LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
DODOMA TO DAR ES SALAAM Tsh 5000/= KM 80

DODOMA TO BABATI Tsh 11,000/= KM 168
Labda kwa sababu Dodoma ni makao makuu kwa hiyo wameona wafanye 5000 Ili kujirahisishia maisha na posho watajiongezea pia hatutaki tuhamie Burundi 😄
 
Mafuta yameshuka kwa mujibu wa EWURA, huku nauli zinapanda tena keshokutwa.

Poleni Watanganyika, Rais wenu yupo bize kuzurura huko Dubai tu. Toka ameanza kuzurura amefanya lipi la maana?

Mwenzie Kikwete alizurura lakini kila jambo lilienda sawia ingawa kulikua na changamoto za hapa na pale.

Mama yenu amejaribu kumuiga Kikwete lakini wapi! The more anavyozurura the more wananchi wanavyozidi kuumia.

Haya mafuta wanasema yameshuka mbona nauli hazishuki? Huyu mtu andolewe tu 2025 aidha kwa kura za maoni huko kijani au kwa sanduku la kura tu maana uwepo wake tunazidi kupata hasara tu.
 
inabidi tumtoe hyo 2025 wakuu yaan ndani ya miaka 3 kapndsha nauli maradufu duuh
 
Serikali yetu pendwa inayojali wananchi na inayojitahidi katika kuwapunguzia raia wake ugumu wa maisha na inayopambana kupunguza gharama vitu na huduma mbali mbali za kijamii mwezi uliopita kupitia latra

hili tangaza ongezeko la nauli za mijini na mikoani nachukua nafasi hii kuwakumbusha kwamba kesho ndio hizo nauli mpya zina anza kutumika usijasahau kama ulikua unachukua mia tano

hili upande dala dala kuanzia kesho nauli ya jero haipo hili kuepuka aibu yakudhalilishwa na makondakta kuanzia kesho chukua mia sita ww uliozoea kulipa mia sita kuanzia kesho chukua mia nane mm nimewakumbusha tu

najua wengi mpo Bize nakujua kati ya simba au yanga nani atavuka hatua ya makundi pongezi kwa serikali yetu inayojali maisha ya watu wa hali ya chini pongezi kwa viongozi wetu wote wa serikali ambao wapo tayari wao walale njaa hili mradi raia wao washibe wapo radhi wao wakose umeme hili mradi raia wao wapate umeme wapo radhi wao wapange hili mradi raia wao wote wawe na nyumba yangu ni hayo
 
Hawa viongozi wa LATRA wamekurupuka na hili suala linagombanisha uongozi wa serikali na wananchi. Watoe sababu ya msingi ya kupandisha nauli.
 
Back
Top Bottom