31 January 2024
BARABARA YA IRINGA MLIMA KITONGA HADI MOROGORO
Mlima Kitonga Ukipanuliwa Barabara ya Njia Nne, Vioo Maalum Kuwekwa | IringaView: https://m.youtube.com/watch?v=RDCGFd0WPBM
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Iringa imeanza kazi ya kuboresha barabara na kupanua mlima Kitonga ili kupata mwanya wa kujenga barabara ya njia nne kwa lengo la kupunguza kero za muda mrefu ikiwemo msongamano wa magari, kudhibiti ajali na kuufanya mlima kitonga upitike kirahisi zaidi.
Akizungumza mbele ya kamati ya siasa CCM mkoa wa Iringa ilipofika kujionea kazi inayoendelea katika barabara ya Mlima Kitonga Januari 31, 2024, Meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Mhandisi Yudas Msangi amesema ujenzi wa mradi huo utagharimu bilioni 6.4 mpaka kukamilika.
Mhandisi Yudas amesema baada ya mlima Kitonga kupanuliwa itajengwa barabara ya kiwango ya njia nne ambayo itakuwa na mifereji mikubwa ya kuongoza maji lakini pia itafungwa vioo maalum kwenye kona zake kwa ajili ya kuongeza uono na kusaidia upishano mzuri wa magari nyakati zote."
Katika mradi huu Shughuli ambazo tumepanga ni kuchoronga mwamba, baada ya hapo barabara itatengenezwa vizuri alafu tutaweka layer tofauti tofauti ambayo ya kwanza inaitwa G15 itakuwa na unene wa milimita 150, itafuata G45 itakuwa na unene wa milimita 150""baada ya hapo tutaweka zege lenye upana wa mita tano kutoka sehemu tuliyochonga, pia itajengwa mifereji kwajili ya kuongoza maji na kuweka vioo maalum" - Amesema Mhandisi Yudas Msangi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kiasi cha bilioni 6.4 ili kufanikisha ujenzi wa mradi huo.
Yassin amesema Pesa ya kupanua mlima Kitonga na kujenga barabara ya njia nne imetolewa na Rais Samia baada ya kusikia kilio cha wananchi huku akisema mradi huo haukuwamo kwenye mipango na ahadi za CCM lakini serikali imeamua kuutekeleza kutokana na kuwepo kwa ajali, kero na changamoto katika barabara mlima Kitonga
View: https://m.youtube.com/watch?v=mg38KQRvb8U