Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Enzi ya Mwinyi akiwa na Omar Mahita ndio tulishuudia majambazi yakilelewa na Kuibuka majambazi Makubwa akina Alex Massawe e.t.c
Kweli wengi wanaochangia huu uzi ni watoto wa miaka ya 90 nawashauri bora mgekuwa wasomaji mgejifunza mengi.

IGP wakati wakati wa Mwinyi alikuwa Harun Mahundi.

Sasa Mwinyi na Alex Masawe wapi na wapi.
 
Hayo maswali kawaulize wadini wenzako
Udini ulete wewe tu hapa ni elimu bila malipo,Nyerere kaongoza kuanzia miaka ya 60,vita ya Kagera miaka ya 78 miaka takriban 6 mbeleni ndioMwinyi kaingia madarakani sasa aliikuta nchi imeyumba na vita ipi ya Vietnam au wapi?

Sio kila mada ya kuchangia ndio maana wengine tunasoma tu na kutoa like hii ilimu tunawaachia akina Ritz.
 
Kweli wengi wanaochangia huu uzi ni watoto wa miaka ya 90 nawashauri bora mgekuwa wasomaji mgejifunza mengi.

IGP wakati wakati wa Mwinyi alikuwa Harun Mahundi.

Sasa Mwinyi na Alex Masawe wapi na wapi.
Watu wavivu wakusoma na kufikiri, wanapenda kuamini stori za vijiweni. Pia wengine wanasukumwa na ushabiki usio na tija. Kwa mtu makini ni rahisi kujua kwamba Mzee Mwinyi alichukua nchi ikiwa taabani.
 
Udini ulete wewe tu hapa ni elimu bila malipo,Nyerere kaongoza kuanzia miaka ya 60,vita ya Kagera miaka ya 78 miaka takriban 6 mbeleni ndioMwinyi kaingia madarakani sasa aliikuta nchi imeyumba na vita ipi ya Vietnam au wapi?

Sio kila mada ya kuchangia ndio maana wengine tunasoma tu na kutoa like hii ilimu tunawaachia akina Ritz.
Hata mkikesha mnajaribu kumchambua nyerere bado hamtaweza kumuharibia yale mazuri aliyo yafanyia watanzania na bado hatujapata kiongozi mwenye uthubutu wa kutenda kama nyerere
 
Luksa maana yake "holela". Kama ndicho hicho unamaanisha tuko wote. Lakini pia kwa nyongeza, wakati wa Mwinyi ndipo:-

1. Vita ya maguruwe ikiongozwa na ustaadhi Rashid sijui nani iliibuka na kuzimwa na ushupavu wa Augustin Mrema.

2. Nicho kipindi shule za Kikristo zilichomwa moto na kupoteza uhai wa watoto wengi wasiokuwa na hatia.

3. Hapo hapo ndipo tuliona urasmishaji wa makundi ya balukta, wenye surualil fupi.

4. Wakati ule ndipo makundi ya mujahidina yalifahamika rasmi.

5. Waraka wa Kigoma Malima ulioasisi ukakasi kwa elimu yetu.

6 Alimpa jina kubwa sana Mheshimiwa Mkapa baada ya yeye kuondoka kwa sababu alichokifaya kilibainisha tofauti ya tawala hizi mbili katika mambo mengi.

Naomba mwenye mazuri mengine tuendee kuchangia.
kuweka udini kwa kigezo cha matukio machache ni kupotosha uhalisia wa mada yote. Udhaifu wa kila kiongozi unadhihirika pale utawala wake unapofika hatamu. Nyerere alichukuliwa kama mungu mtu lakini hii ilikuwa hivyo maana hakukuwa na mwingine wa kumlinganisha nae na haimaanishi hana mazuri yake ila kuja kwa Mwinyi kukafanya mapungufu ya Nyerere kubainika.

Alipokuja Mkapa na mfumo wake kulimfanya Mwinyi aonekane muharibufu pasi kutambua kuwa uwezekano wa maboresho kwa Mkapa ulitokana na uasisi wa Mwinyi.

Kikwete alikuja na muonekano wa kuwa mkombozi na kuna ambayo ameyafanya kupelekea Mkapa kuonekana alikuwa bepari na muuza viwanda pasi kutambua pia ni kupitia kwa aliyofanya Mkapa, Kikwete akaweza kusogea mbele.

