Legacy ya Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete

nimeamini shilingi ina pande mbili, leo mnataja mema yake ila mababaya yake hamsemi
 
Hujui kitu kuhusu Kikwete kaa kwa kutulia huyo ni Iconic figure ya Tanzania
 
Merermeta,IPTL,mapesa ya gadafi,kuuza gesi yetu ya mtwara Kwa mabeberu na sisi wananchi kuuziwa bei ya juu zaidi ya mara saba ya bei wanavyonunua mabeberu,kugunduliwa Kwa mafuta Zanzibar na kuyatoa kwenye masuala ya muungano ili Zanzibar inufaike peke yake,kuuza shirika reli Kwa wahindi na baadae magufuli kuliokoa,kuua shirika la ndege na kubakiza Moja mikweche,kuongezeka Kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na madudu mengine mengi
 
Well.

The same ana regancy ya mambo yafuatayo.
- aliasisi siasa za vurugu,kejeri,na kukomoana
-mafisadi mlipata uhuru haijawahi na haitatokea
 
Mnazi bay ni eneo moja, gesi mtwara inachimbwa maeneo mengi. Ndio wanaosema imeuzwa sababu hatuna umiliki maeneo mengi, mm sipendi kusema imeuzwa sababu hatuna uwezo wa kufanya tafiti wala kuchimba
Maeneo mengi mengine yapi?..kampuni gani inachimba huko
 
Gas gani ya mtwara imeuzwa wazee?.. mbona mnaimba vitu kikasuku?
 
Bora ume Wakumbusha mkuu hawa wapumbavu!

Magufuli pamoja na ukali wake hakuwahi kutumia mabomu ya kivita ila JK aliyatumia pale Olasiti Arusha
 
Maeneo mengi mengine yapi?..kampuni gani inachimba huko
Zipo kampuni nyingi zinachimba gesi huko. BG, ophir, Exxon n.k
Tpdc ananunua kwao, alafu tpdc anaiuzia tanesco. Tanzania haina umiliki sababu haikuwekeza kwenye utafiti na uchimbaji.

Kama unavyoona gas ya lindi ambayo tunataka tuwape Exxon, mradi gharama yake ni Trillion 100. Hiyo pesa hatuna ndio tunawapa hao, wanatafiti wanachimba wakianza uzalishaji wanatuuzia sisi na wanauzia wengine. Kwa kifupi hatuna uwezo wala pesa
 
JK ni mfano wa mtu wa kuigwa kuvumilia maneno pinzani na kujikita kutimiza wajibu bila kumuumiza mpinzani.

Hakuna mkamilifu dunian, JK apewe heshima yake.
Mwanahalisi washawahi andika "Vasco Dagama" safarini ughaibuni, na halikuwahi kufungiwa!!! Jamaa ni mvumilivu na anajua sana Siasa!! Diplomasia!!
 
Ila chama kilikua kina karibia kuteketea mikononi mwake na kwa mara ya kwanza tulikua tunakaribia civil unrest.

Kama yale yaliyokuwa yanaendelea kwake yangeendelea kufanyika kwa miaka mingine mitano tu, watu wangeingia barabarani.

Matajiri walikua wachache wenye ukwasi mkubwa sana na rundo la maskini wasiokuwa na future.

Falsafa ya Magu ilipoza hasira za wanyonge na kutengeneza hali ya usawa mambo yakapoa kidogo.

Samia nae akisema aige staili yake naamini baada ya muda raia watashindwa vumilia.

Cha kufanya kwa Samia, achague kuwa karibu na wananchi, ziara kama hizi za mikoani aziongeze watu wamuelewe.

Asijifungie ndani tu na kukutana na hao mabwanyenye, aende kwa watu wa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…