LATRA: Mabasi 759 yanayofanya safari za Usiku yanazidisha Speed na kuchezea mfumo wa ufuatiliaji taarifa za gari (VTS)

LATRA: Mabasi 759 yanayofanya safari za Usiku yanazidisha Speed na kuchezea mfumo wa ufuatiliaji taarifa za gari (VTS)

Bahati nzuri unaongea na MTU ambaye nasafiri Kila wakati, najua ninachoongea! Labda kama unahitaji tu tubishane which I am not ready for that!
Dear, unaweza kusafiri hata kila siku lakini ukawa wrong kwenye analysis yako. Haya mambo yanakwenda kwa scientific facts zaidi na siyo hisia za mtu mmoja.
 
Sioni Logic ya kuendesha speed 80 usiku, LAZIMA tukubali kubadilika, at least wazungumzie speed 100 sio 80. Mabasi yote ya usiku ni mapya na ni mazima, usiku hakuna kelele nyingi, iweje tuendelee kushikilia Sheria za kipumbavu? Mwanzoni walisema usiku kutakua na ajali nyingine, MUNGU kawaumbua Sasa wanakuja na ujinga mwingine
Unataka usiku speed iwe 100km/hr mkuu, nadhani ufikirie kwanza hayo mawazo yako.
 
Unataka usiku speed iwe 100km/hr mkuu, nadhani ufikirie kwanza hayo mawazo yako.
Ndugu yangu, usiku wanatembea zaidi ya hio, niliwahi kuandika sana hapa jukwani nikaweka Hadi Screenshot, hawa jamaa ni wanafiki tu, Niliwahi kuweka hapa jukwani speed ya Frester tulikua tunatoka Kahama kuja Dar, ilikua 132kh/hr Tena asubuhi, niliwahi kuweka hapa ushahidi mwingine wa Superfeo ya Mwanza to Songea alikua anatembea 140km/hr Tena pale Makambako kwenda Njombe tukaitumia 25 minutes, niliwahi kuweka hapa ushahidi wa Nacharo ya Dar Tanga alikua 130km/hr
 
Dear, unaweza kusafiri hata kila siku lakini ukawa wrong kwenye analysis yako. Haya mambo yanakwenda kwa scientific facts zaidi na siyo hisia za mtu mmoja.
Ila speed 80 hakuna basi linatembea huo mwendo ni uongo Ndugu yangu, why tuseme uongo? Hawa wote ni wachakachuaji, I am not advocating for high speed ila nataka tuwe wakweli
 
Mwezi mmoja tangu Serikali iruhusu safari za mabasi kwa saa 24, tathimini ya mamlaka za usimamizi imeonyesha kuwepo ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za usalama barabarani, hali inayohatarisha usalama kwa abiria na mali zao.

Kutokana na ukiukwaji huo, ndani ya muda huo mabasi 759 yamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kwa kushirikiana na Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuzidisha mwendo na kuchezea mfumo wa VTS unaodhibiti na kutoa taarifa za kasi ya gari.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo na Kamanda wa Trafiki, Ramadhan Ng’anzi ilieleza kati ya mabasi hayo, 723 yalipewa onyo na mengine kusitishiwa leseni.

“Mabasi yaliyositishiwa leseni mpaka mamlaka itakapojiridhisha kwamba wamebadilika ni 36.

“Kati ya mabasi 246, asilimia 80 (mabasi 197) yamebainika yanaendeshwa kwa mwendo kasi kati ya kilomita 86 hadi 89 kwa saa, huku asilimia tisa yakiendeshwa kwa kilomita 90 hadi 103 kwa saa,” ilisema.
Findings za LATRA

View: https://twitter.com/BusesNation/status/1722646636441289050?t=xja2InY5iqqllPF15k2Vjw&s=19
 
Hao latra nao, mtu atembee usiku kucha na maximum speed ya 80km/hr... Hivo vingamuzi vimejaa upigaji mtupu tu hakuna kitu
Mpwa hakuna basi linatembea speed 80, uko sahihi kabisa! Hawa ni wapigaji tu na ni attention seekers. Wanataka waonekane wanafanya kitu
 
Kwa Sasa barabara nyembamba sio issue sana, Kwa uzoefu wangu
Mkuu ni kwa sababu kulikuwa na katazo. Trust me. Usiku kwanza kuna mi-lori mingi na ndiyo ilikuwa chanzo kikubwa cha ajali enzi hizo za zamani. Dreva wa basi analivaa lori lililoharibikia sehemu kwa nyuma huku yuko kwenye mwendo mkali.
 
Mkuu ni kwa sababu kulikuwa na katazo. Trust me. Usiku kwanza kuna mi-lori mingi na ndiyo ilikuwa chanzo kikubwa cha ajali enzi hizo za zamani. Dreva wa basi analivaa lori lililoharibikia sehemu kwa nyuma huku yuko kwenye mwendo mkali.
Mpwa ajali ni ajali tu, Kuna maboresho yanatakiwa kufanyika ila sio kuzuia speed to 80. Ngoja nikwambie kitu, week Moja iliyopita nilikua naenda Mpanda, tukiwa tunakaribia Inyonga saa Saba usiku, Dereva akaanza kusinzia na nusura tugongane uso Kwa uso na Lory kama sio Mimi na co-driver kumstua, my point is sio Kila ajali inasababishwa na lory kupaki njiani na NDIO maana nikasisitiza kuwa inabidi kuboresha tu huu usafiri
 
Hii ilikua ni Kahama, angalia hii speed
Screenshot_2023-11-10-12-30-47-693_com.solotech.apps.digital.gps.speedometer.odometer.jpg
 
Back
Top Bottom