Amekuja Magufuli leo hii, mapungufu ya Kikwete yanaonekana ila kuna swali moja tu la kuuliza je kama Magufuli asingepewa nafasi ya kuwa waziri katika awamu zilizopita tungemjua leo?
Point yangu ni moja tu, kuwa kila kiongozi alielipita ni muasisi wa muendelezo wa anaefuata. Leo hii tusingekuwa tunajadili mema ya Mwinyi kama Nyerere angeng'ang'ania madaraka.
 
Hata mkikesha mnajaribu kumchambua nyerere bado hamtaweza kumuharibia yale mazuri aliyo yafanyia watanzania na bado hatujapata kiongozi mwenye uthubutu wa kutenda kama nyerere
Nani anamuharibia sisi au Tundu Lissu maana haya mi nimeyatoa kwa Mwanasheria mkuu wa Chadema.
 
Wengi wao ni watu wa Tanga

Now naelewa why Tanga iliachwa nyuma kimaendeleo

what about YASIN MEMBA?
Kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, kuna watu walioona kuwa hawaridhishwi na Serikali ya Mwalimu Nyerere, hasa vijana kiasi cha kujasiria hata kuteka ndege ya abiria kwa lengo la kuishinikiza Serikali kufuata matakwa yao. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Boeing 737, ilitekwa mjini Mwanza na vijana watano wa Dar es Salaam.

Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba.

Kama utakuwa na muda takupa dondoo kiduchu.
 
KIkubwa alichofeli ni KUKUSANYA KODI na ndipo ilimbidi Mkapa alipoingia aanzishe TRA.

RUKSA RUKSA ilikuwa RUKSA kwlei kweli watu walikuwa wanahela mbaya na vitu vilipatikana kwelikweli.( Mfano w ahili ni show ya Kanda Bongo Man ndani ya Kilimanjaro Hotel Miaka hiyo ya 90 kiingilio ilikuwa 100,000/= na bado ilijaza)

Nyerere alimpiga dongo sana kuwa anashahuriwa na Mkewe au tuseme wake zake.
T.R.A alianzisha mkapa?..muwe munafuatilia mambo,
 
Mzee Mwinyi alikuwa akimsikiliza Nyerere wala habishani naye wala hagombani naye lakini inapokuja kwenye kufanya maamuzi anafanya maamuzi kwa jinsi yeye anavyoona inafaa!
rejea usemi wake,mwendawazimu akichukua nguo wakati unaoga,ukatoka kumkimbiza utaonekana wewe ndio mwendawazimu,mtu kakalia kiti robo karne,huduma muhimu hakuna,wewe unawezesha hlo,unaambulia kusutwa na kuzodolewa
 
Gulwa.

Nyumba ya Mzee Mwinyi mbona ya kawaida kabisa wafanyakazi wengi tu wa serikalini wana nyumba nzuri kuzidi hiyo.
Nazungumzia nyumba inayojengwa masaki nyuma sea cliff bado haijaisha, ile unayosema wewe kajenga mwenyewe kwa pesa yake
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
Kuwa Mhalisia Bandugu, hata kama umpendi. Ni wakati ambao wananchi wa kawaida waliweza kuwa na pesa za matumizi na maendeleo. Hali ikawa mbaya alipokuja Mzee wa Masasi. JK(Kijana wa Msoga) akaja akarekebisha hali, watu wakapata maendeleo. Sijui huyu wa leo atatufikisha wapi. Kila kitu kwake NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
 
Nchi ilikuwa na haki mbaya hili jamani acha!Vijijini watu walikua wanavaa magunia na mifuko ya simenti,,,kunguni na chawa vilikua sehemu ya mwili wa mwanadamu,,,Mwinyi aliistaarabisha nchi hii sema watu wamesahau tu
Unakuta watu wamekaa kama wanasukana, eti anamtoa mwenzake chawa kichwani..! Na lilikuwa ni jambo ambalo halishangazi"!
 
Tuliweza kupata video..ambazo kabla lazima uwe na kibali maalum
Tuliweza kununua magari...kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa wengi
Kwa ujumla bidhaa zilianza kupatikana ...sinta sahau Stella Artois
 
Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.

Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.

Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
Na ukizingatia serekali ndo ilikuwa inafanya biashara kuanzia uzalishaji usambazaji hata uuzaji rejareja, kodi alilipa mtumishi wa serekali tu. Nyuma kdg kila raia alitakiwa kulipa kodi ya maendeleo (ya kichwa)
 
Back
Top Bottom