Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Enzi ya Mwinyi akiwa na Omar Mahita ndio tulishuudia majambazi yakilelewa na Kuibuka majambazi Makubwa akina Alex Massawe e.t.c
Kweli wengi wanaochangia huu uzi ni watoto wa miaka ya 90 nawashauri bora mgekuwa wasomaji mgejifunza mengi.

IGP wakati wakati wa Mwinyi alikuwa Harun Mahundi.

Sasa Mwinyi na Alex Masawe wapi na wapi.
 
Hayo maswali kawaulize wadini wenzako
Udini ulete wewe tu hapa ni elimu bila malipo,Nyerere kaongoza kuanzia miaka ya 60,vita ya Kagera miaka ya 78 miaka takriban 6 mbeleni ndioMwinyi kaingia madarakani sasa aliikuta nchi imeyumba na vita ipi ya Vietnam au wapi?

Sio kila mada ya kuchangia ndio maana wengine tunasoma tu na kutoa like hii ilimu tunawaachia akina Ritz.
 
Kweli wengi wanaochangia huu uzi ni watoto wa miaka ya 90 nawashauri bora mgekuwa wasomaji mgejifunza mengi.

IGP wakati wakati wa Mwinyi alikuwa Harun Mahundi.

Sasa Mwinyi na Alex Masawe wapi na wapi.
Watu wavivu wakusoma na kufikiri, wanapenda kuamini stori za vijiweni. Pia wengine wanasukumwa na ushabiki usio na tija. Kwa mtu makini ni rahisi kujua kwamba Mzee Mwinyi alichukua nchi ikiwa taabani.
 
Hata mkikesha mnajaribu kumchambua nyerere bado hamtaweza kumuharibia yale mazuri aliyo yafanyia watanzania na bado hatujapata kiongozi mwenye uthubutu wa kutenda kama nyerere
 
kuweka udini kwa kigezo cha matukio machache ni kupotosha uhalisia wa mada yote. Udhaifu wa kila kiongozi unadhihirika pale utawala wake unapofika hatamu. Nyerere alichukuliwa kama mungu mtu lakini hii ilikuwa hivyo maana hakukuwa na mwingine wa kumlinganisha nae na haimaanishi hana mazuri yake ila kuja kwa Mwinyi kukafanya mapungufu ya Nyerere kubainika.

Alipokuja Mkapa na mfumo wake kulimfanya Mwinyi aonekane muharibufu pasi kutambua kuwa uwezekano wa maboresho kwa Mkapa ulitokana na uasisi wa Mwinyi.

Kikwete alikuja na muonekano wa kuwa mkombozi na kuna ambayo ameyafanya kupelekea Mkapa kuonekana alikuwa bepari na muuza viwanda pasi kutambua pia ni kupitia kwa aliyofanya Mkapa, Kikwete akaweza kusogea mbele.

Amekuja Magufuli leo hii, mapungufu ya Kikwete yanaonekana ila kuna swali moja tu la kuuliza je kama Magufuli asingepewa nafasi ya kuwa waziri katika awamu zilizopita tungemjua leo?
Point yangu ni moja tu, kuwa kila kiongozi alielipita ni muasisi wa muendelezo wa anaefuata. Leo hii tusingekuwa tunajadili mema ya Mwinyi kama Nyerere angeng'ang'ania madaraka.
 
Hata mkikesha mnajaribu kumchambua nyerere bado hamtaweza kumuharibia yale mazuri aliyo yafanyia watanzania na bado hatujapata kiongozi mwenye uthubutu wa kutenda kama nyerere
Nani anamuharibia sisi au Tundu Lissu maana haya mi nimeyatoa kwa Mwanasheria mkuu wa Chadema.
 
Wengi wao ni watu wa Tanga

Now naelewa why Tanga iliachwa nyuma kimaendeleo

what about YASIN MEMBA?
Kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, kuna watu walioona kuwa hawaridhishwi na Serikali ya Mwalimu Nyerere, hasa vijana kiasi cha kujasiria hata kuteka ndege ya abiria kwa lengo la kuishinikiza Serikali kufuata matakwa yao. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Boeing 737, ilitekwa mjini Mwanza na vijana watano wa Dar es Salaam.

Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba.

Kama utakuwa na muda takupa dondoo kiduchu.
 
T.R.A alianzisha mkapa?..muwe munafuatilia mambo,
 
Mzee Mwinyi alikuwa akimsikiliza Nyerere wala habishani naye wala hagombani naye lakini inapokuja kwenye kufanya maamuzi anafanya maamuzi kwa jinsi yeye anavyoona inafaa!
rejea usemi wake,mwendawazimu akichukua nguo wakati unaoga,ukatoka kumkimbiza utaonekana wewe ndio mwendawazimu,mtu kakalia kiti robo karne,huduma muhimu hakuna,wewe unawezesha hlo,unaambulia kusutwa na kuzodolewa
 
Gulwa.

Nyumba ya Mzee Mwinyi mbona ya kawaida kabisa wafanyakazi wengi tu wa serikalini wana nyumba nzuri kuzidi hiyo.
Nazungumzia nyumba inayojengwa masaki nyuma sea cliff bado haijaisha, ile unayosema wewe kajenga mwenyewe kwa pesa yake
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
Kuwa Mhalisia Bandugu, hata kama umpendi. Ni wakati ambao wananchi wa kawaida waliweza kuwa na pesa za matumizi na maendeleo. Hali ikawa mbaya alipokuja Mzee wa Masasi. JK(Kijana wa Msoga) akaja akarekebisha hali, watu wakapata maendeleo. Sijui huyu wa leo atatufikisha wapi. Kila kitu kwake NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
 
Nchi ilikuwa na haki mbaya hili jamani acha!Vijijini watu walikua wanavaa magunia na mifuko ya simenti,,,kunguni na chawa vilikua sehemu ya mwili wa mwanadamu,,,Mwinyi aliistaarabisha nchi hii sema watu wamesahau tu
Unakuta watu wamekaa kama wanasukana, eti anamtoa mwenzake chawa kichwani..! Na lilikuwa ni jambo ambalo halishangazi"!
 
Tuliweza kupata video..ambazo kabla lazima uwe na kibali maalum
Tuliweza kununua magari...kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa wengi
Kwa ujumla bidhaa zilianza kupatikana ...sinta sahau Stella Artois
 
Na ukizingatia serekali ndo ilikuwa inafanya biashara kuanzia uzalishaji usambazaji hata uuzaji rejareja, kodi alilipa mtumishi wa serekali tu. Nyuma kdg kila raia alitakiwa kulipa kodi ya maendeleo (ya kichwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…