Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Tatizo la Chadema ni uongozi,tatizo la CCM ni nini? hadi ukakimbia uko na kuacha ubunge?
MaCCM yameamua kumdaharirisha tu, hiyo ni Ng’ombe yao wameikata mkia tayari.
Kila anaerudi ccm , anaandaliwa media press na nilazima aimbe Mbowe.. Mbowe..! Ndio wampe cheo..😂😂
 
Huyu Nyalandu alimkimbia jiwe! lililotaka kumsaga saga kwa kushiriki ujambazi wa mali asili zetu! CDM walikukaribisha kukuepusha na mkono wa jiwe ili akikufuata useme ni SIASA. Unatakiwa uwashukuru
Kama alikuwa jambazi wa maliasili zetu, kwanini Chadema walimpokea?
 
Kama wapinzani watakuwa kila ukikaribia uchaguzi wanapokea makapi-kapi ya chama tawala, basi safari ndefu ya demokrasia itafuata. Nadhani sio kosa kuwapokea bali utafiti wa kumchangua mtu uwe wa kina, na wala asipewe majukumu ndani ya uongozi hadi miaka 5 - 10 imalize.

Akifikisha miaka 10 na bado hajarudi ndio tunaweza kuanza kumuamini kama ana nia kweli ya kujiunga na upande mwengine. Unajua ni vigumu mtu kubadili chama, maana sera za hivi vyama ziko tofauti. Mtu anaweza vipi leo yuko CCM/kada - kesho CDM tena kiongozi wa juu!

Vyama vya upinzani lazima mtafakari vizuri, hii imekalia kama vile mna pupa kidogo katika kufikia malengo.
 
Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending individual reasoning because of fear 'Unyumbu ama kujitoa ufahamu'
 
“Kuna mitihani ilitokea kwenye uchaguzi, kulikuwa na chaguzi za aina mbili, moja ilikuwa kupigiwa kura kwenye kamati, tunaenda kwenye Baraza Kuu. Kwenye Kamati Kuu Nyalandu alipata 100%, nilimgaragaza kweli kweli, kilichotokea viongozi wakasema Nyalandu asije akawa kama Lowassa”

Kwa kweli hapo Chadema waliona mbali sana kwamba tusimpe Nyalandu Madaraka kwani atakuwa kama Lowassa. Kwani sasa walisema uongo?
 

Nyalandu anatakiwa akapimwe akili kwanini,kwasababu, Mara anakimbia ubunge,mara anataka tena uRais,mara anataka tena ubunge alio ukimbia. Mara anakimbia CCM anakimbilia Chadema,mara anakimbia chadema anakimbilia CCM.

 
Ukweli ni kwamba MwanaCCM hawezi maisha ya upinzani. Narudia tena hawezi! Wao wamezoea kuwekewa mezani kila aina ya cheo na anasa. Wamezoea kupiganiwa na vyombo vya dola, na NEC. Aliyeonja pepo ya CCM hawezi maisha nje ya pepo ya CCM. Narudia tena, hawezi hata kidogo.
 
Mlio jirani na Nyalandu mniulizie, ni kwa nini anaonekana hajiamini kwa kile anachokisema? kwani kalazimishwa kutembelea vituo vya radio na kusema hayo ayasemayo?

Kwani akikaa kimya tu anapungukiwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…