Your Argument is very wrong..
Kwahiyo wewe msimamo wako uko wapi?? Kwamba watu wasiende kwenye party za Diamond na Zari ila waenda kwa Madam Rita na party za kina Wema na Wolper?? Una uhakika gani Madam Rita hapewi support na Watanzania?? Unafikiri kile kipindi BSS kinajiendeshaje?? Kusingekuwa na viewers unadhani kingepata wadhamini?? Hao viewers ni Waganda?? Au wewe unataka support ya aina gani labda?? Tutembeze bakuli kumchangia Madam?? Si ana wadhamini ambao wanatangaza bidhaa na huduma zao kwenye kipindi na sisi kama watazamaji ndio tunampa nguvu..
Tukirudi hapo kwa Wema na Wolper, jijengee heshima, fanya kazi kwa bidii na kuwa mbunifu kila kitu kitaenda kama unavyotaka.. wachana na party, hata mazishi yetu yanatofautiana sana, kuna watu wanazikwa na maelfu na wengine mamia na wengine makumi.. Inategemea ulifanya nini wakati ukiwa hai. Huwezi kuwa na ugomvi na bifu na kila mtu hapa mjini ukapata support pindi unapoihitaji wachilia mbali tabia mbovu za hao watu..
Wewe una wivu tu, alafu jaribu kuwaomba radhi Watanzania uliowatukana hapa, hata usipofanya hivyo haiondoi dhana kwamba una wivu wa maendeleo..
Mwisho na Richard hawajapata support ya Watanzania?? walipokuwa kule mjengoni walijipigia wao kura?? walijipigia kampeni?? Tena wakati wao wakiwa kule zilikuwa zile kura za SMS tu, 1 vote 600/= na watu walipiga kama vichaa, ulitaka wafanyiwe nini kingine?? Both of them returned home with cash, i mean big cash lakini walizitumiaje?? Mwisho akahama Moro akaenda rent a big house at Mikocheni akaendekeza anasa mpaka pesa ikaisha, unafikiri mtu mwenye akili atataka kufanya kazi na mtu wa namna hiyo?? Same story to Richard.. Abby alikuja Tz as an underdog i mean with nothing at her account, amefanya kazi kwa bidii sasa ana maisha na coverage kuliko hao waliopata pesa akina Richard, alafu ulifikiri ni Tz tu huyu demu anakubalika, mpaka Naija anafika na anapiga mikwanja huko.. Yaani wewe uzembe wa wapuuzi wengine unatuhusisha Watanzania wote?? wacha hiyo tabia kabisa, after all huyo Mwisho si alipewa kipindi Channel 1?? Kafika nacho wapi mpaka sasa??