukifika.

Binafsi mtu akinidharau nachukulia poa tu maana binadamu tunapita. Sisi sote tupo kwa muda maalam ukipita ndio basi.
Muumba wa mbingu na nchi kuna watu wanamdharau sembuse mimi kiumbe chake!!!
 
Watu wengi tunaishi na wengine kinafki kwa kuhofia tukipata matatizo tutakosa msaada wa namna moja ama nyingine!.

Mtoa mada anazungumzia limit, limit kila mtu ana za kwake,

Mathalani mimi namuwekea kila mtu limit kulingana na mazingira nnayofahamiana nae, i.e mfanyakazi mwenzangu mi na yy ni kazikazi, jirani ni jirani tu hakuna zaidi ya hapo, boss wangu kazini ni kazini tu, ndugu ni ndugu tu na hatakiwi kuinglia kazi zangu, walevi wenzangu ni pombe na eneo la kukutana ni bar tu nje ya hapo ni kuwe na sababu ya msingi sana..

Kuhusu simu hizi kiukweli zimetuondolea ustaarabu, na hua hatuwazii upande wa pili. Mtu akikupigia simu usipopokea anageuza kesi hajui ulikua unafanya nini, au mtu anashindwa kujiongeza kua kuanzia saa 4 usiku mtu amechoka na mihangaiko yake hivyo simu zisizo za msingi za usiku ni usumbufu!.
Hizi simu kwangu mimi binafsi hua naona mtu anipigie mara moja tuu, simu iite mpaka ikate, isipopokelewa nikiiona missedcall ntapiga, kama ni urgent sana basi missed call na angalau meseji moja inayoelezea emergency yenyewe kwa kina na kwa ufupi.
Safi
 
Back
Top Bottom