Lady Jay Dee lazima ukubali, huu ni wakati wa Zuchu

Lady Jay Dee lazima ukubali, huu ni wakati wa Zuchu

sijawahi kumsikiliza uyo zuchu
ila kumlinganisha na jide aisee ni masihara makubwa hata diamond mwenyewe atakua anacheka uko aliko
jide hajapitwa na wakati bado maana naamini mziki hauna umri kama bado una nguvu na sauti iko vizuri
whitney katoa on my own akiwa 40s uko na ukawa hit song
 
Kwanza niweke wazi kumpambanisha Zuchu na wasanii waliotangulia badala yake ni "UJINGA","UZWAZWA","KUTOKUJIELEWA","KUTOJUA MUZIKI","USHABIKI MAANDAZI" na "CHUKI ZA KIJINGA".
Kipindi Zuchu anarelease kazi zake siku sikia sehemu WCB Wasafi walitangaza kwamba amekuja kupambana na wasanii wengine, kingine watu wanatakiwa kujua kuwa kumpambanisha na wasanii waliopita hakumfanyi Zuchu awe mkubwa lakini pia hakuzimi ndoto yake ya kuwa msanii mkubwa. Wapo watu wanaotaka kutengeneza beef ili ionekane Zuchu na Wasafi hawafai, tokea siku ametangazwa mpaka leo mitandaoni zimejaa kejeli juu ya Zuchu.
Ni kweli label inamfanya awe maarufu nani anakataa?, WCB Wasafi imejaa managers ambao wanafahamu soko la music, promotion and so on hii imefanya wasanii chini ya label hiyo kufanikiwa kwa urahisi kulifikia soko la ndani na kimataifa, leo kila msanii anatamani awepo WCB Wasafi japo akiwa pembeni atajinasibu kuwa haipendi or hana interest na Wasafi. Je, ni kosa Zuchu kuwa pale?, licha ya mama yake Khadija Kopa kuwa na ukaribu na Wasafi lakini pia uwezo wake umedhihirika na kuwavutia Wasafi kufanya nae kazi.
Kwanini tusimuache aoneshe uwezo wake kama ilivyo kwa wenzake waliopita?, ukijiona haufurahii anachikifanya Zuchu jua automatically wewe sio "SHABIKI" yake. Sio watu wote watakubali mafanikio yako, Nandy ndio mmoja ya wasanii wakike kupongeza kazi za Zuchu wengine wamebakia ku-like kejeli kwa Zuchu huku wakijiita "LEGENDS". Kinachomtokea Zuchu ndio kilimkuta Rema kule kwao Nigeria baada ya ku-hit siku chache tangu alivyotoka mashabiki wa wasanii wakubwa walim-diss dogo kuwa anaiga style ya Wizkid, lakini Don Jazzy (manager wake) akawaambia mwacheni aimbe na kufurahi mtu unamiaka 30+ unam-diss dogo wa under 20 ili kumfanya ajisikie vibaya?, Harmonize wakati anatoka diss zikikuwa nyingi Mondi akawaambia mwacheni aimbe anavyojisikia. So tumwache Zuchu afanye kile anachopenda ukiona hakivutii kwako jiweke pembeni sio kumpambanisha na wasanii wengine whether wewe ni Wasafi fan/Team Wasafi or ni hater!
 
Huyo zuchu bado Sana kwa jide pia kumlinganisha hamumutendei haki Jide kakaa gemu miaka almost 20 years Sasa kumlinganisha na zuchu asiye na mwaka ni kumuonea hata Nandy, na Vanessa kuwalinganisha sio sawa maana hawajakaa kwenye mziki mda mrefu.

Milinganisho yako mleta mada haiko fair kabisa pia mnaanza kumtilia huyo Zuchu gundu na milinganyisho ya kipuuzi bure kila mtu ni unique kwa namna anavyoimba.
 
