Kwanza niweke wazi kumpambanisha Zuchu na wasanii waliotangulia badala yake ni "UJINGA","UZWAZWA","KUTOKUJIELEWA","KUTOJUA MUZIKI","USHABIKI MAANDAZI" na "CHUKI ZA KIJINGA".
Kipindi Zuchu anarelease kazi zake siku sikia sehemu WCB Wasafi walitangaza kwamba amekuja kupambana na wasanii wengine, kingine watu wanatakiwa kujua kuwa kumpambanisha na wasanii waliopita hakumfanyi Zuchu awe mkubwa lakini pia hakuzimi ndoto yake ya kuwa msanii mkubwa. Wapo watu wanaotaka kutengeneza beef ili ionekane Zuchu na Wasafi hawafai, tokea siku ametangazwa mpaka leo mitandaoni zimejaa kejeli juu ya Zuchu.
Ni kweli label inamfanya awe maarufu nani anakataa?, WCB Wasafi imejaa managers ambao wanafahamu soko la music, promotion and so on hii imefanya wasanii chini ya label hiyo kufanikiwa kwa urahisi kulifikia soko la ndani na kimataifa, leo kila msanii anatamani awepo WCB Wasafi japo akiwa pembeni atajinasibu kuwa haipendi or hana interest na Wasafi. Je, ni kosa Zuchu kuwa pale?, licha ya mama yake Khadija Kopa kuwa na ukaribu na Wasafi lakini pia uwezo wake umedhihirika na kuwavutia Wasafi kufanya nae kazi.
Kwanini tusimuache aoneshe uwezo wake kama ilivyo kwa wenzake waliopita?, ukijiona haufurahii anachikifanya Zuchu jua automatically wewe sio "SHABIKI" yake. Sio watu wote watakubali mafanikio yako, Nandy ndio mmoja ya wasanii wakike kupongeza kazi za Zuchu wengine wamebakia ku-like kejeli kwa Zuchu huku wakijiita "LEGENDS". Kinachomtokea Zuchu ndio kilimkuta Rema kule kwao Nigeria baada ya ku-hit siku chache tangu alivyotoka mashabiki wa wasanii wakubwa walim-diss dogo kuwa anaiga style ya Wizkid, lakini Don Jazzy (manager wake) akawaambia mwacheni aimbe na kufurahi mtu unamiaka 30+ unam-diss dogo wa under 20 ili kumfanya ajisikie vibaya?, Harmonize wakati anatoka diss zikikuwa nyingi Mondi akawaambia mwacheni aimbe anavyojisikia. So tumwache Zuchu afanye kile anachopenda ukiona hakivutii kwako jiweke pembeni sio kumpambanisha na wasanii wengine whether wewe ni Wasafi fan/Team Wasafi or ni hater!