Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Huyu nilijua tu atakuja kurudi, na hapo anataka apewe cheo
 
watarudi wote tu tatizo CDM hawasomi mambo ya nyakati.wanatakiwa kuwa fexible na siyo rigid.wakubali tu kubadilika.dunia inabadilika kwa kasi nao yawapasa kubadilika pia.
Kwani kuna mtu anashikikiwa at gunpoint huku Chadema?
 
Nyie nguruwe wa CCM si ndiyo mlisema kuwa huyu ni mhujumu uchumi kwa kuuza Twiga wetu? Au hukumbuki Kigwangwala alisema atamshitaki huyo Nyalandu kwa kuuza Twiga wetu? Huyu tunajua alikuja Chadema kuomba hifadhi ya kisiasa akikimbia ukatili wa Magufuli, sasa ameona ni salama kwake kurudi huko kwa vile mtesi wake hayupo tena duniani hatuna neno naye tunamtakia maisha mema. Swali jee azma yenu ya kumfungulia mashata ya uhujumu uchumi kwa kuuza Twiga wetu bado ipo? Tunawatakia mashataka mema.
Mkuu, jipange jinsi ya kuanza kumshambulia Nyarandu.

Bila shaka mtaendelea kumwita kamanda asie na njaa ya kumsujudia mtu
 
Upo slow sana, kama hadi sasa hujagundua Tanzania hamna uhusiana wowote kati ya vyama vya siasa na sera ingekuwa hivyo EL, Nyalandu na wenzao wasingekaribishwa CDM ama kudhubutu kurudi CCM.
Hao wote walikimbia udikiteeta uliokuwa umeshamili ndani ya chama
 
"Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amemlipua waziri wa zamani wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka na kumlalamikia kupoteza mabilioni ya fedha za Serikali.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018, Bungeni Jijini Dodoma, Dk Kigwangalla ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.

Dk Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Mbali na tuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.

Hata hivyo wakati Kigwangala akitoa tuhuma hizo tayari Nyalandu alishasema kuwa tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandao dhidi yake si za kweli bali zinalenga tu kumchafua.

Taarifa hiyo imekuja kipindi ambacho Lazaro Nyalandu amejiondoa CCM na kujiunga CHADEMA"
 
Nyalandu naona ameona kuna fursa anaweza ipata kwa kutokuwepo kwa Mwendazake
Si unajua yeye na Mama ndiyo viongozi pekee wa CCM waliokwenda kumjulia hali Tundu Lissu alivyopigwa risasi, they have something in common. Walichukizwa na kukerwa na ukatili wa mwendazake
 
Ndivyo ninavyosikiliza hapa nikiwa Live kutoka Dodoma.

===
Lazaro Nyalandu amerejea CCM akitokea CHADEMA. Amerejea Aprili 30 katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulifanyika Dodoma.

Nyalandu aliwahi kuwa mtia wa kugombea urais kupitia Uchaguzi Mkuu 2020 kupitia CHADEMA. Ambapo katika hotuba yake ameshukuru kwa kumpokea.

Kabla ya kurejea CHADEMA, Nyalandu alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati

Amesema katika nchi ya Ugenini wimbo hauimbiki.
Hawa ndio wale malaya Mwalimu Nyerere aliwaona kabla hajafa.
Jamaa ukirudia maneno aliyo yaongea akijiunga na Chadema na maneno ya leo utagundua kweli huyu ni malaya maana hakumbuki aliongea nini!!
 
Upinzani utakuwa na maana pale tutapata katiba mpya, reform ya sheria zinazohusiana na siasa na chaguzi, watu kuwa na vipato binafsi huru na upinzani utakapoacha kuchukua makapi.
 
Upinzani utakuwa na maana pale tutapata katiba mpya, reform ya sheria zinazohusiana na siasa na chaguzi, watu kuwa na vipato binafsi huru na upinzani utakapoacha kuchukua makapi.
Mmeshindwa kuwa na taasisi Imara halafu unadhani katiba ndiyo ije iimarishe Chama chenu?

Katiba haina uhusiano na M/kiti Chama chako, haina uhusiano kabisa na maswala yenu ya ndani ya Chama, katiba inahusu mambo ya nchi kisheria, Pambane na Chama chenu
 
Upinzani utakuwa na maana pale tutapata katiba mpya, reform ya sheria zinazohusiana na siasa na chaguzi, watu kuwa na vipato binafsi huru na upinzani utakapoacha kuchukua makapi.
Mkuu, Nyarandu kuhamia na kupewa vyeo chadema hakuhusiani na ubovu wa katiba yetu.

Ni ulafi na umbumbumbu tu wa vyama vya upinzani
 
Back
Top Bottom