Maisha ya muziki ni kama fashion za nguo, ikipita imepita na huwezi lazimisha. Hivyo basi JD akubali ni kweli alikuwa msanii mkubwa kipindi chake na itabaki hivyo ila kwa sasa kuna wasanii wapya na kizazi kipya ambao wengine si ajabu hawajahi hata kusikia nyimbo zake au walisikia wakiwa wadogo ila hawakujua nani kaimba, na ndio maana akitoa kazi zake haziendi, ni kwa sababu wale walaji wa kazi zake walishamove on sasa hivi ni watu wazima wengine wamemrudia muumba wao angali siku za ujana wao wanaogopa maisha ya kesho, na kizazi kipya hawawezi kuvutiwa na kazi zake waache za watoto wazuri kama kina Zuchu, Mars nk nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiachana na ushabiki kiukweli zuchu ana sauti yees anayo ila choice of songs mi kiukweli bado hajanikuna 😎 hiyo Ni maoni yangu tu na kamabatapita kusoma hapa hii maoni yangu kiukweli zuchu usitungiwe nyimbo tena na lavalava wala mboso Mara mia tafuta mitindo ya kisasa katika beat upite kama anavyo pita Beyonce beat ngumu anailainisha na sauti ya wimbo dat will be nice.
Alafu sawa zuchu anaweza kuwa juu ila sio sawa na lay jay Dee
 
Mzee acha uongo eti ujauona Uzi wakati Uzi upo open kabisa.
bwana mdogo sijaona uzi wako, na nikiuona pia nitampongeza Diamond,
ila kwasababu umenijuza hapa natanguliza pongeze zangu za dhati kwa Diamond kwa kuingia kwenye Billbord ni hatua kubwa.

Una swali lingine? au hupendi nikimsifia Diamond wako 🤣 🤣 🤣
 
Kwa nini ameamua kujiita Puchu?
 
bwana mdogo sijaona uzi wako, na nikiuona pia nitampongeza Diamond,
ila kwasababu umenijuza hapa natanguliza pongeze zangu za dhati kwa Diamond kwa kuingia kwenye Billbord ni hatua kubwa.

Una swali lingine? au hupendi nikimsifia Diamond wako 🤣 🤣 🤣
Sio Diamond wangu kwa sababu me sifaidi as personal Bali Taifa ndio linafaidika.Diamond wa Tanzania kwasababu kupitia hayo Mafanikio yake yatachangia kukuza industry ya music Tanzania na kuanza industry ya mziki wa Tanzania kuangaliwa kwa jicho la tatu Kama tulivyoanza kupenya kwenye soko la Africa.Sijui umnamchukiaga nini mond cos kupitia yeye anatoa njia kwa watu wengine
 
Mnaua vipaji kwa vijana wanaochipukia kwa kuwapa sifa ambazo hawastahili.

Jide kwa sasa mziki anautamani lakini mshale sasa unaanza kuelekea mwisho

Huyo Zuchu bado sana, kumpa sifa nyingi ni kumpumbaza akili ili wengine waje kumpita.

Msaada mkubwa kwake ni kumpa support ya kazi zake na msaada ya fikra & miongozo ya kumjenga katika sanaa.
 
Diamond ana media, ana mashabiki wengi wanaomsapoti kuliko msanii yoyote kashinda Vita dhidi ya clouds kwasababu ya ukubwa wake sio kwa sababu ya mameneja wake

Usipende kudandia treni kwa mbele..
Vita ya clouds na Diamond ilianza lini.? Media zake binafsi alianzisha lini.??
 
Mkuu sio mimi niliomringanisha ni watanzania ndio wanasema uwezo wa Zuchu ni mkubwa kuliko hao waliomtangulia.
Na unaposema hawezi kupafom yeye kama yeye ni lini umemuona kasimama jukwaani akashindwa kupafom? Tuwasikilize watanzania sio wajinga.
Hao watanzania walifanyia wapi huo mkutano na kufikia hayo maamuzi?

Mwenyekiti wa huo mkutano alikuwa nani na nani alikuwa katibu atupe hizo miniti tuzione
 
Back
Top Bottom