LBL: Pyramid Scheme Inayowatapeli Watu kwa Kisingizio cha Uwekezaji

Status
Not open for further replies.
Kuna jamaa yangu kanipigia jana ananiambia hii furusa, nikamwambia sawa apambane ikija furusa lazima ujaribu either upate or ujifunze. Nilimjibu hivyo baada ya kuniambia kaamua kujilipua kwa kuwekeza Fedha kiasi kama mil 13(kashawekeza). Sikutaka kumwambia ukweli maana kashaweka pesa ndio ananishauri na mm nijiunge. Nimeishia tu kumsikitikia rohoni.

Baada yakuongea akaona anitumie na video kutoka ITV, inayozungumzia hio furusa.
View attachment 3225774
Fursa gani hiyo
 
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la makampuni yanayodai kutoa fursa za uwekezaji wa mtandaoni, lakini kwa uhalisia ni matapeli wa hali ya juu. Moja ya makampuni haya ni, ambalo limekuwa likiwahadaa watu kwa mfumo wa Pyramid Scheme — utapeli wa kifedha unaojificha chini ya kivuli cha uwekezaji.

LBL ni Pyramid Scheme, Si Uwekezaji wa Kweli
LBL linadanganya watu kuwa wanaweza kupata faida kubwa kwa kuwekeza kiasi kidogo cha pesa na kuwashawishi wengine kujiunga. Mfumo wake unategemea kusajili watu wapya ambao hulipa pesa zao kwa wale waliowatangulia badala ya kufanya biashara halali. Hii ni tabia ya kawaida ya Pyramid Scheme, ambapo faida inapatikana tu endapo watu wapya wataendelea kuingia kwenye mfumo.

Mbinu wanazotumia Kutapeli watu
  1. Ahadi za Faida Kubwa kwa Muda Mfupi — Wanadanganya kuwa unaweza kuongeza pesa zako kwa haraka bila juhudi yoyote.
  2. Motisha kwa Kusajili Watu Wengine — Ili upate “faida,” unalazimika kuwaleta watu wengine, jambo linalothibitisha kuwa si biashara halali.
  3. Matumizi ya Ushuhuda wa Uongo — Wanatumia video na picha za watu wakidai kuwa wamepata mafanikio, ilhali ni sehemu ya mbinu za kushawishi watu zaidi.
  4. Hakuna Bidhaa Halisi Inayouzwa — Biashara yoyote halali lazima iwe na bidhaa au huduma inayoeleweka. LBL haifanyi hivyo, inaendeshwa kwa mfumo wa mlolongo wa udanganyifu.
Kwa nini LBL ni Hatari?
  • Mfumo wake hudumu kwa muda mfupi kabla ya kuanguka na watu kupoteza pesa zao.
  • Walioko juu tu ndio hunufaika, lakini wanachama wapya huishia kulia baada ya kuliwa pesa zao.
  • Serikali nyingi zimekuwa zikifungia makampuni ya aina hii kwa sababu ni kosa la jinai kuendesha Pyramid Scheme.
USIJINGE! CHUKUA HATUA MAPEMA
Ikiwa umeshawahi kushawishiwa kujiunga na LBL, usiweke pesa zako hata kidogo. Ikiwa tayari umeshaingia, tafuta namna ya kutoka mapema kabla hujapoteza zaidi. Onyo watu wengine kuhusu utapeli huu ili tusiruhusu matapeli kuendelea kueneza hadaa zao.

View attachment 3225058
Everything comes and go,hata maisha yenyewe yanapita,kila mtu abakie alipo.
Wastaafu wanatapeliwa mafao malori yanaanguka mchana kweupe,hata pale kawe mnasema mengi,lakini kila kitu ni scamm hata siasa ni scam hata dollar pia ni scamm hata vita zote za kisiasa na uchumi ni scamm.
 
Halafu hata sio watu wapya wanaotapeliwa, wale wale waliotapeliwa kwenye kampuni ya kalyinda ndo hawa wamejazana kwenye LBL,

Walio wengi ni wale walokole wanaoishi kwa kuombewa na manabii na mitume wao, Kuna watu nchi hii wanaamini wanaweza kufanikiwa bila kutumia akili bali kulia makanisani na kutapeliwa sadaka na hao manabii

Watu waliozoea kutapeliwa sadaka, wanaowatapeli wananunua magari na kuishi kifahari lakini watapeliwa kutwa wanaombewa ili wapate magari na mali. Hao watu ukiwaeleza kuwa LBL ni utapeli wanakuona wewe hamnazo, Kiukweli Tanzania ina wajinga wengi sana

Niko nafanya mpango wa kutengeneza application/Mfumo kama wa LBL najua nitawapata tu watanzania wajinga niwapige pesa.

NB: Kuwa tajiri huitaji kuwa na huruma na mtu unaemwibia
Halafu wakristo huona ni weng wenye kutapeliwa kuna uhusiano gani na hii dini
 
Kuna jamaa yangu kanipigia jana ananiambia hii furusa, nikamwambia sawa apambane ikija furusa lazima ujaribu either upate or ujifunze. Nilimjibu hivyo baada ya kuniambia kaamua kujilipua kwa kuwekeza Fedha kiasi kama mil 13(kashawekeza). Sikutaka kumwambia ukweli maana kashaweka pesa ndio ananishauri na mm nijiunge. Nimeishia tu kumsikitikia rohoni.

