LATRA yatangaza bei mpya za mabasi, daladala

LATRA yatangaza bei mpya za mabasi, daladala

Tunataka nauli za ndani ya mkoa, kutuwekea za mkoa.....Dar haijatusaidia watz, utadhani kila tukiamka asubuhi watz wote tunaenda Dar na kurudi jioni.
 
Labda nchi za dunia ya tatu, kwa nchi nyingi usafiri wa umma ni kama bure sababu ya serikali zao wanawapa ruzuku.
Mwendokasi wana gharama nafuu labda sijui unapimaje.
Kutoka gerezani hadi kimara ni 650. Kapande daladala uone utatumia kiasi gani
Sio kweli, nchi gani hiyo?? Usafiri ni kama bure??
 
Hizi bei hata hawasimamii, hizi bei za awali watu walikuwa wanalipa zaidi ya hapo, dar to dom basi ilikuwa elfu 20 huko, 22 na hilo ndio basi la kawaida, wakati nauli halisi ilikuwa ni 16 hiv.. Sasa imepanda 18 tutegemee mtu kutozwa 25 elfu
Uko sahihi. Hata hizi Daladala, kuna sehemu Daladala tayari nauli zilikuwa juu kuliko hizi zonazotangazwa. Hivyo sasa nao wataongeza tena! Mfano nauli ya Moro - Mzumbe ya LATRA ilikuwa 750 wao walikuwa wanatoza 900 au 1000 na sasa ya LATRA ni 850. Ni kwa vyovyote vile itapanda sana. LATRA hapo wanaimba ngonjera tu labda wawe na magari yao ya usafirishaji.
 
Hii nchi tuna matatizo.

Kutokana na vita inayoendelea imesababisha mafuta kua adimu na imesababisha nauli kupanda.

Watu wanakuambia "Tunakukumbuka Magufuli" nina uhakika Magufuli asingeweza kumzuia Putin na uchizi aliouamua.

In fact Magufuli angehimiza kulipa hizi nauli haraka kwakua alishawahi kutuambia kama hatuna 200 tupige mbizi. Kama hutaki lipia choo baki na mavi nyumbani kwako.

Kama unadhani angekubembeleza tulia hapo hapo.

Mtu anaandika tunakukumbuka Magufuli akitoka hapo unamkuta uzi wa vita ya Urusi akisifia vita inavyoendelea.

Na ndugu zetu Latra hawana namna ya kucompensate zaidi ya kupandisha nauli za usafiri, na maajabu ni kwamba nauli walizotangaza watu tumekua tunalipa miaka 3 nyuma. Latra hua hawafanyi confirmation na kile chama cha kutetea abiria?

Au wote siyo field workers hua wanakaa tu ofisini kuperuzi fb na insta?
 
Pole sana mkuu. una uchungu kuzidi hata familia yake
Maombolezo au furaha? Mimi furaha bado haijaisha , na haitaisha milele. Maombolezo ni kwa sukuma gang na wanyonge.
 
Uku Geita Masumbwe bodaboda kwa safari moja wamepandisha kutoka 1000 kabla ya mafuta kupanda sasa hivi ni 2000 na asiyelipisha wanamfungia mnyororo na faini ya keti tatu za soda Serikali mngelitolea ufafanuzi na hili wananchi wanateseka kwa kutembea na miguu kilometa 10
Kwamba serikali iache kufanya mambo ya msingi ihangaike na bodaboda wa geita?

Nendeni hata ofisi za kata au serikali ya mtaa.
 
Kwenye huo mkeka naona semi luxury Dar to Arusha ni 36,700/=

Na sisi tulishazoea nauli ya 36K wao wanaita ni full luxury.. gari ina choo, tv zipo za kutosha, nyingine zina WiFi, kipupwe OG, coffee/ milk, maji & pipi

Hiyo imekaaje? Kwamba tutalipia nauli ya semi luxury au?

Cc QUIGLEY na Kaskazini ilivyo na gari nzuri [emoji1787] si tutalipishwa 40K aisee

Viwango vilivyopo na kwa ajili ya kuzuia usivuke bei tajwa. Unaweza weka bei pungufu au hata bure hakuna maamlaka inayokukutaza. Ili hutakiwi kuzidi bei elekezi
 
Hivi kwenye ndege ni shirika lipi la umma linapanga bei za ndege? kwa maana nauli ya kwenda dubai ni nafuu zaidi kuliko nauli ya kwenda Bukoba
Ndege inategema mambo mengi, mfano ukibook ticket ya kesho bei itakuwa kubwa kuliko atakayebook ya miezi 3 kabla,
 
Mkuu kwani nimekukosea nini kwa kutoa maoni yangu? Kuna watu wanamwona yule shetani kama shujaa wao nami nachukulia kuwa ni maoni yao. Siyo lazima tuwe na maoni sawa
Wewe katoto huna adabu, umetumwa uje kumtusi jpm shetani? Shetani ni ukoo wako mzima.
 
Ulisema 🙌
Kuanzia tar 10 BM, Arusha to dar via Chalinze ni 50K
Via bagamoyo 40

Yale ya kawaida 36K

QUIGLEY
 
Ongeza sh 100
Kama ulikua unalipa 300 basi itakua 400, kama ilikua 400 itakua 500, kamaa ilikua 500 itakua 600
Kuna route nauli imepanda kutoka 1000 hadi 1500.

Mbona pamepanda parefu tofauti na hiyo 100 unayoisema.
 
Back
Top Bottom