Lazaro Nyalandu ataongea na Watanzania kesho kuelezea udhaifu wa Upinzani kupitia kipindi cha Clouds 360

Siasa za bongo zina utofauti mkubwa sana na nchi nyingine.
 
Hakuna haja yeye,ajae kimya tu
 
Kwa nini hayo madhaifu asingewaambia hao CHADEMA kabla ya kutoka huko ili kuwapa mbinu za kuwakabili wapinzani wao, mpaka asubir abadili Chama zen ayaanike hadharani?? Yatasaidia nini?

Asituchoshe!
Mwamba haambiliki
 
Huyu naye! Kama anadai upinzani ni dhaifu si aanzishe chama chake ambacho kitakuwa imara badala ya kulamba matapishi yake kama alivyofanya kwa kurudl kwenye chama alichohama na kukishif??!!
 
Ataongea nini ambacho watangulizi wake hawajaongea?
 
Asisahau kutukumbusha na habari ya kwamba Wamarekani wamemtuma kugombea Urahisi Tanzania
 
Lazaro Nyalandu aliyerudi CCM kama kawaida yao, kesho asubuhi atakua Clouds, hata hivyo hajaweka wazi agenda anayokwenda nayo huko.

Unahisi ataongea nini? Na ungependa kumshauri nini?

 
Kabla hajatuambia madhaifu ya chadema atuambie ya mwendazake alomfurusha akakimbilia chadema.

Tunajua kwenda kwake chadema ilikuwa ni mkakati ulotengenezwa ili mwendazake apite bila kupingwa

Katumwa mapema ili kuwahadaa chadema kuwa hakubaliani na mwendazake. Wakiamini kuwa angeaminiwa apewe nafasi ya mgombea urais ili katika mazingira tata angejitoa kama Membe.

Bahati mbaya wakateleza script kwenye mtego alowekewa Sumaye akajitoa kabla ya wakati.

Alomtuma kaondoka, uchaguzi umeisha hana tena cha kufanya huko CHADEMA anabakije huko!?

Somo
Chadema wajue hakuna mwana CCM anaeweza kuja upinzani kwa mapenzi. Kuwaamini sana hao mamluki kutaendelea kuwakwamisha sana.

Fikiria tu uwepo wa hao wadudu kwenye vikao vya chama siri ngapi za chama zimeenda ccm kama maji.

Nawaambia tena hakuna mwanaccm kindaki anaeweza kuhamia upinzani. Ispokuwa katumwa kwa kazi maalum.

Tengenezeni wanachama wapya kwa watu wapya wasio na damu ya kijani.
 
Amkimbie jiwe kwa kwenda chadema? Kwani ni nje ya nchi? Kwa uchafu aliokuwa nao huyu jamaa, kwenda upinzani ilikuwa ni ticket ya Dpp kupewa maagizo. Lakini hakuguswa wala hata traffic kumsumbua bus lake kipindi anagombea. Huyu alitegeshwa awe 'lowasa', sema cdm walikuwa na hesabu nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…