Baada yakuongea akaona anitumie na video kutoka ITV, inayozungumzia hio furusa.
View attachment 3225774
daah Noma sana
 
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la makampuni yanayodai kutoa fursa za uwekezaji wa mtandaoni, lakini kwa uhalisia ni matapeli wa hali ya juu. Moja ya makampuni haya ni, ambalo limekuwa likiwahadaa watu kwa mfumo wa Pyramid Scheme — utapeli wa kifedha unaojificha chini ya kivuli cha uwekezaji.

LBL ni Pyramid Scheme, Si Uwekezaji wa Kweli
LBL linadanganya watu kuwa wanaweza kupata faida kubwa kwa kuwekeza kiasi kidogo cha pesa na kuwashawishi wengine kujiunga. Mfumo wake unategemea kusajili watu wapya ambao hulipa pesa zao kwa wale waliowatangulia badala ya kufanya biashara halali. Hii ni tabia ya kawaida ya Pyramid Scheme, ambapo faida inapatikana tu endapo watu wapya wataendelea kuingia kwenye mfumo.

Mbinu wanazotumia Kutapeli watu
  1. Ahadi za Faida Kubwa kwa Muda Mfupi — Wanadanganya kuwa unaweza kuongeza pesa zako kwa haraka bila juhudi yoyote.
  2. Motisha kwa Kusajili Watu Wengine — Ili upate “faida,” unalazimika kuwaleta watu wengine, jambo linalothibitisha kuwa si biashara halali.
  3. Matumizi ya Ushuhuda wa Uongo — Wanatumia video na picha za watu wakidai kuwa wamepata mafanikio, ilhali ni sehemu ya mbinu za kushawishi watu zaidi.
  4. Hakuna Bidhaa Halisi Inayouzwa — Biashara yoyote halali lazima iwe na bidhaa au huduma inayoeleweka. LBL haifanyi hivyo, inaendeshwa kwa mfumo wa mlolongo wa udanganyifu.
Kwa nini LBL ni Hatari?
  • Mfumo wake hudumu kwa muda mfupi kabla ya kuanguka na watu kupoteza pesa zao.
  • Walioko juu tu ndio hunufaika, lakini wanachama wapya huishia kulia baada ya kuliwa pesa zao.
  • Serikali nyingi zimekuwa zikifungia makampuni ya aina hii kwa sababu ni kosa la jinai kuendesha Pyramid Scheme.
USIJINGE! CHUKUA HATUA MAPEMA
Ikiwa umeshawahi kushawishiwa kujiunga na LBL, usiweke pesa zako hata kidogo. Ikiwa tayari umeshaingia, tafuta namna ya kutoka mapema kabla hujapoteza zaidi. Onyo watu wengine kuhusu utapeli huu ili tusiruhusu matapeli kuendelea kueneza hadaa zao.

View attachment 3225058
Kweli mkuu,lkn yanaingiaje nchini haya makampuni,inakuwaje yanasajiriwa?, maana hawa hawana tofauti na wale almaarufu DESI,waliwaliza wengi enzi hizo,na mengine mengi tu .
 
Hawa jamaa wajanja sana. Sio matapeli. Wanakwambia wanakupa faida 2% kwa siku alafu Hela yako wanaenda izalisha kwa at least 10%-15%. Wakiwa na hiyo mitaji yenu yote mliowakusanyia, kutengeneza 10% kwa siku sio issue. Sio wapigaji
 
Mbinu wanazotumia Kutapeli watu
  1. Ahadi za Faida Kubwa kwa Muda Mfupi — Wanadanganya kuwa unaweza kuongeza pesa zako kwa haraka bila juhudi yoyote.
  2. Motisha kwa Kusajili Watu Wengine — Ili upate “faida,” unalazimika kuwaleta watu wengine, jambo linalothibitisha kuwa si biashara halali.
  3. Matumizi ya Ushuhuda wa Uongo — Wanatumia video na picha za watu wakidai kuwa wamepata mafanikio, ilhali ni sehemu ya mbinu za kushawishi watu zaidi.
  4. Hakuna Bidhaa Halisi Inayouzwa — Biashara yoyote halali lazima iwe na bidhaa au huduma inayoeleweka. LBL haifanyi hivyo, inaendeshwa kwa mfumo wa mlolongo wa udanganyifu.
Kwa nini LBL ni Hatari?
Kuna mapadre na makasisi humo wanapiga promo kwa waumini balaa, mwanzo nilidhani ni project ya RC
 
Kweli mkuu,lkn yanaingiaje nchini haya makampuni,inakuwaje yanasajiriwa?, maana hawa hawana tofauti na wale almaarufu DESI,waliwaliza wengi enzi hizo,na mengine mengi tu .
Hiii kitu ni views za trailer na wala sio kitu cha Bure,mnasema you tube inatoa commission, sasa Hawa wamefanya small akaunti za views na wanakupa commission ukikamirisha,sio kitu cha Bure ni sub task.
 
Sijakuelewa mkuu
 
Wajanja wanaowahi wanakula pesa. Ukitaka kufanikiwa usiogope kupoteza. Kipi Bora, kubeti au hii pyramid? Muhimu kufanya uchaguzi juu ya uhalali wa hii fursa na kufanya maamuzi sahihi, badala kukurupuka na kusema huu ni utapeli!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom