Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Udini ulete wewe tu hapa ni elimu bila malipo,Nyerere kaongoza kuanzia miaka ya 60,vita ya Kagera miaka ya 78 miaka takriban 6 mbeleni ndioMwinyi kaingia madarakani sasa aliikuta nchi imeyumba na vita ipi ya Vietnam au wapi?

Sio kila mada ya kuchangia ndio maana wengine tunasoma tu na kutoa like hii ilimu tunawaachia akina Ritz.

Hueleweki unataka kusema nini. Hebu rudia tena!
 
Kuwa Mhalisia Bandugu, hata kama umpendi. Ni wakati ambao wananchi wa kawaida waliweza kuwa na pesa za matumizi na maendeleo. Hali ikawa mbaya alipokuja Mzee wa Masasi. JK(Kijana wa Msoga) akaja akarekebisha hali, watu wakapata maendeleo. Sijui huyu wa leo atatufikisha wapi. Kila kitu kwake NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

Kwahiyo mnataka upigaji uendeleee kweli bongo mufilisi
 
Kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, kuna watu walioona kuwa hawaridhishwi na Serikali ya Mwalimu Nyerere, hasa vijana kiasi cha kujasiria hata kuteka ndege ya abiria kwa lengo la kuishinikiza Serikali kufuata matakwa yao. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Boeing 737, ilitekwa mjini Mwanza na vijana watano wa Dar es Salaam.

Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba.

Kama utakuwa na muda takupa dondoo kiduchu.

Most interesting thing ni kuwa that was back in 80's if im not mistaken
Hao vijana walikuwa in their early and mid 20's
WOTE walikuwa ni vijana wa Kiislam (based on majina)
What does that tell you?
Does this mean kuwa pamoja na kuwa vijana wa miaka hiyo walikuwa hawana twitter or internet lakini waliamka au how did they knew kuwa Nyerere alikuwa anaturudisha nyuma?

Je walikuwa wanatoka Tanga au maeneo mbali mbali ya nchi?
 
Kumbe wlaikuwa magaidi!. Magadi na utekaji wa ndege ni samaki na maji. Wanajulikana wala usihangaike.
 
Kwa ufupi tu Nyerere alitinyanga Mwinyi akaweka sawa,Mkapa akaharibu tena JK akarekebisha sasa sijui awamu hii wasije kumpa tabu tu Membe au January Makamba.

Dah...kuna watu mna mahaba mpaka mnapitiliza kwahiyo mzee wa msoga ameweka sawa kwenye upigaji
 
Kwa kwlei ukiwa na haiba ya ugaidi lazima uwe mbweha. Hivi uchangiaji a hapa unauvalidate namna gani hadi kudhania ni uwakilish sahihi wa ukweli halisi?

Sasa uende shule ya kikweli ukajifunze haya masuala maana umezidi kutia aibu. Au hii ndiyo analysis ya elimu kuzimu?
 
Mkuu wewe mwenyewe umesema hiyo nyumba ipo nyuma ya Sea Cliff nimekuwekea picha tumeona Sea Cliff ipo baharini tena Peninsula.

Sasa hivi unasema ipo karibu na jiko la Sea Cliff na Store daaah!!

Mkuu hivi unajua maana ya Peninsula?
we una asili ya ubishi, hutaki kutafuta ukweli
 
Kuwa Mhalisia Bandugu, hata kama umpendi. Ni wakati ambao wananchi wa kawaida waliweza kuwa na pesa za matumizi na maendeleo. Hali ikawa mbaya alipokuja Mzee wa Masasi. JK(Kijana wa Msoga) akaja akarekebisha hali, watu wakapata maendeleo. Sijui huyu wa leo atatufikisha wapi. Kila kitu kwake NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

Kwweli mbweha ni mbweha hata akivaa kanzu. Wewe watu wanalia na ufisadi uliokithiri kumbe wewe kwa ko ndiyo marekebisho?

Ndiyo maana mmerundikana kwenye wakwepa kodi, watorosha makontena bandarini na waingiza malori kibao kwa jina la kusalia. Mmezowea vya kunyonga. Sasa tumewashtukia na hatuwapi nchi tena!

Watu wanahangika makisha magumu, wizi kila mahala huduma muhimu hakuna, nini wacheza bao mnahujumu uchumi halafu bila haya hata huoni unasifia hadharani!. Tumewatambua... Tanzanai si ya mafisadi na wapenda hujuma.

Sasa utasubiri sana mtu wa kutuharibia nchi kwa manufaa ya wacheza bao, hutampata tena!!!!! nakuambia.
 
Wapi nimebisha mie nimeuliza tu! Wewe umesema Mzee Mwinyi kajengewa nyumba kubwa ya bilioni 9 ipo nyuma ya Sea Cliff.

Nikauliza ili kupata kujua mbona nyuma ya Sea Cliff kuna bahari.

View attachment 346019

Hiyo barabara ndiyo yakuingilia Sea Cliff mkuu.

View attachment 346020
Mkuu ukiingia Sea Cliff ndiyo pako hivi huko nyuma kuna bahari ni Peninsula.

Labda tufahamishe huyo nyumba ya Mzee Mwinyi ipo kwa sehemu gani mkuu wangu.

Nakala: FaizaFoxy
Muhammad-Ali.jpg
 
Most interesting thing ni kuwa that was back in 80's if im not mistaken
Hao vijana walikuwa in their early and mid 20's
WOTE walikuwa ni vijana wa Kiislam (based on majina)
What does that tell you?
Does this mean kuwa pamoja na kuwa vijana wa miaka hiyo walikuwa hawana twitter or internet lakini waliamka au how did they knew kuwa Nyerere alikuwa anaturudisha nyuma?

Je walikuwa wanatoka Tanga au maeneo mbali mbali ya nchi?
Hao vijana wa wakati ule wanatoka maneo tofauti nadhani siyo vyema kuangalia majina yao na kuwajadili kama Waislam maana hata wanajeshi waliyota kumpindua Mwalimu Nyerere walikuwa na majina ya Kikristo lakini tuwajadili kama Watanzania siyo dini zao.

Takupa hiki kisa cha watekaji ndege kiduchu.

Baada ya maagano na ndugu, jamaa na marafiki, abiria walipanda katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania iliyokuwa na jina la Kilimanjaro, Boeing 737, kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Ijumaa ya Februari 26, 1982, saa 11 jioni.Uwanja wa ndege wa Mwanza ulikuwa na sifa mbaya kwa sababu haukuwa na usalama kiasi kwamba baadhi ya marubani walikuwa wakiutaja kama ‘kituo cha basi.’Makundi yaliyokuwa uwanjani hapo yalikuwa ya kawaida kama ya siku zote kwa wasafiri wa kwenda Dar es Salaam. Wasafiri wengi walikuwa ni Wahindi, Waarabu na Waafrika wachache. Ingawa mambo yote yalionekana kuwa ya kawaida, jambo dogo liliifanya safari hiyo isiwe ya kawaida.

Ndege ya Kilimanjaro ilipaa angani kutoka uwanjani hapo saa 11.20 jioni ya siku hiyo kwa kile kilichotazamiwa kuwa ni safari ya dakika 90 - maili 500, kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.Lakini ikageuka kuwa safari ya juma zima - maili 9,500 - na kwa wakati mwingi abiria wa ndege wakisafiri ‘chini ya mtutu wa bunduki’ kabla ya kuwasili Dar es Salaam.Dakika tano tu baada ya ndege kupaa angani, vijana wanne walisimama ghafla kwa wakati mmoja. Mmoja wao alijipenyeza ghafla katika chumba cha rubani, halafu akaelekeza ‘bastola’ yake kwenye kichwa cha mmoja wa marubani wa ndege hiyo, Kapteni Deo Mazula, na kumtaka awapeleke kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Wakati huo huo, watekaji nyara wengine, huku wakipunga ‘bastola’ zilizotengenezwa kwa vigogo vya miti na ‘mabomu’ ya kutupwa kwa mkono, waliwatangazia abiria kuwa wao ni viongozi wa ‘Vijana wa Harakati za Mapinduzi Tanzania’ na kwamba shabaha yao ni “kuhakikisha kuwa Rais Julius Nyerere anajiuzulu.”Wakati hayo yakitokea, Rais wa Tanzania waliyemtaka ajiuzulu, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa Ikulu mjini Dar es Salaam akijiandaa kurudi nyumbani baada ya kupokea risala kutoka kwa Chipukizi nchini waliomwahidi kuwa “Tutaendelea kuwa watiifu, wakakamavu na wenye bidii kwa kuwa tunafahamu mchango wetu unahitajika sana katika ujenzi wa nchi.”

Mpaka wakati anaondoka kwenda nyumbani kwake, Msasani, akiwa amefurahishwa na risala aliyosomewa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chipukizi, Frank Uhahula (15) wa darasa la saba katika Sule ya Mingi ya Tumbi, Kibaha katika mkoa wa Pwani, Mwalimu Nyerere hakuwa amejua kilichotokea upande mwingine wa nchi -Mwanza.Watekaji nyara hao waliwaamuru abiria wote wakae kimya kwenye viti vyao na kufumba macho yao na, kwa sababu ambazo hazikujulikana lakini za kustaajabisha, waliwalazimisha watumishi kuzima viyoyozi vya ndege. Wakati hali ya hewa katika ndege hiyo ilipoanza kuwa nzito na kukaribia kutovumilika tena, ndege hiyo ilitua mjini Nairobi kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Lakini katika kipindi cha dakika kadhaa baadaye, Rais Nyerere alipewa taarifa za kutekwa kwa ndege hiyo na kuambiwa kwamba tayari ilishatua Nairobi, Kenya. Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, John Samuel Malecela, ambaye aliteuliwa rasmi kushughulikia utekaji huo, alitumwa kwenda Nairobi kushughulikia tatizo hilo. Mwalimu Nyerere alitaka kuwa na hakika kwamba Serikali ya Kenya haingeruhusu ndege hiyo iondoke Nairobi.Wakati huo huo polisi wa Kenya wakifunga uwanja wa Ndege wa Kenyatta, na wanajeshi walisambazwa uwanjani hapo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Robert Ouko, alikuwa uwanjani hapo akitokea Addis Ababa, Ethiopia, wakati ndege ya Tanzania ilipotua.Alipopewa habari za yaliyotokea, Dk Ouko hakusita, alikwenda kwenye chumba cha kuongozea ndege kujaribu kushughulikia jambo hilo.

Hii habari ndefu nadhani tawachosha tunaendelea muda mwingine.
 
Mkubali msikubali siyo wewe tu,bali na mwenzako Fayza Fox na The big show, nyerere ndio atabakia kwa ni kielelezo cha viongozi walio wahi kuwa bora kabisa hapa tanzania
mkuu ni sawa sawa kumlinganisha didier drogba na didier kavumbagu. mwl nyerere alikuwa alikuwa wakimataifa na mpaka leo anaheshima kubwa sana ndani na nje ya nchi, mpaka mzee mugabe anaandika kitabu kumuhusu. ukisikiliza hotuba za mwl nyerere utaona jinsi alivyo kuwa na upeo mkubwa. sasa wanasahau mwl aliichukua nchi ilikuwa katika hali gani katika nyanja zote hata wataalam alikuwa nao wachache sana akafanya juhudi za kusomesha.

wakati anajaribu kuiweka nchi kwenye mstari kuna ibuka vita na uganda lakini bado mzee wa watu hakushindwa wala kukata tamaa na ikumbukwe alikuwa na maadui wengi wa ndani na nje.
 
Luksa maana yake "holela". Kama ndicho hicho unamaanisha tuko wote. Lakini pia kwa nyongeza, wakati wa Mwinyi ndipo:-

1. Vita ya maguruwe ikiongozwa na ustaadhi Rashid sijui nani iliibuka na kuzimwa na ushupavu wa Augustin Mrema.

2. Nicho kipindi shule za Kikristo zilichomwa moto na kupoteza uhai wa watoto wengi wasiokuwa na hatia.

3. Hapo hapo ndipo tuliona urasmishaji wa makundi ya balukta, wenye surualil fupi.

4. Wakati ule ndipo makundi ya mujahidina yalifahamika rasmi.

5. Waraka wa Kigoma Malima ulioasisi ukakasi kwa elimu yetu.

6 Alimpa jina kubwa sana Mheshimiwa Mkapa baada ya yeye kuondoka kwa sababu alichokifaya kilibainisha tofauti ya tawala hizi mbili katika mambo mengi.

Naomba mwenye mazuri mengine tuendee kuchangia.
sikukuu itayo kuwa jumamosi au jumapili basi ilikuwa luksa kuwa na mapumziko jumatatu . ilikuwa ni kipindi cha kubweteka na naona ndio chanzo cha uvivu
 
Back
Top Bottom