Watoto wakike wapo kwenye hatari maeneo mengi Sana ya mapito yao ya maisha, siyo chuo tu, nimeshuhudia maeneo mengi sana kuanzia safari yao ya masomo ya primary Hadi kupata ajira kote ni hatari tupu na hii inatokana na mifumo mibaya ya elimu ktk nchi yetu,
Anapokuwa shule ya msingi na secondary wengi hurubuniwa na waalimu wenyewe na hata wauza chips na zaidi Sana Bodaboda kwa wale wanao soma Day haswa shule za kata zilizo vijijini,
Kwa wanafunzi wa vyuo vyoootee kuanzia certificate had masters hao ni chakula ya ma lacturers, ili apate GPA nzuri lazima aliwe, na katika hili mm nailaumu sana serikali kwa kuwaachia hao lacturers kutunga mitihani na kuisahisha wenyewe, viongozi wetu wengi ni wanawake sijui hawalioni hilo?
Wanapo enda Field huko nako wanakutana na changamoto za wakuu wa idara ama kazi, ili wapate ripoti nzuri lazima agawe papuchi kwa mkuu wa idara na pengine hata wasaidizi wao,na wengi hudanganywa kuwa baada ya field watapatiwa ajira eneo husika.
Wanapo enda Sasa kutafuta ajira huko ndiko balaa kabisa maana kama hugawi uchi basi ajira utaisikia kwa wenzako, namfahamu jamaa mmoja yeye ni manager wa kituo fulani kikubwa cha mafuta ambacho pia kinahusika na masuala ya Hotel's, yeye kila wiki anatoka na demu mpya kwa kuwadanganya atawapa kazi,wengi wanao enda omba ajira pale huacha no zao za cm na baadae jamaa anawatafuta private na kuwarubuni,
Kwahiyo kwa ujumla watoto wakike wapo ktk wakati mgumu kwa 80% ya maisha yao.