25 January 2024
BARABARA YA SONGEA NJOMBE MAKAMBAKO KUJENGWA UPYA
View: https://m.youtube.com/watch?v=w_W-Mvw4QZY
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatarajia kuanza kujenga upya barabara ya Songea – Njombe - Makambako kwa kiwango cha lami kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba na muda wake kuisha.
Waziri Bashungwa amesema hayo Wilayani Ludewa, mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi wa Mlangali katika mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufungua mikoa na nchi jirani kwa barabara za lami
View: https://m.youtube.com/watch?v=qjae7T-g68Y
HABARI KWA KINA BARABARA YA SONGEA, NJOMBE HADI MAKAMBAKO
24 January 2024
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatarajia kuanza kujenga upya barabara ya Songea – Njombe - Makambako kwa kiwango cha lami kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba na muda wake kuisha.
Bashungwa amesema hayo Wilayani Ludewa, mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi wa Mlangali katika mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufungua mikoa na nchi jirani kwa barabara za lami.
Bashungwa amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu 2024 Serikali itakuwa imempata Mkandarasi atakayenga upya barabara hiyo ikiwa ni dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
“Ukitoka bandari ya Mtwara unakuja kwa lami hadi Songea, na kutoka Songea kuja Njombe mjini kwenda makambako, lami ilijengwa miaka ya 80 imechoka, tayari Mheshimiwa Rais ametupatia fedha na kufika mwezi wa tatu au wa nne 2024 tutakuwa tumepata mkandarasi anakuja kuijenga upya”, amesema Bashungwa.
Bashungwa amewataka wananchi kuendelea kuheshimu Sheria na kutofanya shughuli katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuondokana na usumbufu pale Serikali inapotumia Sheria zilizowekwa kuwaondoa katika maeneo ili kujenga miundombinu ya barabara.
Source : tovuti MOW